Tukio ambalo sitoweza kulisahau daima

Tukio ambalo sitoweza kulisahau daima

daah mleta mada umenikumbusha kitambo sanaa, ni kijiji alichokuwa anaishi bibi yangu (RIP), kinaitwa Mngeta.
kipindi hicho kulikuwa na sifa kubwa ya kuvamiwa na simba sema wenyeji wanasema simba wengi wa kule ni wakutumwa na watu siyo simba halisi. mfano labda kulikuwa na ugomvi wa shamba au umedhurumu mpunga wa mtu bas rafiki yangu jiandae kuonana na simba mubashara.
nakumbuka mwaka 2004 nilienda kupeleka dawa ya kuua majani kwenye mpunga, kufika kule waliokuwa wanalima wakanambia yaani leo alfajiri tu simba walipita wakanionyesha na alama za miguu. nakumbuka ilitakiwa nirudi mapema ila nilikaa hadi wale jamaa wamalize kazi nirudi nao
 
Kitu kimoja pekee kingeweza kuwaokoa ni ummoja na kujiamini. Wangefanya formation ya defence kama wafanyavyo zebra kuwekeana migongo mkiwatazama simba, simba wangeogopa kuwashambulia lakini ni kama wangekuwa ktk eneo wazi nje ya kibanda. Kama waliwaona simba ndio wakakimbilia ndani basi hilo ndio lilukuwa kosa lao kubwa. Simba walishajua jamaa ni waoga hawawezi kudhuru hao simba. Simba mwoga pia lakini ujasiri wa kutowaogopa ni lazima ufundishwe au Siku hiyo Mungu akupe huo ujasiri ili ukuokoe.
Ushawahi kumuona nyamaume lakini mkuu?
 
Wewe ni mtu wa hovyo kabisa yaani Ndugu zako wanatafunwa na Simba unaangalia tu bila hata kupiga makelele au kurusha hata udongo au kuwakojolea hao Simba, RIP Ndugu wa huyu jamaa
Angepiga kelele na yeye angeliwa. Simba unawafahamu lakini? Hawakujua kuwa yupo mru mwingine vinginevyo wasingeondoka wangevuruga kibanda hadi wamshushe wamle.
 
Hamna kitu hapo...
Mimi naona huu ni uongo kama sio ukweli uliozidishwa chumvi.

Simba wakikamata windo huwa wanakunywa damu tu na kuondoka.
Hawali mizoga Simba, hiyo ni kazi ya Mbweha (Hyena).

Hata kwenye Animal Planet tunaonaga sana tu.
Mkuu sio kukukosoa, ila unadhani pale simba anapomkamata mnyama shingo ni kwamba anamnyonya damu?

Sawa hawalagi mizoga per se (yaani sio Modus Operandi/method zao), ila wale simba dume wadogo waliofukuzwa na territorial males yaani nomads wanapozidiwa huwa wana'scavange/kula mizoga.

Check the fact sheet again mkuu.
 
Hamna kitu hapo...
Mimi naona huu ni uongo kama sio ukweli uliozidishwa chumvi.

Simba wakikamata windo huwa wanakunywa damu tu na kuondoka.
Hawali mizoga Simba, hiyo ni kazi ya Mbweha (Hyena).

Hata kwenye Animal Planet tunaonaga sana tu.
 
Hasira wapi wewe acha kujifanya una hisia za matatizo yasiyo kuhusu wewe!!!

Una uhakika gani kama hiyo habari ni ya kweli... Ulikuepo???

Wapi uliona Simba anakula nyama na kubakiza mifupa!!
Simba anakunywa damu tu, akishiba damu anasepa zake...
Kula mizoga ni kazi ya Fisi.
Mtu ambae hajui hata maana ya mzoga siwezi kubishana nae. Eti simba anakunywa damu tu????!!!! "I bet" wewe hujaona live mabaki yaliyoachwa na simba baada ya kumuua mnyama. Basi hata kuangalia picha tu za video na still pics mitandaoni au kwenye TV hauoni zile documentary? Nenda basi Youtube zipo kibao. What kind of CCNP Engineer who is so lame like this? Very unconvincingly feeble!!
 
Mhh kweli kila mtu na akili yake, "CCNP Engineer"Kwani umelezimishwa kunipa pole, kama kifo cha mama yako hakikukuumiza ni wewe mimi ndio kitu ambacho sitakisahau ktk maisha yangu. Hebu watu humu ndani tujaribu kuwa wastaarabu, hivi "CCNP Engineer" Engineer mzima unaweza andika kitu kama umetoka usingizini???? Nina wasiwasi na Uinjinia wako, Kuwa na busara. Wala siitaji pole yako maana haitanisaidia.
 
Mkuu sio kukukosoa, ila unadhani pale simba anapomkamata mnyama shingo ni kwamba anamnyonya damu?

Sawa hawalagi mizoga per se (yaani sio Modus Operandi/method zao), ila wale simba dume wadogo waliofukuzwa na territorial males yaani nomads wanapozidiwa huwa wana'scavange/kula mizoga.

Check the fact sheet again mkuu.
Hebu mwambie huyo, anadhani simba anaishi kwa kunywa damu!!!.....na mzoga anaujua???
 
Iliwatokea jirani zetu..Japo ni zamani lkn lile tukio lilikuwa si la kiungwana..Walikuwa wanamsafirisha Dada yao na mtoto wake waliofariki kwa ajari ya gari Tegeta!wakiwa njiani walivamiwa na watu wenye siraha za jadi, na kuwapora kila kitu walivyokuwa washenzi walizifungua maiti zote na kuzisachi,Ile gari waliitoa mafuta na wakatoa upepo mataili yote!!
Isiishie hapo wakaondoka na kila kitu hadi nguo zao za ndani,,
Kumbuka kwenye ule msafara wote ni ndugu Baba Mama wa yule Dada marehemu wote walikuwepo,,,,
Yule Bi Mkubwa alishindwa kustahimili kule kijijini!!!Mungu amsamehe kwa kujitoa uhai baada ya mazishi ya mjukuu wake na mwanae...
 
H
Kitu kimoja pekee kingeweza kuwaokoa ni ummoja na kujiamini. Wangefanya formation ya defence kama wafanyavyo zebra kuwekeana migongo mkiwatazama simba, simba wangeogopa kuwashambulia lakini ni kama wangekuwa ktk eneo wazi nje ya kibanda. Kama waliwaona simba ndio wakakimbilia ndani basi hilo ndio lilikuwa kosa lao kubwa. Simba walishajua jamaa ni waoga hawawezi kudhuru hao simba. Simba mwoga pia lakini ujasiri wa kutowaogopa ni lazima ufundishwe au Siku hiyo Mungu akupe huo ujasiri ili ukuokoe.
Hakuna cha kuweka defense wala nn wale jamaa wakikubamba network ya Kichwa inakata kabisa maxima wanatisha eti weka mbali na watoto
 
Wabongo bwana...
Ili mradi tu na wewe uonekane una kitu special...
Kwahiyo kila mtu aliyefiwa na mama yake aje hapa aanze kulia lia kama wewe then watu wampe pole!!
Si tutapeana pole jukwaa zima sasa!!

Kufiwa na mama watu kibao tumefiwa bwana, wala sio jambo eti special kiviiile mpaka uanze kutoa makamasi...

Tunataka tukio special, ambalo ukisimulia miili yetu isisimke zzzzzz!!

Halafu mijitu humu ilivo mbumbumbu eti inakupa pole..
Mie hata sikupi pole.
Acha kujitoa akili kijana. Tunapokea matukio ktk hali tofauti,acha kumcrash mwenzio.

Wewe unataka mtu aelezee tukio litakalo kusisimua mwili zzzz kwani umeambiwa tunapigana shot hapa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom