Tulikuwepo Hukuwepo!

Tulikuwepo Hukuwepo!

Umesahau raba za Moro shoes, zilikuwa zinauzwa 450/= wakati huo. Hiyo ilikuwa kwenye 1982 huko.
kumbe tuko wengi wa longi humu! nakumbuka nilinunuliwa baieskli mpya kabisa kwenye duka la RTC ilikua inauza sh 661 aina ya Raleigh, yani buku ilikua hela nyingi sana
 
kumbe tuko wengi wa longi humu! nakumbuka nilinunuliwa baieskli mpya kabisa kwenye duka la RTC ilikua inauza sh 661 aina ya Raleigh, yani buku ilikua hela nyingi sana
wewe buku mwanaume anaenda kuichukulia mkopo bank.
 
kumbe tuko wengi wa longi humu! nakumbuka nilinunuliwa baieskli mpya kabisa kwenye duka la RTC ilikua inauza sh 661 aina ya Raleigh, yani buku ilikua hela nyingi sana
Ninakumbuka dingi alikuwa anasafiri sana, basi akituaga alikuwa anatupa sh 30-50 unajiona tajiri vibaya mno, outing ni Fanta na mihogo ya kukaanga jioni kama ukipewa ruhusa.
 
Siwezi kusahau nilikuwa kwenye ngonjera na bado ninakumbuka beti zangu, na mwimbo wa kuingilia ulikuwa "watoto ni mwaka wetu, tusonge mbele tusirudi nyuma daima".
Mkuu wa wilaya alikuwa makamba snr kama sikosei
 
Siku tulipochujwa wapatikane wa chipukizi mimi nilipanic nilirusha mguu na mkono, wenzangu waliokwenda kwenye gwaride baada ya michezo waliitwa wakale wale na pofu wakati sisi wa ngonjera unalinda ile shilingi uliyopewa home asubuhi.
Wali na pofu umenikumbusha mwanafunzi mmoja alitoka Lushoto basi lile pilau alikataa kula kwa kuwa lilikuwa chafu na mijiti. (mdalasini)
 
Wewe hapo tujadili wazee tu mwaka huo nina miaka mitatu toka kuhitimu elimu ya msingi
 
Siku hizi mkulu anahesabu hadi shoe shine ni viwanda alivyoviwezesha[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Na hizi ndio zilikuwa zama zetu!
View attachment 491309
Palikuwa na bimkubwa mmoja pale bora shoes akikuona tu hahitaji kukupima mguu anakwenda penye chanja akirudi na mguu hutoki yaani mulemule. Palikuwa na buti moja nyeusi hivi kule chini soli yake ilikuwa kama msumeno hivi ilikuwa balaa hapa juu pana fungwa tundu tatu tuliviita vya jeshi nilisota navyo sana haviishi tu basi nikitoka school mawe yote halali yangu lakini wapi kiatu kipo tu.
 
Sana. Mzee alikuwa MORO SHOE, aliwahi kunletea raba nikiwa darasa la pili, wadogo zangu wawili nao waliachiana raba hiyo hiyo!
Umenikumbusha kuna sneaker alinletea mzee nikavaa mpaka kikanibana,akavaa mdogo wangu naye vikamruka akavaa na mdogo wake enzi hizo wakinga hawajaanza kwenda china kuleta vitu feki.
 
Ninakumbuka dingi alikuwa anasafiri sana, basi akituaga alikuwa anatupa sh 30-50 unajiona tajiri vibaya mno, outing ni Fanta na mihogo ya kukaanga jioni kama ukipewa ruhusa.
Zile Fanta zilikuwa na utamu wa kipekee mimi nilikuwa nazibatiza (naongeza maji ili iwe nyingi )lakini ule utamu wake ulikuwa haupotei kirahisi.
 
Back
Top Bottom