KIBITI BOYZ
Member
- Mar 31, 2017
- 14
- 32
HESHIMA KWENU WANAJUKWAA.
Mnamo mwaka 2000 mwezi February tukiwa shamba kwa kilimo cha mpunga katika wilaya ya Kilombero(Ifakara) maeneo ya Mchombe mashambani sehemu inayoitwa Simbagungile tulivamiwa na simba majira ya saa 6 kasoro.
Nyumba ilikuwa ya chini yaani imejengwa kwa miti tu na kutumia nyasi kama ukuta na juu nkuezeka kwa nyasi, walikuwa simba wawili na sisi ndani tulikuwa watu wanne, punde tukajikuta katika shambulio nashukuru nifakiwa kupanda juu ya kitanda chetu cha miti na kupanda juu ya nguzo moja wapo ya kile kinyumba chetu.
Huku nikiwa juu nilishuhudia simba wakiwatafuna wale ndugu zangu bila huruma hadi kuwaua wote watatu na kuwatafuna na kubakiza mabaki kama ngozi, fuvu la kichwa na miguu na mikono kwa wote. Walipomaliza wakaingia huku na kule na kutoka nje ya nyumba baadae mmoja akarudi ndani na kutoka pia wale simba walienda kuvamia nyumba zingine mbili.
R.I.P ALL.
JE WEWE MWENZANGU NI TUKIO LIPI AMBALO HUTOWEZA KULISAHAU?
Karibu