Tukio ambalo sitoweza kulisahau daima

Tukio ambalo sitoweza kulisahau daima

H

Hakuna cha kuweka defense wala nn wale jamaa wakikubamba network ya Kichwa inakata kabisa maxima wanatisha eti weka mbali na watoto
Me nakimbuka juzi kama wiki mbili zimepita tulikuw twaenda mbea msibani sasa taa za dani ya gari ziligoma kuzima sababu sehemu ya mlangoni tuliweka jeneza kumbe mlango aukufunga
Tumepita mikumi kama SAA nne na nusu usiku mbele tunaona kundi la simba wawili wakawa wanakuja kwenye gari yetu weeee bwana kumbe wanatuona ndani ya gari sasa dereva akawa anapiga kelele zibeni taa maana walitanda barabaran magari yakawa yanatembea taratibu yaani tulitaftana mbona kwenye gari kila mtu akuiyona taa aisee simba anatisha asikwambie mtu
 
Tulikuwa tunawinda

Sasa mimi nilielekea kwenye gari sasa yule mwanzangu alikuwa yupo makini kutafuta target ya kumpiga digidigi sasa kumbe simba alinyata mpaka nyuma ya yule jamaa yangu mimi sikuona sababu kuna ishu nilikuwa nafanya ndani ya gari sasa ile kuinua macho nikashuhudia mchezo mzima sasa yule jamaa akahisi kitu kizito nyuma yake na akili yake akadhani ni Mimi sasa akawa anamsukumiza yule simba na kunitaja "bwana ...desh desh" Sogea bwana unaniharibia target jamaa alihisi kitu tofauti maana ngozi ya binaadamu haina manyoya ile anageuka atizame vizuri mara paap uso kwa uso na simba

Kilichotokea ni siri yangu
Mungu wangu... Alirukiwa na simba na dani ya dakika kumi ukaona fuvu la kichwa chake na viatu ndio vilivyobakia!
 
Hakuna sehemu jamaa kaongelea mzoga, by the way simba akikamata shingo sio kuwa lengo anywe damu, NOPE.

Lengo ni kumbana pumzi mnyama ili afe...
Akikamata shingo anatoboa "jangular vein" (kama sijakisea spelling), unapoteza damu nyingi na eventually unakufa.
 
Hii ni historia fupi ya uwindaji wa simba..

Simba ni wanyama wenye nguvu ambao mara zote huwinda kwa makundi na kumkazania windo walilochagua. Hata hivyo hawajulikani sana kwa stamina yao, kwa mfano, moyo wa simba jike unajumisha tu asilimia 0.57 ya uzito wa mwili wake (wa dume ni asilimia 0.45 ya uzito wa mwili wake), wakati ule wa fisi ni karibu asilimia moja ya uzito wake. Hivyo basi, japokuwa simba anaweza kufikia mwendokasi wa km 81 kwa saa, wanaweza kufanya hivyo kwa mwendo mfupi tu na inawapasa kuwa karibu na mawindo kabla ya kuanza shambulio. Hutumia mwanya wa kupunguza uoni; kwa kufanya uwindaji sana nyakati za usiku. Humnyatia adui mpaka pale wamekaribia kwa walau mita 30 au pungufu. Kisha kukaribia huchagua mnyama aliye karibu. Shambulio huwa fupi na la nguvu; hujaribu kumkamata kwa kumkurupusha kwa kasi na kisha kumrukia. Mnyama huyo daima huuawa kwa kunyongwa. Mara kadhaa pia huweza kuuawa kwa kuzibwa mdomo na pua zake kwa taya za simba. Wanyama wadogo huuawa tu kwa kupigwa ngwala kwa mguu wa simba.

Kitoweo cha simba hujumuisha wanyama wengi wakubwa, hasa wildebeest, nyati, impala, pundamilia, na warthogs kwa Afrika na nilgai, wild boar na aina kadhaa za tandala huko India. Spishi nyingine huwindwa kutokana na upatikanaji wao.

Simba wakiwa wanawinda katika kundi kubwa wana uwezo hata wa kuangusha wanyama wakubwa lakini mara nyingi huwa hawashambulii wanyama wakubwa sana kama vile twiga kwa kuhofia kujeruhiwa pia.

Simba pia wana uwezo wa kushambulia wanyama wanaofugwa na binadamu; kwa mfano huko India ng’ombe wengi huwa chakula cha simba. Simba pia wanaweza kula wanyama wenzao wanaokula nyama kama vile chui, duma, fisi na mbwa mwitu. Pia wakati mwingine hula mizoga ya wanyama wengine waliouawa kwa majanga au na wanyama wengine, na huangalia sana mahali wapozungukazunguka tai, wakijua fika mahali walipo patakuwa na mizoga. Simba anaweza kula mpaka kg 30 kwa mlo mmoja; na kama hawezi kula windo lake lote, hupumzika kwa saa kadhaa na kisha kuendelea tena. Wakati wa mchana na joto kali, kundi la simba hukaa kivulini na dume mmoja au wawili kubakia kama walinzi. Simba jike anahitaji walau kg 5 za nyama kwa siku wakati dume ni kg 7.

Kwa sababu simba huwinda kwenye sehemu wazi, ambapo wanaonekana kwa urahisi na adui zake, uwindaji wa ushirikiano ndio husaidia na kufanikiwa, hasa kwa wanyama wakubwa. Ushirikiano huu husaidia pia kulinda mawindo yao kwa urahisi dhidi ya wanyama wengine, kama vile fisi, ambao mara moja hujua mzoga ulipo kwa kuangalia mahali ambapo tai wanaruka. Uwindaji mkubwa hufanywa na simba jike; simba dume waliopo kwenye kundi hawashiriki kwenye uwindaji mpaka tu pale wanapohitaji kuwinda wanyama wakubwa kama vile twiga au nyati. Wakati wa kuwinda kila simba jike ana nafasi ya kuwinda na kumpata mnyama, aidha kwa kunyatia kwenye na kisha kushambulia au kusogea umbali kidogo karibu na katikati mwa kundi na kumkamata mnyama huyo amwindaye kutoka kwa simba wengine.

Simba wadogo huonesha tabia ya kunyatia wanyama wakiwa na miezi mitatu tu, ingawa hawashiriki kwenye uwindaji mpaka wawe na umri wa mwaka mmoja. Huanza rasmi kuwinda wakiwa na umri wa miaka miwili.
 
Hii sentesi yako inamaana sana ila hawawez kuelewa sisi tuliowapoteza wazazi wetu kati ya mama au baba tunajua umuhimu wa wazazi wetu
Inauma sana,kila nikimkumbuka my mumy,nlikuwa na miaka sita tu
 
Hamna kitu hapo...
Mimi naona huu ni uongo kama sio ukweli uliozidishwa chumvi.

Simba wakikamata windo huwa wanakunywa damu tu na kuondoka.
Hawali mizoga Simba, hiyo ni kazi ya Mbweha (Hyena).

Hata kwenye Animal Planet tunaonaga sana tu.
Yan hata kufikiri umeshindwa kabisa..Unahisi simba wanaishi KWA KUNYWA DAMU TU!!!! me mwenyewe naangaliaga hiyo ANIMAL PLANET na DISCOVERY zote na ni mpenzi wa vipindi vya wanyama ila SIJAWAHI ONA simba akawinda,akakamata... akanyonya damu then akaondoka..NI UONGO MTUPU HUO..
 
Akikamata shingo anatoboa "jangular vein" (kama sijakisea spelling), unapoteza damu nyingi na eventually unakufa.
Uwezekano wa jugular vein kuwa punctured upo, lakini sio sababu ya simba kumkamata windo lake shingoni.
"Evolutionary" intention/aim ni kum'bana mnyama/prey windpipe/throat/koromeo ili asiweze pumua na hivyo kufa kwa kukosa hewa.
Na hii inahitaji "seasoned" huntress/lioness/lion (yaani simba aliye na uzoefu wa kuwinda) ku'perfect the art of strangulation.
Uuaji huu hauna tofauti na ule wa "constrictors"/nyoka wauao kwa kunyonga.
 
Hii ni historia fupi ya uwindaji wa simba..

Simba ni wanyama wenye nguvu ambao mara zote huwinda kwa makundi na kumkazania windo walilochagua. Hata hivyo hawajulikani sana kwa stamina yao, kwa mfano, moyo wa simba jike unajumisha tu asilimia 0.57 ya uzito wa mwili wake (wa dume ni asilimia 0.45 ya uzito wa mwili wake), wakati ule wa fisi ni karibu asilimia moja ya uzito wake. Hivyo basi, japokuwa simba anaweza kufikia mwendokasi wa km 81 kwa saa, wanaweza kufanya hivyo kwa mwendo mfupi tu na inawapasa kuwa karibu na mawindo kabla ya kuanza shambulio. Hutumia mwanya wa kupunguza uoni; kwa kufanya uwindaji sana nyakati za usiku. Humnyatia adui mpaka pale wamekaribia kwa walau mita 30 au pungufu. Kisha kukaribia huchagua mnyama aliye karibu. Shambulio huwa fupi na la nguvu; hujaribu kumkamata kwa kumkurupusha kwa kasi na kisha kumrukia. Mnyama huyo daima huuawa kwa kunyongwa. Mara kadhaa pia huweza kuuawa kwa kuzibwa mdomo na pua zake kwa taya za simba. Wanyama wadogo huuawa tu kwa kupigwa ngwala kwa mguu wa simba.

Kitoweo cha simba hujumuisha wanyama wengi wakubwa, hasa wildebeest, nyati, impala, pundamilia, na warthogs kwa Afrika na nilgai, wild boar na aina kadhaa za tandala huko India. Spishi nyingine huwindwa kutokana na upatikanaji wao.

Simba wakiwa wanawinda katika kundi kubwa wana uwezo hata wa kuangusha wanyama wakubwa lakini mara nyingi huwa hawashambulii wanyama wakubwa sana kama vile twiga kwa kuhofia kujeruhiwa pia.

Simba pia wana uwezo wa kushambulia wanyama wanaofugwa na binadamu; kwa mfano huko India ng’ombe wengi huwa chakula cha simba. Simba pia wanaweza kula wanyama wenzao wanaokula nyama kama vile chui, duma, fisi na mbwa mwitu. Pia wakati mwingine hula mizoga ya wanyama wengine waliouawa kwa majanga au na wanyama wengine, na huangalia sana mahali wapozungukazunguka tai, wakijua fika mahali walipo patakuwa na mizoga. Simba anaweza kula mpaka kg 30 kwa mlo mmoja; na kama hawezi kula windo lake lote, hupumzika kwa saa kadhaa na kisha kuendelea tena. Wakati wa mchana na joto kali, kundi la simba hukaa kivulini na dume mmoja au wawili kubakia kama walinzi. Simba jike anahitaji walau kg 5 za nyama kwa siku wakati dume ni kg 7.

Kwa sababu simba huwinda kwenye sehemu wazi, ambapo wanaonekana kwa urahisi na adui zake, uwindaji wa ushirikiano ndio husaidia na kufanikiwa, hasa kwa wanyama wakubwa. Ushirikiano huu husaidia pia kulinda mawindo yao kwa urahisi dhidi ya wanyama wengine, kama vile fisi, ambao mara moja hujua mzoga ulipo kwa kuangalia mahali ambapo tai wanaruka. Uwindaji mkubwa hufanywa na simba jike; simba dume waliopo kwenye kundi hawashiriki kwenye uwindaji mpaka tu pale wanapohitaji kuwinda wanyama wakubwa kama vile twiga au nyati. Wakati wa kuwinda kila simba jike ana nafasi ya kuwinda na kumpata mnyama, aidha kwa kunyatia kwenye na kisha kushambulia au kusogea umbali kidogo karibu na katikati mwa kundi na kumkamata mnyama huyo amwindaye kutoka kwa simba wengine.

Simba wadogo huonesha tabia ya kunyatia wanyama wakiwa na miezi mitatu tu, ingawa hawashiriki kwenye uwindaji mpaka wawe na umri wa mwaka mmoja. Huanza rasmi kuwinda wakiwa na umri wa miaka miwili.
Asante mkuu kwa elimu sahihi.
 
hivi mkuu ktk huo mpango ww ungekaa upande wa kumuangalia simba au ungewapa mgongo simba?
Kama mpo watu wanne na wenzako wameanza kukimbia basi hakuna namna itabidi ukimbie sababu tayari hakuna wa kuangalia au kukulinda mgongoni kwako.
 
Hamna kitu hapo...
Mimi naona huu ni uongo kama sio ukweli uliozidishwa chumvi.

Simba wakikamata windo huwa wanakunywa damu tu na kuondoka.
Hawali mizoga Simba, hiyo ni kazi ya Mbweha (Hyena).

Hata kwenye Animal Planet tunaonaga sana tu.
Mkuu naomba kukuuliza. Nini maana ya mzoga???
 
Nakumbuka siku kama ya leo tarehe 21/04/2016 nilikuwa katika mtihani mzito ambao sitakuja usahau katika maisha yangu yaliyobakia hapa duniani, Niliondokewa na mama yangu mzazi Duniani tarehe 19/04/2016 na tulimzika tarehe 21/04/2016 mkoani Tanga Wilayani Muheza. Ndugu zangu had leo hii sina mama mwenzenu, kitu hiki kinaniumiza sana katika maisha yangu ya kila siku. Siwezi kusahau na huwa halinitoki moyoni. Naumia sana. Bali namuomba mwenyezi mungu amuepushe na adhabu ya kaburi na amuwekee mwanga katika kaburi lake. "Ameen"
Mtolee sadaka.
 
Great Thinkers bana
Hiv kweli Fumba fumbua simba huyu hapa halaf unaanza Kutengeneza Formation defence, hv unazan n km mourihno akipak bas kuzuiz magol?, Mwingne et umtishie simba kwa kelele au mkojo m nahc simba mwenyewe ataweza azimie kwa kukucheka
Mkuu kama hakuna mti mrefu karibu sana au upo mti lakini simba wapo karibu sana basi ni kujidanganya ukijaribu kukimbilia juu ya mti kwani simba anakasi sana kuliko binadamu na kuna simba wengine (aina ya mbarara) wanaweza wanaweza kupanda juu ya miti. Au mti ukiwa mfupi simba yeyote anakushusha. Hapo njia pekee ni kuambizana jamani wote tukae pamoja tusikimbie tuwatazame simba. Kwa vile simba anaweza kuanza kuwazungukia kwenda kila upande inabidi muwekeane mgongo. Kama wale simba walikuwa wawili kwa vyovyote vile mkisimama simba mmoja atakuja toka upande tofauti na mwenzie, watajaribu kuwazingira. Simba hatulii upande mmoja hivyo hakuna mtubmmoja atakae kuwa yeye tu ndio anatazamana na simba.
 
Uwezekano wa jugular vein kuwa punctured upo, lakini sio sababu ya simba kumkamata windo lake shingoni.
"Evolutionary" intention/aim ni kum'bana mnyama/prey windpipe/throat/koromeo ili asiweze pumua na hivyo kufa kwa kukosa hewa.
Na hii inahitaji "seasoned" huntress/lioness/lion (yaani simba aliye na uzoefu wa kuwinda) ku'perfect the art of strangulation.
Uuaji huu hauna tofauti na ule wa "constrictors"/nyoka wauao kwa kunyonga.
Ahsante kwa ufafanuzi mkuu. Sikuwa nikilifahamu hili kabla. Ama kweli jf ni kisima cha maarifa.
 
Mkuu kama hakuna mti mrefu karibu sana au upo mti lakini simba wapo karibu sana basi ni kujidanganya ukijaribu kukimbilia juu ya mti kwani simba anakasi sana kuliko binadamu na kuna simba wengine (aina ya mbarara) wanaweza wanaweza kupanda juu ya miti. Au mti ukiwa mfupi simba yeyote anakushusha. Hapo njia pekee ni kuambizana jamani wote tukae pamoja tusikimbie tuwatazame simba. Kwa vile simba anaweza kuanza kuwazungukia kwenda kila upande inabidi muwekeane mgongo. Kama wale simba walikuwa wawili kwa vyovyote vile mkisimama simba mmoja atakuja toka upande tofauti na mwenzie, watajaribu kuwazingira. Simba hatulii upande mmoja hivyo hakuna mtubmmoja atakae kuwa yeye tu ndio anatazamana na simba.

Hapo kwa namna flan nimekusoma mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom