Tukumbuke majina ya utani kwa walimu shule tulikotoka

Fiudo-mwalimu anyefundisha Civics, pat ya modes of production (Feudalism)
Exotic-Mwalimu aliyepewa jina baada ya kufundisha exotic breeds of livestock
Mzee tulikuwa pamoja ile shule karibu na bahari nini?
 
du kwa waliosoma NYAKATO Bukoba.kulikua Ndondocha headmaster,ukikosea alikuita ndondocha jina likawa lake,sistep p madam mselamsela,mwanambuzi,cadastro mwalimu wa geograghy form 3,kikongwe mwalimu wa math.pokati huyu jamaa sitamsaau kwa ukorofi,alikua anaimiza form one wadundwe.miloso au bwana mzee alipenda kutuita hivo alikua anapiga fimbo 6 kwa kila kosa liwe kubwa au dogo.kamanda. Na LL yaani elo elo.huyu akikumata unatoloka kwenda town utafyeka hatua 40 kwa 40.
 
PUSI - huyu alikuwa Discipline Master "Makumix" pamoja na sifa nyingine alizokuwa nazo kwa madenti, alikuwa anatabia ya kunyemelea sehemu madenti wamepoa kwa story au kujisomea. Sometimz alikuwa anabadili mwendo kwenye giza ili tusimtambue. Sijui yupo wapi kwa sasa. This was 1998
 
PUSI - huyu alikuwa Discipline Master "Makumix" pamoja na sifa nyingine alizokuwa nazo kwa madenti, alikuwa anatabia ya kunyemelea sehemu madenti wamepoa kwa story au kujisomea. Sometimz alikuwa anabadili mwendo kwenye giza ili tusimtambue. Sijui yupo wapi kwa sasa. This was 1998

Ulifutiwa mitihani ya form four, wewe ulikuwa mmoja wao form IV ya 1998?
 
Fimbo mbili - kila wakati alikuwa anatembea na fimbo mbili
Perpendicular - Mwalimu wa hesabu
 
mwalimu mkuu wa shule ya msingi msimbazi mseto sasa ni marehemu Sara sanga aka kijeba dodo miaka ya 90's
mwalimu wa malezi Karatu high schoo mr,Amnayye aka Bichwa miaka ya 2005-06
 
CCS-(inatamkwa sisiesi)huyu alikuwa mwl wetu wa maths form 2 alikuwa hawezi kusema siksi eksi(6X). Mwanzoni ilituwia ngumu kumuelewa,hlf nae alikuwa ukikosea hakuachi bila viboko 6 afu ndo unajieleza sasa.

JOBUFAYA-Alikuwa anaitwa mwl kazimoto.

Okwonkwo-mwl wa kiingerza kwenye novel alikuwa maarufu utasema ndo jina lake halisi.cku moja mwanafunzi kaingia staff room akauliza namtafuta mwl onkwonkwo,wee hzo bakora alizopigwa ni nouma.
 
KIPUTE-huyu mwl alikuwa chapombe sn,akifundisha kidg tu utsikia huuuh...huuuh

KAHAWA- jina lake hals ni Kahwa,huyu mhaya alikuwa anajickia sn mwl wa Geog advance
 
kigonsera au kigonsese;jina la h/master aliyehamia PUGU BOY akitokea shule ya kigonsera
MABAGS; master minds..alikua anajua majina ya wanafunzi wooote
SHUNGU;jina la head master wangu uzuri prymary2000
you must be my school mate...mr.sherimo now ni DEO wa Temeke that man was genius.
 
mzee see - huyu ni alikuwa pale ujiji seminary 2001 sijui yupo wapi sasa..
 
"Gori Moshi" - huyu alikua anavuta sigara c mchezo, alikua ana tabia ya kukariri examples za kitabu cha Advanced Mathematics cha kinunda halaf anafundisha bila kitabu, wakambatiza jina lingine "Kinunda".
 
hahaha jamani kuna mwalimu wetu wa kemia form2 anaitwa Chilima,yeye tulikua Tunamwita ELEMENDI kwa sababu alikua hawezi tamka Element.waliosoma AlQAEM SEM DOM 2007 kurudi nyuma watakua wanamfahamu mana alikuja kwenda morogoro.
 
Jamani Mwl Magambo yupo? Alikuwa second master Nganza miaka ya late 1980s!

alipotoka Nganza , aliletwa Kwiro Mahenge, alituletea zawadi ya magunia ya Dagaa ! Alikua mkali sana , alitisha kama Simba . Alikua mcheza volleyball wa aina yake. . . . Magambo alipokuja Kwiro ndo akapachikwa jina la Mbwiko .
 
Mbungi - mwalimu wangu wa somo la umeme Ifunda f2 hadi f4
Kocha - mwalimu wa bweni Ifunda adhabu zake yeye mazoezi tu kama psh up na kichurachura
People- mwalimu wa ung'eng'e f3 hapohapo Ifunda alikuwa haongei maneno matatu bila kusema 'you people'
 
Kifu2 wa bongo =huyu ni mwalimu wa phy.materials yote kaweka kwenye bongo yake. alikua anaingia darasani na choki 2 bila summary wala notes lakini anawaandikia notes ubao mzima na kuujaza na kufuta kama mara 7
 
Gurudumu: mwalimu mmoja Ashira girls, sikumbuki jina lake halisi ila shape kama gurudumu alikuwa mwl wa cookery
 
Gurudumu: mwalimu mmoja Ashira girls, sikumbuki jina lake halisi ila shape kama gurudumu alikuwa mwl wa cookery

Lol, Mhandisi!
Nimecheka lakini sasa namhurumia huyo Gurudumu.
Tumshukuru Mungu kwa kazi zake.
 
Back
Top Bottom