Tulia Ackson Mwansasu, PhD, ananikumbusha mbali sana

Tulia Ackson Mwansasu, PhD, ananikumbusha mbali sana

wait and see!! huweze kuwaonea vijana 7800 na kuwafukuza bila huruma halafu utegemee watakupenda.Bunge zima limekosa ladha tulio izoea kwasababu vichwa vyenye akili havipo Bungeni. sasa 2020 wabunge wa upinzani lazima wafike 200 ndio ccm wajute kuwatambua upinzani.
Mkuu unatisha kwa kubadilisha terminology na uhalisia... kwa mtazamo wa watanzania tulio wengi...Bunge limemalizika vizuri kwa heshima, taadhima na radha yenye viwango. Mhe TULIA amerudisha heshima... Tunatambua kutumbuliwa kwa VILAZA 7800 watoto wa wakubwa huku watoto wetu wakihaha wenye matokeo bora wakipata shida... thank you very JPM kwa USTADI wa kazi. Unavyooviita VICHWA VENYE AKILI ! unaushangaza umma wa Watanzania...watu ambao hawana uwezo kwa kuzungumza bila kutumia TUMBAKU YA ARUSHA...unawaita vichwa!!! Thanks very much mhe TULIA....you have done a great JOB!!!!
 
Wewe jiulize wababe wote waliishia wapi? Hakuna hata mmoja ambae mwisho wake ulikuwa mwema.anzanza na Hitler, Nguema, bennito Musolin, Mabutu tsetseko, Idd Amin,Charles teller, n.k Wote waliishia kufa kama nugunungu.
Wababe kama mbowe mwenye kiti wa kudumu, waliojaribu kuhoji mustakabali wa chama wote nje
 
Hivi hawa
Yeye akifanya vile anafurahi kwamba UKAWA hawana chao na pengine kifo chao kimewadia. Kumbe ni kinyume chake, huku mitaani kuna watu hawapendi kabisa kusikia majina ya wabunge wa ccm, wanatamani kumuona Tundu Lisu, Mnyika, Halima Mdee, James Mbatia nk. Siku wakirudi bungeni nakuanza manjonjo yao watashangiliwa utadhani Tanzania tumechukua kombe la dunia.
Hivi jana wakati wanajiziba na ma karatasi mbowe alikuwepo? Au amewafanya misukule
 
Fanyeni uchaguzi huru mwenyekiti chadema muone
Ni lini haukufanyika uchaguzi huru ndani ya CDM na ni lini ccm mmefanya uchaguzi huru wa kuchagua mwenyekiti tofauti na kushuhudia makabidhiano ya utawala wa chamani!!????.
 
Wanabodi salamu!

Zamani sana kulikuwa na hadithi mashuhuri sana iliyo mhusu mama wa kambo na mtoto yatima.Mama yule kimsingi hakumpenda kijana yule, alikaa nae kwasababu tu ni mtoto wa mme wake. kwakuwa familia ilikuwa inajiweza mara nyingi chakula chao kilikuwa na nyama kama kitoweo. basi mama yule minofu yote aliwagawia watoto wake na yule yatima akapewa mchuzi na kipande kidogo cha nyama.
Siku wakipika makande aliwajazia watoto wake makande na yule mtoto kuambulia mchuzi na maharage kwa mbali sana.

Siku zilisonga, miaka ikasogea lakini kilicho mshangaza yule mama ni kwamba yule mtoto yatima ndio alipendeza na kuwa mwenye afya kuliko watoto wake. Kila akijiuliza alikuwa hapati jibu. Basi kwa jinsi yule kijana alivyo kua na kupendeza,binti mfalme alivutiwa nae na akatamani aolewe nae. Mfalme akafanya mipango yule kijana akamuoa binti mfalme.

Siku moja yule mama akasema nashangaa watoto wangu nawapa nyama tele lakini yule yatima nampa mchuzi tu lakini ndio anae nawiri! Basi mme wake akamwambia, kwenye mchuzi ndio kuna kila kirutubishi, ndio maana mtoto ambae hukumpenda kwa kumpa mchuzi ulimjenga kiafya badala ya kumkomoa.

Kiukweli Wanasiasa wa upinzani kule bungeni wananyanyaswa sana lakini ndio wanao jengwa kisiasa! Dr tulia mwenyewe anadhani anabomoa upinzani lakini kumbe ndio anaujenga na kuuimarisha zaidi na zaidi.Mpaka tunafika 2020 ,kuna watu watawachagua UKAWA kwa kuwaonea huruma tu kwasababu wameteswa miaka mingi.Kuna watu watawachagua UKAWA kwa kuchukizwa na ukatili na roho isiyo na chembe ya huruma ya spika.Kwahakika UKAWA wanatafutiwa ufalme badala ya kifo.

umekaa na kuwaza sana, ukafika hapa???

2020 tena? why not 2015??
 
Endeleeni kuimarika na kupata hivyo virutubisho vya mchuzi!!! 2020 CCM lazima iwatolee mahari. Msipende kupata fursa kwa kuonewa huruma.
 
Endeleeni kuimarika na kupata hivyo virutubisho vya mchuzi!!! 2020 CCM lazima iwatolee mahari. Msipende kupata fursa kwa kuonewa huruma.
Wenzako walisema mwisho wa upinzani ni 2015, lakini wanashangaa ndio wabunge wameongezeka maradufu! sasa 2020 ndio utashangaa, vijana wanazidi kuichukia ccm wanasema bora hata ya Kikwete fedha walikuwa wanapata kuliko sasa fedha imekuwa bidhaa adimu na wanao kula mlo mmoja wameongezeka kwa maelfu.
 
Wakati utasema nami sitachoka kukumbusha! Mabadiliko yoyote yanataka utashi. Kulikuwa na pesa ambazo walikuwa wanamiliki na kufaidi watu wachache. Ila wengi wa watu wa kati na maskini kama mimi hatukuziona hizo pesa. Au nawe ni muhanga wa hapa kzi tu!
 
kwa akili yako unafikili vitendo anavyofanyiwa Tulia na Ukawa ungekuwa wew ungevumilia au ungefurahi, Achen ushabik mchwala. Sasahv Ukawa wana mnyanyapaa yule Mama waziwaz hadi imefikia hatua wamekataa chakula cha wazir mkuu et kisa Tulia Akson yupo
Nani amesababisha?
 
Wakati utasema nami sitachoka kukumbusha! Mabadiliko yoyote yanataka utashi. Kulikuwa na pesa ambazo walikuwa wanamiliki na kufaidi watu wachache. Ila wengi wa watu wa kati na maskini kama mimi hatukuziona hizo pesa. Au nawe ni muhanga wa hapa kzi tu!
Ukiwa masikini jitahidi uwafikie matajiri siyo kuomba matajiri wafilisiwe! tajiri ana mbinu nyingi za kupata fedha, jiongeze ndugu yangu usikae kuomba matajiri wawe masikini.
 
Kubalini tume huru muone kama mtapata wabunge50 wabunge wengi mmelazimisha kwa maji ya kuawasha
mkitaka tume huru anzeni na kufanya uchaguzi huru wa mwenyekiti. sio mnadai democrasia wakati nyumbani kwenu ni madikteta wa kutupwa..
 
Haruma kwa UKAWA! wapi...over our dead bodies!!!
Usijiapize labda kama ww si Mtanzania, mwaka jana Watanzania wengi walimchagua Lowassa si kwa mapenzi bali huruma ya kutukanwa matusi ya kidhalilishaji huku mgombea ambae leo na Rais akishangilia (ilitokea kwenye mkutano wa Mwanza) ajabu leo hii neno bwege limekua tusi la mwaka wao yao sijui wamesahau au wana haki ya kutukana wenzao.
 
Safi sana mtoa mada ...
Huwezi kushinda pasipo ushindani, ccm wanajifanya washindi wakati hawajashindana na yeyote. Na ninachokifahamu mimi hata miongoni mwao wapo wenye busara wanaoyaona haya madudu ila wanafungwa midomo na itikadi za chama chao.
Nitoe mstari mmoja wa kwenye biblia ..
Zaburi 49:20 .. Mwanadamu mwenye heshima iwapo hana akili amefanana na mnyama apoteaye.
 
mkitaka tume huru anzeni na kufanya uchaguzi huru wa mwenyekiti. sio mnadai democrasia wakati nyumbani kwenu ni madikteta wa kutupwa..
Jiulize wewe kama mwenyekiti wenu huwa anachaguliwa au anawekwa tu kwa mujibu wa utaratibu ambao sio wa kidemokrasia.
 
Jiulize wewe kama mwenyekiti wenu huwa anachaguliwa au anawekwa tu kwa mujibu wa utaratibu ambao sio wa kidemokrasia.
anachaguliwa na wanachama, tena anakubali kuondoka mwenyewe baada ya 10 yrs. sio wa chama flani aliyeondoa kipengele cha ukomo wa madaraka. kama museven yaani.
 
Ukiwa masikini jitahidi uwafikie matajiri siyo kuomba matajiri wafilisiwe! tajiri ana mbinu nyingi za kupata fedha, jiongeze ndugu yangu usikae kuomba matajiri wawe masikini.

Sina shaka wala wivu na utajiri wa halali. Wengi wa matajiri nchi hii wanapata utajiri kwa kunyonya maskini.Kodi hawalipi na kufanya vitu kwa kujuana na kuwanyima fursa watu wa hali ya chini.
 
Usijiapize labda kama ww si Mtanzania, mwaka jana Watanzania wengi walimchagua Lowassa si kwa mapenzi bali huruma ya kutukanwa matusi ya kidhalilishaji huku mgombea ambae leo na Rais akishangilia (ilitokea kwenye mkutano wa Mwanza) ajabu leo hii neno bwege limekua tusi la mwaka wao yao sijui wamesahau au wana haki ya kutukana wenzao.
Watu wasiojitambua ndio walimchagua Lowassa! kama wagombea wanachaguliwa kwa huruma ya kutukanwa JK atakuwa kwenye GRADE ya JUU...... kwa ufupi..UKAWA wamekosa DIRA....hawana pa kushika....Mara Zanzibar, mara MCC, Mara Sukari... mara kutetea wanafunzi wasio na qualification.... mara madawati.... kwa sasa haijulikani wanasimamia nini!
 
Muwe mfano badala ya kulalamika tu name kwani lowassa ana cheo gani hadi asikilizwe kwenye nchi
 
Tulia anaweza kuwa na shida kisaikolojia, ni SADIST; yaani mtu anayefurahia anapomuumiza mtu au watu.
CCM wanamfurahia kwakuwa leo anapambana na ukawa ila atakapopewa kitengo kwenye Chama watalia.
Tulia amedefine upinzani kama uadui ila anachokifanya kitamnyima kufurahia maisha kwa uhuru mtaani.
Atakuwa anaishi kama kunguru, akiona hata mtu anataka kujikuna kwenye kichwa anaruka,anajua atapigwa!

Mi nafikiria kuwa anawalipishia kisasi kwa kuwa kwenye bunge la awali UKAWA walihoji taarifa zake na hasa kuhusiana na uanachama wake CCM alijiunga lini wakati alikuwa mwanasheria wa serikali (hakupaswa kuwa na chama), na baadae ikapelekea zomea zomea kuwa kabebwa. Hiyo itakuwa ilimuuma mno, sina uhakika kwamba kwa nini aliumia sana endapo hoja hizo hazikuwa za kweli au za msingi! Na ndio sababu yule mbunge wa CCM alivyowaambia wabunge wa CDM hawapewi ubunge hadi waitwe baby alifurahi kama aliyesamehewa kufa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom