JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,112
- 3,536
Wanabodi salamu!
Zamani sana kulikuwa na hadithi mashuhuri sana iliyo mhusu mama wa kambo na mtoto yatima.Mama yule kimsingi hakumpenda kijana yule, alikaa nae kwasababu tu ni mtoto wa mme wake. kwakuwa familia ilikuwa inajiweza mara nyingi chakula chao kilikuwa na nyama kama kitoweo. basi mama yule minofu yote aliwagawia watoto wake na yule yatima akapewa mchuzi na kipande kidogo cha nyama.
Siku wakipika makande aliwajazia watoto wake makande na yule mtoto kuambulia mchuzi na maharage kwa mbali sana.
Siku zilisonga, miaka ikasogea lakini kilicho mshangaza yule mama ni kwamba yule mtoto yatima ndio alipendeza na kuwa mwenye afya kuliko watoto wake. Kila akijiuliza alikuwa hapati jibu. Basi kwa jinsi yule kijana alivyo kua na kupendeza,binti mfalme alivutiwa nae na akatamani aolewe nae. Mfalme akafanya mipango yule kijana akamuoa binti mfalme.
Siku moja yule mama akasema nashangaa watoto wangu nawapa nyama tele lakini yule yatima nampa mchuzi tu lakini ndio anae nawiri! Basi mme wake akamwambia, kwenye mchuzi ndio kuna kila kirutubishi, ndio maana mtoto ambae hukumpenda kwa kumpa mchuzi ulimjenga kiafya badala ya kumkomoa.
Kiukweli Wanasiasa wa upinzani kule bungeni wananyanyaswa sana lakini ndio wanao jengwa kisiasa! Dr tulia mwenyewe anadhani anabomoa upinzani lakini kumbe ndio anaujenga na kuuimarisha zaidi na zaidi.Mpaka tunafika 2020 ,kuna watu watawachagua UKAWA kwa kuwaonea huruma tu kwasababu wameteswa miaka mingi.Kuna watu watawachagua UKAWA kwa kuchukizwa na ukatili na roho isiyo na chembe ya huruma ya spika.Kwahakika UKAWA wanatafutiwa ufalme badala ya kifo.