Tukio gani lilitokea maishani likabadilisha mtazamo na imani yako?

Mchanya

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
976
1,526
Nilipokuwa mdogo, miaka kadhaa iliyopita nilipoteza kamera ya rafiki yangu mmoja aliyekuja kututembelea nyumbani kwetu. Nilikuwa bado mwanafunzi nikiishi pamoja na wazazi. Rafiki huyu aliipata kamera hiyo kama zawadi kutoka kwa ndugu yake aliyekuwa akiishi ughaibuni.

Tulipiga picha nyingi naye na baadhi ya wanafamilia, marafiki na majirani na tukapanga siku ya pili yake twende 'kusafisha mkanda' (Wale wahenga wananielewa) ili tupate picha. Bahati mbaya tulipoamka asubuhi kamera haikuwepo, ilishaibiwa.

Mimi na familia hasa mama yangu tulihuzunika sana, tulihisi aliyeiba hakuwa mbali nasi, na anatufahamu sisi na pia anafahamu mazingira yetu, lakini kwa kuwa hatukuwa na ushahidi hatukuweza kumkamata yeyote. Wakati huo hakukuwepo na simu janja kama hizi za sasa, hivyo kumiliki kamera ilikuwa ni jambo kubwa, na ungeweza hata kufanya biashara ya kuwapiga picha watu mbalimbali na kujipatia fedha na kuendesha maisha.

Akajitokeza mama mmoja aliyekuwa jirani yetu, akamshauri mama yangu kwamba twende kwa mganga wa kienyeji kupata suluhu ya tatizo letu. Tulipokwenda kwa mganga, baada ya 'kufanya vitu vyake' akatuambia kamera 'anaiona, ipo, haijapelekwa mbali na itarudi ndani ya saa 24', mama alimlipa chake mganda nasi tukarudi nyumbani kwa hamu tukisubiria kamera irudishwe ndani ya saa 24. Hadi leo imepita miaka mingi tangu kamera ile kuibiwa na haijarudishwa.

Kuibiwa kwa kamera ile likuwa jambo baya na la kuhuzunisha kwangu, lakini kwa upande mwingine limenifundisha msingi na imani muhimu iliyokuja kunisaidia maishani mwangu baadaye kwamba waganga wa kienyeji si watu wa kuwaamini kabisa. Tangu wakati huo sitaki na wala sina mpango wa kusikia habari kuhusu mganga wa kienyeji.

Je, una lolote limekutokea maishani lililobadilisha mtazamo au imani yako kuhusu mambo fulani fulani?

Hebu tiririka hapa, ili nasi tujifunze.
 
Ilikua mwaka 2010, tuliibiwa baiskel tukaita sheh ikasomwa albadiri baada ya wiki tukamkuta nayo mtu bugurun tukamuuliza baskeli yako ? Yule mtu akasema ngoja nikamuite mwenyewe hakurudi kabisa had usiku ukaingia
 
Ilikua mwaka 2010, tuliibiwa baiskel tukaita sheh ikasomwa albadiri baada ya wiki tukamkuta nayo mtu bugurun tukamuuliza baskeli yako ? Yule mtu akasema ngoja nikamuite mwenyewe hakurudi kabisa had usiku ukaingia
Asingefanta albadiri msingemkuta nayo buguruni?
 
Back
Top Bottom