Tukio la ufinyangwaji wa Sheria huko Shinyanga si la kukaa kimya

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,781
2,301
Serikali imefanikiwa kupata zaidi ya trilioni kadhaa kwa ajili ya mapambano ya uviko 19.

Lakini wanasiasa na baadhi ya viongozi wameanza ufinyangaji wa sheria kwa kisingizio cha haraka ya Mh. Rais.

Tumemuona Mkuu wa Mkoa Shinyanga akifanya hivyo, wakurugenzi, madiwani na hata baadhi ya Wizara.

Watu wanasahau kwamba kuna sheria. Kwenye hili Takukuru amkeni. Huko TAMISEMI ni hatari zaidi. Zipo Taasisi zimejipa mamlaka yasiyo yake.

Rushwa, Rushwa..
 
Mkuu eleza tatizo lipo wapi ili hata mamlaka zipate pa kuanzia

Kuandika kitu kana kwamba wote tunajua yaliyotokea shinyanga si sawa

Endeleza uzi tujue tatizo
 
Hata mimi huyo mkuu wa mkoa wa Shy amenikwaza sana.Yani anamsimamisha kazi mtumishi anayesisitiza sheria ya manunuzi ifuatwe kikamilifu ktk kujenga hayo Madarasa, kweli!?. Kisingizio eti anawachelewesha, kwani sheria si zilitungwa na Bunge letu wenyewe? Ninahisi kuna mazingira ya upigaji yanawekwa hapo.
 
Mkuu eleza tatizo lipo wapi ili hata mamlaka zipate pa kuanzia

Kuandika kitu kana kwamba wote tunajua yaliyotokea shinyanga si sawa

Endeleza uzi tujue tatizo
Mkuu huko Shinyanga , mkuu wa mkoa amemsimamisha afisa manunuzi na huko Tamisemi kila mtu ni mnunuzi, wizara ya afya ndio balaa, hakueleweki. Maji wapo vizuri.
 
Kuna watu wanapiga hela aiseeee...nilikuwa sijui mtu ukiwa nje ya system huna tofauti na mtu alieko kaburini.....
 
Back
Top Bottom