Tulioletewa bili za ajabu za maji ya DAWASA tukutane hapa

Fernando sucre

JF-Expert Member
Jul 14, 2018
293
344
Wakuu hivi hawa DAWASA hizi meter zao wamezitemptor? Majirani zangu nilikuwa naona wanalalamika wanaletewa mabili ya ajabu nikaona labda matumizi yao.

Jana wakanitumia bili yao, toka bili ya 5000 to 40000? Tena ya Desemba wakati kipindi hicho watu wengi walikuwa wamesafiri? Je, mliopata shida kama hii mlifanyaje?
 
Tulilipa hiyo 40,000 halafu bill ikarekebishwa mwezi uliofuata.

Hiyo ni mbinu ya Dawasco kuweza kuvuka malengo ya mwezi na labda kulipa Gawio la serikali kama bado hawajalipa kwani mwisho ni January 31!

Dawa yao ni kuwapeleka mahakamani kwa Wizi wa udanganyifu.

Mjikusanye wote mlioletewa bill za aina hiyo muende kwao kutafuta ushahidi ndipo mumtafute Wakili atakayesimamia kesi yenu hapo ndipo watakoma vinginevyo hawawezi kuacha mchezo huo unaoathiri bajeti za watu kipindi hichi cha vyuma kukaza.--- na kwanjia hiyo watu wengi wanaibiwa kwani sio wote hupeleka malalamiko yao na wala hawajui kulalamika au muda wa kulalamika hawana.

Jambo jingine watu wengi huwa hawana muda wa kusoma mita zao nyumbani au watu wengi hatujui jinsi ya kusoma mita, hiyo ni shida nyingine.
 
Nani huyo ambae hana kazi ya kufanya

Kazi ya kufanya ndiyo hiyo ya kupambana na Kibaka wa pesa za bili ya maji,--- wenye pesa haramu hawatakuwa na muda lakini wale wenzangu mie wa kuuza maandaazi kujikimu kimaisha--- Tsh 40,000 for water bill charge a month is a hell . Na mbaya zaidi imekuwa ni tabia yao ku over charge.
 
Kuna mtu anauza maji anasema kuna wakati alipigwa bili kubwa zaidi kabisa ya alivyouza, kama mara tano ya kawaida (huwa anarekodi kwenye kidaftari mauzo yote)

Alivyolalamika wakasema tatizo wanamwaga sana maji, eti pale bombani haitakiwi paloane.

Aliwaomba waangalie vizuri ili alipe kama miezi mingine, lakini jamaa wakasema asiwe na wasi, awe analipunguza taratibu kila mwezi hadi atamaliza.

Sasa hivi kwa mujibu wa hesabu zake anasema ni kama anawafanyia kazi ya kuuza maji wao kwa ajili ya deni.
 
Dawa yao ni kuwapeleka mahakamani kwa Wizi wa udanganyifu.

Mjikusanye wote mlioletewa bill za aina hiyo muende kwao kutafuta ushahidi ndipo mumtafute Wakili atakayesimamia kesi yenu hapo ndipo watakoma vinginevyo hawawezi kuacha mchezo huo unaoathiri bajeti za watu kipindi hichi cha vyuma kukaza.--- na kwanjia hiyo watu wengi wanaibiwa kwani sio wote hupeleka malalamiko yao na wala hawajui kulalamika au muda wa kulalamika hawana.

Jambo jingine watu wengi huwa hawana muda wa kusoma mita zao nyumbani au watu wengi hatujui jinsi ya kusoma mita, hiyo ni shida nyingine.
point hii sana
 
Kazi ya kufanya ndiyo hiyo ya kupambana na Kibaka wa pesa za bili ya maji,--- wenye pesa haramu hawatakuwa na muda lakini wale wenzangu mie wa kuuza maandaazi kujikimu kimaisha--- Tsh 40,000 for water bill charge a month is a hell . Na mbaya zaidi imekuwa ni tabia yao ku over charge.
Asante mkuu umemaliza
 
Wakuu hivi hawa DAWASA hizi meter zao wamezitemptor? Majirani zangu nilikuwa naona wanalalamika wanaletewa mabili ya ajabu nikaona labda matumizi yao.

Jana wakanitumia bili yao, toka bili ya 5000 to 40000? Tena ya Desemba wakati kipindi hicho watu wengi walikuwa wamesafiri? Je, mliopata shida kama hii mlifanyaje?
Mimi ni mhanga,lakini siko Dar,na nilikuwa likizo December,bili imeongezeka kutoka 3,000 wameniletea bili 40,000...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kifupi wasoma mita ni wezi sana wakishirikiana na wahasibu, hizi bill huwa wanazifanyia mchezo na kuwapiga wateja kisha zile unit za ziada wanakula wao.

Kiukweli hili suala la wateja kubambikiwa extra payment ni donda sugu, nimepiga kelele pale Dar Es Salaam ofisi za Dawasco tegeta, umfano, unatumia 12unit wanakuletea bill ya 45,000 hapo unaweza kubadirika rangi..!!.
 
Mimi kuna wakati walianzisha mchezo wa kunipandishia bili "eksponenshale" yaani mwezi huu ikija 20,000 mwezi ujao inakuja 40,000 then 60,000 sasa mi nikawa nazitunza zile meseji mpaka ikafika 140,000 nikaona huu ujinga, nikawaibukia ofisini na vielelezo vyote pamoja na barua kali kwa meneja! Mwezi uliofuata ikaja 13,000 na mpaka leo ni zaidi ya mwaka haijawahi kuzidi 16,000
 
Back
Top Bottom