Tatizo la mita za kusoma maji, DAWASA toeni ufafanuzi wa kueleweka, mnawanyonya na kuwaibia wananchi

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Wakuu kwema?

Suala la mita za DAWASA limekuwa ni changamoto na kero kubwa kwetu watuamiaji, na si kwamba ni watu wachache, malalamiko ni mengi ikiwemo na kwangu mdau lakini DAWASA wanakaza shingo.

Nilishangazwa na mhudumu wa DAWASA kuona ni jambo la kawaida kwa familia ya watu watatu kuletewa bili ya unit 15-20, hawana biashara yoyote ya kuuza, muda mwingi wapo kazini, hakuna leakage na anaona ni kawaida tu kupokea bili hiyo, nikaacha hata kubishana nae, kama anaona hilo ni sawa.

Mimi bili yangu ilianza kushoot nikaletewa bili ya unit 12, mara ikaenda 15, iliyofuata ikaja unit 21! Hapo naishi mwenyewe, siku nzima inatumika kwenye shughuli za kujiingizia kipato, weekend kufua ni nguo hizo zilizovalia kwa wiki nzima, sijawahi kuacha bomba wazi hata siku moja, naweza sikae hapo kwa wiki au hata wiki mbili lakini bado nikaletewa bili hiyo!

Kuwatafuta DAWASA kwanza walinijibu kwa nyodo, nilipoendelea kuwasumbua waliniletea mtu wa kucheki mita, walipocheki wakasema hakuna leakage shida itakuwa kwenye matumuzi yangu au jirani yangu atakuwa anatumia maji upande wangu (mimi na jirani yangu tuna mita tofauti, jirani ni familia ya watu wanne na watoto wawili).

Nikamwambia hatushei maji, na hata tungekuwa tunashea bado bili hii ni kubwa kwetu wote kwa matumizi ya kawaida, ukizingatia hata wao wanaoshinda siku nzima ndani hawazidi wata watatu. Ndio huyo muhudumu akanipa majibu hayo kwamba jirani yake alikuwa anatumia maji yao baada ya kuwadhibiti sasa hibi wanatumia uniti 15-20 kwa mwezi, na anaona kupata bili hiyo ni sawa kabisa!

Nimesikia fununu kuwa DAWASA wanataka kubadili mita hizi kwasababu zina mtatizo na ndio chanzo cha kuleta bili hizi ambazo haziendani kabisa na matumizi ya watu na hivyo kuongeza mzigo kwa wananchi.

Kama ndivyo kwanini hawatoi taarifa kwa umma na bado wanaendelea kutuletea bili hizi za kipuuzi kwa makusudi? Sawa, mwenye uwezo anaweza kulipa huku akiwa na manung'uniko, lakini vipi kwa ambaye hana uwezo huo? Unampelekea bili hiyo mtu wakati unajua fika unamuonea na akishindwa kulipa unamuondolea hudumuma hiyo, hii ni haki?

Au mnataka wote tuanze kuwa wakorofi mkija kusoma mita tuwe tunashikana mashati?
 
Mimi yangu inachezea 30000 hadi 35000 watu watatu wazima watoto wawili. Kuna kipindi ilifika 55000 nikalalamika wakaibadilisha meter kwa sharti la kwanza nlipe bill hiyo
 
Bypass kula mzigo! Ikijaa rudishia! Dawa ya moto ni moto! Sipendagi ujinga!
Unajua kuna baadhi ya taasisi za kiserikali huwa unatamani kama mnufaika direct wa huduma ulipe kadiri ya unavyotumia lakini unakuta wana errors za kukera sana kiasi zikafanya uwafanyie uhuni.

Hawa hawa DAWASA kuna kipindi system yao ilifanya vitu vya ajabu kwa kutuma randomly bill za watu wasiohusiana yaani bill ya yule ikaja kwangu ya kwangu sijui ilikutana na nani na nilishailipa sijui aliyeiona aliielewa vipi kilichoniokoa muda mfupi nyuma nilikuwa nimetoka kulipa bill yangu sahihi kama siyo hivyo ningesoma ujumbe wao kwa wenge nikachukua control # na kulipa ningemlipia mtu deni bila kujua,yaani ndani ya ½saa nilipata text zaidi ya hamsini za madeni ya mita nisizozijua mwisho wakaniomba msamaha lakini bado wakinisisitiza kudaiwa wakati nimeshalipa.

DAWASA badilikeni acheni mazoea kwenye pesa za watu sisi pesa hatuokoti
IMG_20240102_231250.jpg
 
Back
Top Bottom