andjul
JF-Expert Member
- Dec 14, 2013
- 19,032
- 120,518
Mwaka 1979 ulikuwa mwaka wa ki-mataifa wa mtoto, kulikuwa na viatu pia vilitoka Bora, viliitwa mwaka wa mtoto.
muda acha uende.Mimi niliishia kupima tu kama vinanitosha,niliahidiwa kununuliwa sabasaba ikikaribia.Mungu alivyo na makusudi,nilitumwa kununua unga nikapewa sh.20.Ili uwahi unakoenda ni eidha uwe na ringi la kuzungusha au mpira wa majani ya mgomba,unaupiga na kuukimbilia.Mpira wangu uliniponza nikapoteza 20 ya mama,nilipigwa hadi nilichoka kulia.Ahadi ya viatu iliishia hapo hapo,ila kila mara nilikua naenda kwenye duka la Bora navichungulia viatu vyangu kwenye kioo.R.I.P mama yangu mpenzi.