Bin Maryam, haya maneno mazito sana yaani nakubaliana na wewe 100% isipokuwa binafsi nawaogopa hata wazawa sasa hivi kwa sababu sijui mzalendo ni nani haswa ikiwa watu wenyewe ndio hawa Mafisadi...
.....NN, ingelitokea kuwa umekaa karibu nami halafu ukawa umetamka maneno kama hayo juu, na katika mazingira ya ajabu ajabu nami nikajikuta nimeshika baseball bat mkononi.... hakika ningeitumia.... the thick end of it could have landed on you at the highest velocity possible!!!!!!
.....NN, but why why why you tryna indoctrinate us with this self-hatin' sh...t?! dawg, you oughtta bring it to a halt....... pliiiiiiiiiz!
nuff' respect
Prof Ndulu said Tanzania would only manage to retain the remitted earnings when local contractors attain competence to compete equally with foreign firms.
Rev.Kishoka,
Nakubali sana kuwa wakoloni walitumia hila kutuweka chini wapate kutawala lakini sidhani kama moja wapo ni pamoja na kutufundisha Ujinga..isipokuwa walitunyima nafasi sawa ktk kila kitu cha kujiendeleza ikiwa ni pamoja na Umoja wetu.
Ujinga ni kutokuwa na Elimu na mkoloni katukuta tukiwa wajinga na katuacha wajinga... moja ya imani za kijinga ni hizo za kuutukuza Uzungu ambazo zilikuwepo hata kabla Mjarumani hajaweka mguu Afrika. Hizi imani za kulaumu Biblia ama Kuran penye tafsiri chafu ni mafundisho yetu sisi wenyewe, tumefundishana sisi kuwatukuza wazungu.
Nina imani kubwa kwamba haya mafundisho tumeyatunga sisi iwe ni sababu kubwa ya kuleta mapinduzi ya kifikra ama Unafiki wa baadhi makolokoloni wa wazungu kwa sababu dini zote hizi zilitufundisha UPENDO... na ni katika mafundisho hayo ya Upendo ndipo sisi tuliposhusha ngao zetu kuwapa mwanya wakatumia UPENDO huo huo kuboresha azma zao za kutawala..
Hawa hawana tofauti na viongozi wetu leo hii ambao wanatumia sheria, maazimio na sera za vitabu vyetu kupora mali zetu za taifa lakini hata siku moja hawawezi kufundisha kitu kutujaza ujinga...kwa sababu elimu yoyote inayotolewa mara nyingi humwamsha mjinga akili yake na akaanza kuitumia akili yake...
Ni katika mafundisho hayo hayo ya Biblia na Kuran yaliweza kuwaamsha viongozi wengi Machief wetu enzi hizo kukataa kutawaliwa. As a fact vitabu hivi vinajenga zaidi self esteem kutokubali kutawaliwa hata kama wewe ni mtumwa..Ni vitabu kama hivi vilivyoanzisha vita toka enzi za Nabi iDaud hadi kina Kinjeketile - Majimaji kina Kenyatta na Maumau na hata Ghandi wakitumia quotes za vitabu hivi..
Kwa mfano siku zote tulikuwa ktk ujinga wa kuamini viongozi wetu ni makini na hakuna somo la siasa ambalo limepokewa kuwaweka wao mbele yetu zaidi ya unyenyekevu wao kwetu. Ni katika hali hiyo waliweza kuvuta Upendo wa wananchi na kupewa nafasi ambazo wao wamezitumia kutimiza azma (ambition) zao..hawakutujaza Ujinga isipokuwa ujinga tayari tulikuwa nao kabla hawajaingia madarakani. Wanayafanya yote haya wakifahamu sisi ni Wadanganyika, wajinga kina Ndivyo tulivyo hali ktk Ujinga huo huo wao pia wamo kwa sababu walikuwa ktk kundi la wajinga na ni reflection yetu sote. Hivyo basi wajinga ni pamoja na wao wanapotumia nafasi kama hizi za Uongozi kutawala badala ya kuboresha maisha ya kizazi chao..Kesho Tanzania itabaki maskini na kizazi chake kitaendelea kuishi ktk mazingira duni..
Kama nilivyosema Ujinga ni pale mtu hajui na akafikiria kuwa anajua...Ukisha jifahamu kwamba hujui na kweli hujui kitu basi hiyo ni hatua ya kwanza ya kuondokana na Ujinga..
hamuwezi kuamini lakini huo ndiyo ukweli, yafuatayo ni mambo yaliyowekwa na wakuu kuhakikisha kuwa local contractors hawawezi kufurukuta
1.0, kila tender inayotangazwa hapa nchini kuna sharti la kuwa na bid security in form of unconditional bank guarantee, yaani kama una-tender kazi ya 100m, lazima uwe na angalau cash bank 10m, ukipata kazi wANAKUDAI UNCONDITONAL BANK GUARANTEE YA 20%, NA ILI UPATE ADVANCE LAZIMA UWE NA GUARANTEE KAMA HIYO, KWA MAHESABU YA HARAKA HARAKA LAZIMA UWE NA KAMA 45M BANK. sharti hili liliwekwa na wenzetu walioko maofisini kuwabaeba wahindi kwa kuwa wao wanapata guarantee kwenye benki zao kama vile savings&finance hata kama hawana shilingi kule ndani, wachina nao wanakuja na za kwao toka chinatoka kwenye mabenki yao hata kama ni feki hakuna anayejua!
pamoja na tanroads kukakomalia kuwa badala ya hizo guarantee kampuni za ki-local zitoe kitu kinaitwa tender securing declaration, bado mashirika kama PPF, NSSF, lapf etc, yamekomalia sysytem ya bank guarantee, kazi zote za majengo ambazo ndizo zenye peasa na zinaweza kufanywa na wazalendo wahandisi waliosoma pale UDSM, au ardhi university zinafanywa na wahindi kupitia benki zao uchwara. asilimia 90% ya contrators class one wahindi waliobebwa na mfumo huu uchwara list ni kama masasi construction, bh ladwa, gk patel,nk, hawa ndo wanafanya majengo yote nchi nzima, hawana cha maana zaiidi ya kubebwa na kamfumo walikojitengenezea wenyewe
unajua kuna kitu kimoja kinachonisumbua sana kuhusu hili.
a. Hivi watu wanaosoma katika vyuo vyetu vikuu hivyo vitu wanavyovisoma vinatofauti kubwa kiasi gani na vile watu wanasoma nchi nyingine? Yaani, engineer wa umeme wa Tanzania, au Engineer wa barabara anatofauti gani kiujuzi na yule wa nje? Je tukimpa nafasi ya kufanya kazi kama US au UK atafanya hayo anayoweza kufanya Tanzania (kama alivyosema Kuhani Mkuu)?
b. Ni kitu gani kinachomfanya mtumishi wa TAnzania anapowatumikia watanzania wenzake anawapa minimal quality of service lakini akija mzungu au mtu wa nje hasa nchi za magharibi anamuonesha ukarimu na huduma bora kweli. Nazungumza toka personal experience.
NIlipokuwa home mara ya mwisho about four years ago, nilikaribisha marafiki zangu toka Ujerumani na tukawa tunaenda nao kutembelea Serengeti. Through out the tour wao walikuwa wanapapatikiwa ingawa ni mimi nilikuwa nalipia gharama nyingi. Kwanini? Sitoshangaa wengine mmewahi kwenda kupata huduma na ukachukuliwa with contempt lakini mtasha na mabegibegi yake anakaribishwa na "welcome sir, how can I help you" with bis a.s smile! kwanini Watanzania wanastahili huduma ya chini au bidhaa za chini?
c. Je Mtanzania akipewa nafasi ya kuitumikia nchi yake anavutiwa kwa kiasi gani to provide the best quality service? Kuna utaratibu gani wa kuhakikisha the Standard Operating Procedures katika maeneo mbalimbali zinafuatwa to the letter?
kazi wanazopewa makandarasi wa kizalendo hasa za halmashauri hazina tija yeyote, rushwa ndo kikwazo kikubwa, utaoewa kazi ya kuweka kifusi km 5, kwa shilingi 35m, utatakiwa kupeleka hongo kama 10m, zinazobaki hazitoshi kazi ndo maana watu wanalipua kazi, nimekuwa kwenye hii industry as profession kwa miaka 18 sasa, usanii ni mwingi. kilichowashinda konoike kumaliza dodoma-manyoni road project ni hicho hicho, ukisikia kazi inafadhiliwa na g0vernment ya tanzania kaa chonjo. kutoka singida -to shelui kazi imemalizika vema contractor ni mchina pesa zimetoka world bank hakuna rushwa, toka singida-manyoni contractor mchina, kazi imeshindikana, pesa ni za serikali shauri ya rushwa..., toka manyoni-dodoma, contractor konoike kazi inasua sua ile mbaya, pesa za serikali ya tz shauri ya rushwa, toka makuyunu-ngorngoro, konoike hao hao wamemaliza kazi nzuri sana, pesa iantoka na kulipiwa japani rushwa hamna, jifunzeni kable hamjawalaumu makandarasi. ukifanya kazi nzuri bila kutoa rushwa unaweza hata kufutwa ukandarasi
Mkuu, Mwikimbi!
Hata sisi hii industry tunaifahamu kwa zaidi ya miaka hiyo uliyoitaja. Tatizo ni kuwa utakubalije kutoa rushwa ya milioni kumi kwa mradi wa milioni 35? Kwa nini usimchomee anayekudai hiyo rushwa? Na ukikataa kutoa ina maana atakataa kukuandalia certificate? Mara nyingi, na hii inatokana na uzoefu, makandarasi wetu wanatanguliza ahadi za kuwekana sawa mara watakapopata mradi! sasa mradi ni competitive na unatakiwa kuweka bei itakayokuwa chini ya wenzako, hiyo hela ya hongo utaitoa wapi? Wenzetu walipoona haya wakajitoa kwenye local projects, na hizo nyingine zilipopotea, wakafunga virago! Sisi tunashindwa nini? Kwani lazima tuwe makandarasi? Kwa mtazamo huu wa kutaka kazi hata kama ni ya hasara ndiyo kunakowafanya waseme kuwa tu wajinga![/FONT]
tumesha kubali kuwa sisi ni wajinga na inauma je tumefanya au tunafanya nini ili kujikwamua?
Fundi Mchundo said:Hivi ni wangapi kati yetu tunapotaka kujenga kasri zetu nyumbani tunatumia wataaalamu wazalendo? Wangapi tunaajiri kampuni za architects, quantity surveyors, structural engineers, electrical engineers wazalendo? Baada ya hapa ni wangapi tunaajiri makandarasi wazalendo? Naamini sio wengi.
Mhandisi ujenzi aliyesomea Tanzania ana uwezo saa wa kitaaluma na Mhandishi aliyesoma Marekani? Je mhasibu wa Tanzania amesomea sawasawa na yule aliyesomea Uingereza?