DAWASA- kufanya hujuma kuibia wananchi "meter" za maji kisha kuja kutoza gharama za ufungaji wa mita hiyohiyo iloibiwa ni dhuluma

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,398
Moja kwa moja kwenye mada.

Kwanza naomba JF isiutoe uzi huu kwani mada hii nafikiri ni muhimu sana kwa mstakabali wa wateja wa DAWASA ambao huko mitaani wamekosa wa kuwasemea.

Natambua kuna uzi humu kwa ajili ya DAWASA lakini nimeufuatilia na nimejiridhisha kwamba hauna response nzuri kutoka DAWASA.

Hivyo nimeamua kuweka hii mpya ambayo ndo habari ya mjini kwa sasa, wizi au uharibifu wa meter za maji katika makazi ya watu.

Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za wananchi ambao ni wateja wa DAWASA kuharibiwa kwa makusudi au hata kuibiwa meter za maji kutoka majumbani.

Wezi hao huruka ukuta kuingia ndani ya nyumba za wateja na kufungua meter hizo kisha kuziacha ili mjai yamwagike.

Wale ambao huibiwa meter hizo huja kuuziwa mita hizohizo ambapo kabla ya kufungwa upya mafundi wa DAWASA mtea huambiwa apewa siku kadhaa na atahitajika kulipa kiasi cha shilingi 50,000 au zikizidi siku hizo gharama hupanda hadi kuwa kiasi cha shilingi 200,000.

Kama meter hurabiwa na vijana wanofahamiana na mafundi ambao hupeana nao michongo basi maji huvuja na hata mteja akitoa taarifa kuwa mita imeharibika na maji yavuja na mteja kuamua labda kukinga ndoo mbili tatu huku akisubiri mafundi waje, kuna uwezekano mkubwa mteja huyo akatishiwa kupelekwa mahakamani kwa wizi wa maji.

Kwanza mwizi yoyote wa maji hana haja ya kutoa taarifa DAWASA kuhusu uharibifu wa meter na pili, mteja huyo aogopa zoezi zima la kukutwa amevuna maji yalokuwa yavija. Pili, kitendo cha maji kuwa yavuja wakati yakisubiri mafundi waje kwaweza kusababisha maafa mengine kama mafuriko na uharibifu wa mali za mteja.

Taarifa hizi za wizi au uharibifu wa hizi meter zipo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar-es-Salaam na DAWASA wanazo. Ningependa kuwaomba wasimamizi au mameneja wa DAWASA katika maeneo yao wajaribu kufuatilia hili kwani ni dhuluma.

Katika miaka hii miwili tatizo la maji limerudi katika hali yake ya zamani ya wananchi na wateja kuwa wanakosa maji ambao ni moja ya mahitaji ya msingi kabisa kwa mwanadamu. DAWASA ina wajibu wa kujisikia aibu na kujaribu kuepusha kadhia hii ya kuendelea kuwasumbua wananchi kwanza kwa kuwakosesha huduma ya maji na pili, kuwadhulumu fedha zao kwa kutofuatilia vitendo viovu vya baadhi ya watumishi wake waso waaminifu ambao hushirikiana na wezi kuharibu au kuvunja meters za wananchi.

Ningependa kutoa ushauri kwa DAWASA kuwasaidia ushauri wateja wao kwa kuhakikisha wananchi wazijengea meter hizo uzio wa tofali mbili au nne eneo linozunguka meter hizo na kuweka kufuli au komeo na kuacha eneo la kusoma meter hizo na siku DAWASA wakitaka kuja kusoma meter hizo basi hutoa taarifa kwa mteja ambae ataweza kufungua eneo hilo kwa ajili ya ukaguzi au kusoma meter.

Pili, kwa wateja wote DAWASA ni jambo la uzuri kuhakikisha katika ujenzi wa uzio wa nyumba zao wana busdi kuacha sehemu ndogo kwa ajli ya kuweka meter ambayo itakuwa yasomeka nje tu lakini iliyojengewa kwa ndani ya uzio ili pia kuzuia vitendio cha kujaribu kuvunja na kuiba meter hiyo.

DAWASA ni kampuni kubwa inoshughulika na maji safi na maji taka hivyo ni kampuni yenye uzoefu mkubwa na huduma za maji mijini.

DAWASA ina wajibu wa kuhakikisha inafanya kazi zake kitaalam na pia kuzingatia wateja wake maana wao ndo wanoifanya iwe yajiendesha kwa fedha zao wanozilipia.

Kuhakikisha wateja wahudumiwa ipasavyo ni moja ya majukumu ya kampuni katika kutekeleza kitu ambachio chaitwa "corporate responsibility" yaani kampuni kuwajibika kwa kuleta mabadiliko katika utoaji huduma zake kwa wananchi na jamii kwa ujumla, kuwajibika kwenye mazingira na kiuchumi pia.
 
Unaambiwa Serikali ina mkono mrefu. Unakumbuka nahau ya "ana mkono mrefu, maana yake?".
 
Back
Top Bottom