Tukitumia maexpert kutoka nje inaweza kusaidia kuendesha mashirika kama TAZARA?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,210
12,710
Zamani kuna historia kuwa Mobutu alipoona uchumi unaenda hovyo akaajili mbobezi kutoka Ulaya kuwa gavana wa benki kuu.

Jamaa akaja na mipango mizuri sana ya kuokoa uchumi. lakini alikuta vikwazo kibao, Mobutu alikuwa anaifanya benki kuu kama kibubu chake.

Wakashindwana jamaa akasepa. Mkapa baada ya kuona uzembe wa kuendesha mambo serikalini akaleta mtaalamu wa kuendesha hospitali kutoka Ulaya aendeshe hospitali ya Muhimbili. Nasikia jamaa alifanya kazi yake kwa weledi sana. alijenga uzio wa hospitali.

Na kuweka mipaka ya wahadhiri wa chuo na wafanyakazi wa hospitali. kabla ya hapo wahadhiri walikuwa na cheo wakisimamia kitengo hospitali huku wanavitengo vingine chuoni.

Pengine mashirika yetu mengi yanababaika kwa sababu maadminstrator hawana weledi wa kufanya hizo kazi. kuwa na elimu tu haitoshi, inaonekana ubobezi unahitajika kuendesha mashirika kwa ufanisi.

sasa badala ya kubinafsisha mashirika yetu kwanini tusitafute wabobezi wayaendeshe, Ulaya kumejaa watu waliopiga kazi hizi miaka na miaka, wanaweza kutusaidia.
 
Mkuu unaonaje kama tungejaribu ma expert kutoka nje kuendesha nchi kabisa ili kuukata mzizi wote wa fitina?
Ingekuwa poa pia, sema kutakuwa na kelele za uzalendo nk. Maafisa wa JWtz walitaka kumpindua Nyerere kwa sababu kama hiyo.
 
Ingekuwa poa pia, sema kutakuwa na kelele za uzalendo nk. Maafisa wa JWtz walitaka kumpindua Nyerere kwa sababu kama hiyo.

Mkuu kama ma expert kutoka nje wataleta tija Tazara? Vipi Tanesco? ATCL?

Vipi TRC, Tanroads, TRA, Tanpol, Magereza, kuliko na kina SABAYA, au kote kwa ujumla?

Tuna matatizo ya msingi. Ndiyo maana tumefikia kubambikiziana makesi.

Badala ya kuhangaika na matawi twende kwenye shina.
 
Back
Top Bottom