Tulikuwepo Hukuwepo!

Tulikuwepo Hukuwepo!

Mwaka huo ulikua mgumu Sana, serikali ikatangaza tufunge mkanda miezi michache mambo yatarudia kua sawa(baada ya vita ya kagera), weeeeeeeeee, mpaka Leo hajawahi kurudi kua sawa.

Umenikumbusha mbali Sana Mkuu, kupanga foleni kusubiri unga wa Yanga.

Mambo hayakuanza kuharibika mwaka huo. Mambo yalianza kuharibika mara tu baada ya kutangazwa azimio la Arusha 1967.

Miaka huyo ya 79 na 80s ni climax tu ilikuwa inafikia.
 
Mambo hayakuanza kuharibika mwaka huo. Mambo yalianza kuharibika mara tu baada ya kutangazwa azimio la Arusha 1967.

Miaka huyo ya 79 na 80s ni climax tu ilikuwa inafikia.
Ha ha ha Haaaa , kwahiyo tuliwahi kufurahia maisha miaka 6 Tu baada ya uhuru, baada ya hapo Ni majanga mpaka Leo?

Unajua ule Uzi Wako Wa Mambo ambayo Nyerere alikosea Hua naupita Tu, ngoja nikausome, huenda Kuna kitu mule.
 
Very strategic, kwamba kipo kiwanda cha baiskeli cha Swala lakini BORA wanatengeneza tairi kama 'out-supply'.
Ukweli ni kwamba Mwalimu Nyerere aliikomboa na anaendelea kuikomboa nchi hii lakini sababu ya ujinga wetu uliokithiri hatuelewi hili. Miaka kama sabini ijayo tunaweza kuelewa labda! Tunaendelea kuamini katika kutopenda kufanya kazi hivyo kujiaminisha kuwa ukiikabidhi nchi kwa madalali ndio 'maendeleo' kumbe nao watakufanyisha kazi mara kumi zaidi na kwa masilahi madogo kupitiliza na mwisho wanahamisha chote walichopata kupeleka kwingine.

Unachopaswa kujua ni kuwa Mfumo wa Ujamaa umekufa Dunia Nzima kutokana na kuwa Mfumo wa kufikirika zaid!

Mfumo uwe Mzuri ni Pamoja na kuwa na uwezo wa kuwa applicable 'site'.

Mfumo wa Ujamaa ni Mzuri sana kwny Discussion na Mijadala ya Maendeleo tu lakin ukija kwny uhalisia ni Mfumo wan kufikirika zaid na Ndio sababu ulikufa japo Wakandarasi wake walikuwa Watu wenye Dhamira na akili za kutosha!
 
Ukimwi ulikua akuna ukienda uwanja wa fisi kavukavu

Gonjwa pekee lililokuwa linatutesa ni Gono, mambo ya Condom hayakuwepo na hata yalipoanza kuingia tuliamini ndani yake kuna virusi vya Ukimwi vimepandikizwa na Wazungu tukawa tukiwa kwny Safar za Kikazi ni Mwendo wa Misuguano ya Ngozi kwa ngozi tu
 
Kumbe Moro ilikua na viwanda?!
Ila sasa naona godowns tu
Polyster. Tumbaku. Canvas. Moproco. Moroshoes. Kiwanda cha Ngozi. Ndio ninavovikumbuka Mkuu!
 
Ile Ijumaa ya mwisho ya holiday mnakutana wote kwenye duka la Tanzania Elimu Supplies kununua mdaftari kalamu, vifutio, mikebe.......
Bila kusahau crepe bandages zilikuwa zinauzwa shilingi tatu nyeupe hizi nzuri sana basi utajifunga mguu au mkono hata kama hujaumia ili watu wajue unayo ilikuwa ni kogo (mikogo )ya enzi zetu.
 
Gonjwa pekee lililokuwa linatutesa ni Gono, mambo ya Condom hayakuwepo na hata yalipoanza kuingia tuliamini ndani yake kuna virusi vya Ukimwi vimepandikizwa na Wazungu tukawa tukiwa kwny Safar za Kikazi ni Mwendo wa Misuguano ya Ngozi kwa ngozi tu
Yaah kuhusu kondomu Swadakta kabisa maneno yako hilo wimbi la kutumia halikuwepo jaribu tu kukumbuka mwaka 1992 remmy ongala aliimba MAMBO KWA SOKSI na bado ikaonekana hauna maadili huo wimbo itakuja kuwa enzi zetu adhwimu hizo?kaswende kisonono duh ujue pana watu waliharibika vizazi kabisa kwa kadhia hizo watu walidungwa mpaka sindano za mifugo.
 
Hela kubwa kabisa ilikuwa ni Sh. 100/- ya noti(picha ya mmasai) not zilikuwa ni (Sh. 5/-, 10/-,20/- 50/- na 100/=) iliupate Sh 1000/- ilikuwa lazima upange noti kumi za 100/- na kuzifunga kwa kuikunja noti moja, na ndipo jina BUKU likapatikana maana lazima ujihesabu kwa kufungua kurasa mojamoja hadi kumi.
 
Enzi hizo secondary, day na boarding wote chakula kipo shuleni.
 
Back
Top Bottom