Tulimcheka Kikwete kumbe wengine wapo!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
IMG_0605.JPG

Meneja Uhusiano wa TBL,Edith Mushi (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milion 4.8 kwa Mwenyekiti wa TASWA FC,Majuto Omary kwa ajili ya mashindao ya Bonanza huko mkoani Arusha.katikati ni Afisa Uhusiano wa TBL,Lilian Erasmus.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imetoa sh. 4, 875,000 kwa timu ya soka ya Waandishi wa Habari za Michezo Nchini (TASWA FC) kwa ajili ya kushiriki katika bonanza la waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha.
 
Mi nadhani pamoja na sababu nyingine, pengine lugha inayochechemea pia ni sababu inafanya watu washindwe kusema kile wanachotaka kukisema katika maandishi.
 
Sasa hapo kama wewe ndiye mtu wa benki unayetoa hizo pesa kutoka hiyo akaunti ya TBL utatoa kiasi gani ?

Nchi yetu ina matatizo katika hesabu na kiingereza, hili nalijua, lakini hii ni level mpya. Au wahasibu na walioandika kwenye cheki walikuwa tayari washaonja matunda ya kazi yao hapo TBL (Kilaji)

This one is for the books, I am sorry.It would've been be funny if it wasn't so tragic.

Yaani mijitu yote hiyo haijaona kitu, mpiga picha hajaona kitu, publishers hawajaona kitu ?
 
Duuh..... lol, sikumbuki vizuri, sijui ile nyingine ilikuwa cheque inayotoka T. Breweries au kampuni mojawapo ya simu... hebu ngoja niisake ile thread :)
 
Mi nadhani pamoja na sababu nyingine, pengine lugha inayochechemea pia ni sababu inafanya watu washindwe kusema kile wanachotaka kukisema katika maandishi.

Walishindwa nini kuandika hundi hiyo kwa lugha ya Kiswahili??!!
 
Walishindwa nini kuandika hundi hiyo kwa lugha ya Kiswahili??!!

Mara nyingine tatizo wala si lugha, hata Kiswahili tunachotumia mara nyingi tu kina matatizo.Ni rahisi kusingizia Kiingereza kwa sababu ni lugha ya kigeni, lakini ushajiuliza nani anajua kuisema Roman Alphabet yote kwa Kiswahili ?
 
Walishindwa nini kuandika hundi hiyo kwa lugha ya Kiswahili??!!

Hapo sasa ndio nami najiuliza. Kulikuwa na ugumu gani kuandika 'shilingi milioni nne na laki nane tu'....

Sisi tunashangaza sana wakati mwingine. Tunalazimisha vitu pasipo na ulazima wowote. Ulazima wa kuandika kwa lugha ya Kiingereza kwenye hiyo hundi ulikuwa ni upi?

Au watasema Kiswahili hakina misamiati na maneno ya kutosha kama wasingiziavyo kwenye sheria zetu zilizoandikwa kwa Kiingereza? Yaani ni uzumbukuku mtupu hadi unatia kichefuchefu.
 
Mwe...kweli kazi tunayo! Umakini ni zero kabisa.
 
Au waliandika haraka haraka kuwahi picha

Kitu chochote unachoweka sahihi hakitaki haraka haraka. Aliyetia sahihi nchi za watu wanaojali kuwajibika hana budi kujieleza au hata kuwajibishwa.

Kama hilo hundi kubwa hivyo anaboronga sijui kama anaweza kufuatilia small print za contracts zinazohitaji sahihi.
 
Hapo sasa ndio nami najiuliza. Kulikuwa na ugumu gani kuandika 'shilingi milioni nne na laki nane tu'....

Sisi tunashangaza sana wakati mwingine. Tunalazimisha vitu pasipo na ulazima wowote. Ulazima wa kuandika kwa lugha ya Kiingereza kwenye hiyo hundi ulikuwa ni upi?

Au watasema Kiswahili hakina misamiati na maneno ya kutosha kama wasingiziavyo kwenye sheria zetu zilizoandikwa kwa Kiingereza? Yaani ni uzumbukuku mtupu hadi unatia kichefuchefu.

Home boy it has been a long time since I pressed thanks in your posts, thumbs up!
 
Mara nyingine tatizo wala si lugha, hata Kiswahili tunachotumia mara nyingi tu kina matatizo.Ni rahisi kusingizia Kiingereza kwa sababu ni lugha ya kigeni, lakini ushajiuliza nani anajua kuisema Roman Alphabet yote kwa Kiswahili ?

Mazee, tunaongelea lugha rahisi tu ya kawaida inayoweza kueleweka kwa wengi wetu, nomino na misamiati ya kutosha ipo inayoweza kutosheleza hilo kwenye swala kama hili bila ya kuingia kwenye asili na vyanzo vya maneno tuyatumiayo.
 
Hii yote ni kwa sababu watu hawafanyi kazi zao vizuri, wanaofanya kazi nimimi nawewe ambao hata 5% ya watz hatufiki. wengine wanapiga domo muda mwingi ni kupeana porojo tu. Angekuwa anafanya kazi muda mrefu kwa siku lazima angekuwa makini, matatizo kama haya mtu anaweza kuyasahihisha kama anafanya kazi mara kwa mara.
 
Mazee, tunaongelea lugha rahisi tu ya kawaida inayoweza kueleweka kwa wengi wetu, nomino na misamiati ya kutosha ipo inayoweza kutosheleza hilo kwenye swala kama hili bila ya kuingia kwenye asili na vyanzo vya maneno tuyatumiayo.

Umesema sawa kabisa katika swala hili, kwamba kutumia Kiswahili ingeweza kuwa rahisi zaidi.

Mimi naongelea swala kubwa zaidi katika makosa ya lugha ya kila siku, mara nyingi watu wanapokosea Kiingereza tunakuwa rahisi kulaumu kwamba Kiingereza ni lugha ya kigeni, lakini tukianza kuangalia hata tunavyoandika Kiswahili, hata hapa JF, hatuwezi kusema kwamba hata hicho Kiswahili ambacho ni lugha yetu tunakijua vizuri.

Kwa hiyo tatizo letu ni lugha na mawasiliano, pamoja na umakini. Utasikia mtu kakosea, unamsahihisha kwa mfano, halafu anakwambia "si umenielewa?" yaani hamna umakini, hamna kutaka kufanya mambo sawa, kila mtu anataka kulipua lipua tu aende zake.

Yaani kwenye hiyo hundi tatizo si Kiingereza tu, maana nina hakika kama mtu mmoja Kiingereza chake si kizuri, lakini kama kuna utamaduni wa kupitia vitu kwa macho ya pili, ku hakiki na kadhalika, watu wangeona makosa hapo.

Lakini naona Kiingereza ni tatizo, lakini zaidi ya hilo umakini ni tatizo kubwa zaidi.Tatizo linalotufanya hata Kiswahili chetu wenyewe tusikiweze.
 
Mwe...kweli kazi tunayo! Umakini ni zero kabisa.

Sio swala la umakini wala lugha! Kwenye mahojiano na vijana wetu (kwa ajili ya kazi na darasani) usilogwe ukamuulize swali linalohusu tarakimu hata mara moja! Mwanzoni nilikuwa nawacheka lakini niligundua kumbe ni tatizo. Enzi zetu za kusoma tulikuwa tunakariri orodha ya 1 hadi 14 kama mnanipata. Halafu kukariri jinsi ya kuzitamka hizo tarakimu. Siku hizi hawafanyi hivyo, ukikutana na muuza duka kijana, ukataka soda 6 na kila moja ni shs 500/= kijana atafuta calculator. Tunawafundisha kuwa watumiaji wa mashine bila kujua kinachoendelea, tatizo ni hapo linaanzia.
 
Sasa na wewe badala ya kufagilia "kujua" vitu unafagilia "kukariri" vitu......SMH
 
Unaanza kwa kusema sio swala la umakini wala lugha, unamaliza kwa kulaumu elimu inayofundisha kutumia mashine bila kumjuza mwanafunzi nini kinaendelea katika mkokotoo.Kimsingi unalaumu kudorora kwa stadi za hesabu.

Ukishaongelea stadi za hesabu ushaongelea umakini, huwezi kuhesabu bila kuwa makini.

Kwa hiyo ingawa umeanza kwa kukataa umakini kama swala hapa, unavyomaliza unaonyesha kwamba umakini ni swala.

Hatuna umakini katika mitaala, ndiyo maana wanafunzi wanahitimu bila kujua kukokotoa na hata kutaja nambari.

Wanafunzi hawana umakini katika kujifunza, wanataka kufanya kila kitu kwa kikokotoo, hatimaye mbongo zalemaa.

Utakataa vipi kwamba umakini sio swala hapa?
 
Sasa na wewe badala ya kufagilia "kujua" vitu unafagilia "kukariri" vitu......SMH

Wenyewe wanakwambia unakariri kwanza, kuelewa baadaye!

Wakati wenzetu wanaona mishazari ya mirandano ya nambari za kijedwali, na wanaelewa anuwai, ankara na formula zinatokaje, kwa mfano kwa nini utumie pai katika kutafuta eneo la duara, kutoka historia ya jinsi ilivyopatikana (somo la kwanza kabisa katika mada hiyo) sisi tunakimbia kukariri formula na kupata jawabu ili tupite mtihani, bila ya kujiuliza kwa nini pai ni 3.14 na si 3.3.

Ndiyo maana hata wasomi wetu ni watu wa kukariri tu, hatuna wavumbuzi.Utavumbua nini wakati unasubiri kukariri bila kuelewa undani wa mambo ?
 
Nionavyo mimi:
1. Ukosefu wa umakini, hundi kama hii ilitaka ipitiwe na mhasibu ku''authenticate quantity, quality and content'' TBL wana wahasibu wa viwango vya juu. Wamelala na kuwaachia makarani wamalize kazi.
2. Meneja uhusiano aliisoma kabla ya kupiga picha au alikimbilia Publicity tu.
3. Je si kweli kuwa wapo wanaoajiriwa hatakama ni vilaza,provided that baba au mama ni mkubwa fulani. unategemea nini.
4. Si kweli kuwa watz ni vilaza, ila mfumo wetu hauruhusu watoto vipanga wa masikini kuwa maafisa uhusiano au wahasibu.
5. Yaweza kuwa aliyeandika ni mtoto wa masikini lakini kamaliza sekondari ya kata! kwanini alaumiwe.
maswali ni mengi kuliko majibu.
 
Ndiyo maana hata wasomi wetu ni watu wa kukariri tu, hatuna wavumbuzi.Utavumbua nini wakati unasubiri kukariri bila kuelewa undani wa mambo ?

Hapo ndipo mimi ugomvi wangu ulipo. Mtu unapokijua kitu huna tena haja ya kukikariri maana hata uamshwe toka usingizini ukiulizwa swali utajibu kwa sababu unajua. Lakini kama umekariri uwezekano wa kusahau ni mkubwa sana.

Sasa ni kweli kama unavyosema, kama hujui kitu basi hata kuvumbua kitu hutaweza. Utavumbua nini wakati hujui? Ni lazima ujue kitu fulani ili uvumbue kitu fulani. Mwisho wa hadithi.

Sasa huyu jamaa anakuja bila soni na kutamba wao enzi zao eti walikuwa wanakariri badala ya kujua kwa nini hicho walichokuwa wanakariri kipo jinsi kilivyo. Ndio maana tuko kwenye hali tuliyonayo!!!!
 
Back
Top Bottom