Tukidhani ni Binadamu wenzetu, kumbe ni mashetani! Mtu unaombeaje mwenzako afe kwa Corona? Can't believe this wickedness! Huu sio utu, ni ushetani!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,497
113,592
Wanabodi,

Mtu unachokiandika, ndicho unacho kiwaza!, kuna watu, tunaishi nao, tunakula nao, tunalala nao, tukidhani ni binaadamu wenzetu, kumbe ni machoni tuu ndio kama watu, lakini mioyoni ni mashetani wakubwa!. Mtu unaombeaje binaadamu mwenzako afe kwa Corona?!. Can't believe this wickedness imewakuta Watanzania wenzetu!. Huu sio utu, sio ubinaadamu, ni ushetani!

Unaweza usiamini hili ninaloandika hapa lakini ni kweli kabisa, wakati dunia ikihangaika na janga la ugonjwa wa Corona linaliitesa dunia nzima tukiwepo sisi Tanzania, kuna baadhi ya wenzetu humu mitandaoni utu na ubinaadamu umewatoka wamekuwa sio watu tena, sio binaadam bali ni mashetani kwa kuombea wenzao sio tuu wapate Corona, bali wapate Corona na wafe kwa vifo vya Corona!.

Hili nimelishuhudia humu jf na mitandao mingine baadhi ya wenzetu waki andika ku wish wenzao wapate Corona na wafe kwa Corona kwa wengine kuwataja kabisa kwa majina mimi nikiwa ni mmoja wao na wengine kuwataja kwa majina ya utani au hata bila kutaji jina ula unajua ni nani!.

Lengo la bandiko hili sio mimi kulalamika kuwa kuna watu wananitaka nipate Corona, kwasababu mimi ni nobody, hata nikichomoka na Corona, it's only my wife, my kids na my family ndio wata suffer, bali kuna watu very wicked wana wish viongozi wetu fulani fulani wafe kwa Corona, kutokana na positions za hao viongozi, ikitokea kweli wakachomoka kwa Corona, taifa tuta suffer kwa kupigwa na double tragedy!.

Mimi ni miongoni mwa Watanzania wenye uwezo wa kitu kinachoitwa graphology ni uwezo wa kusoma maandishi ya watu, kisha ukabaini mwandishi alimdhamiria nini, hata akiandika neno "bora tuu afe kwa Corona ", bila kumtaja ni nani, kupitia graphology unajua ni nani alidhamiriwa afe!, japo huyo mwandishi anaweza kuwa hakuandika kwa kumtaja jina expressly kuwa nataka fulani afe kwa Corona, lakini kupitia uwezo huo wa graphology, then unatambua impliedly aliyedhamiriwa ni nani!.

To wish someone specific afe kwa Corona ni highest stages of wickedness, Watanzania siku zote ni watu wenye upendo, tunapendana na tunawapenda viongozi wetu, na hata chama chetu japo tunakilalamikia sana humu mitandaoni kuwa ndicho chanzo cha umasikini na madhila yote yanayolikuta taifa letu, lakini in reality, tunakipenda sana na kila mwaka huwa tunakichagua tena na tena mwaka hadi mwaka, na kama janga la Corona halitadumu muda mrefu na kuleta madhara makubwa, then mwezi October, 2020, tunakichagua tena, sasa iweje binadamu wenzetu, Watanzania wenzetu kuingiwa na roho ya ushetani wa ajabu kwa kuwa na wishful thinking ya kuombea viongozi wetu fulani fulani tegemewa, wafe kwa Corona?!.

Ajabu kubwa zaidi ni idadi ya members watakao toa likes kwa huyo mtu, inaonyesha jinsi tulivyo na kundi kubwa Watanzania wenzetu ambao ni wicked kwa kusupport hizo wicked ideas!, na kipimo rahisi kwa mashetani hawa, utakiona kwenye uchangiaji kwenye hili bandiko.

Swali la kujiuliza hivi ni kweli Watanzania watu tuliiokuwa na upendo wa ajabu zaidi hata ya upendo wa mshumaa, wa kumulikia wengine huku kwako unateketea, sasa tumefika hapa kuombeana vifo vya Corona?. Huu ni utu, ni Ubinaadamu au ni ushetani wa ajabu?.

Hivi kweli sisi Watanzania tumefikia stage ya kuishi na binadamu wenzetu wenye mawazo ya kishetani kama haya halafu tunaishi nao tukiendelea kula nao, kunywa nao na kulala nao na wengine hadi tunawapongeza!, hivi ushetani huu unatofauti yoyote na ule ushetani wa Sodoma na Gomorrah?!.

Ingekuwa kila kitu mtu anachokiwaza kinaandikwa kwenye paji la uso wake, hivyo nikikuambia ufunge macho na kuwish ulitaka mtu gani afe kwa Corona, amini usiamini, watu tungekuwa surprised kukuta mke ana wish mume ndio afe, mume ana wish mke ndio afe na nikiuliza ungewish kiongozi gani afe kwa Corona, majibu yangekuwa yanaandikwa usoni!, watu mngeshanga na ungeweza usiamini!.

Tiba Nambari One Duniani ni Imani, yaani faith, kwa janga kama la Corona ili liishe na lisilete madhara makubwa na maafa kwa Tanzania na duniani kwa ujumla, ni kama Watanzania na watu wote, ikiwa wote tuta wish kwa dhati ya mioyo yetu kumuomba Mungu kwa dhati, alipishie mbali, hili janga la Corona, lakini kitendo cha wengine tunasali, na kumuomba Mungu atuepushe na janga la Corona, huku kuna wenzetu wengine wao waki wish fulani apate Corona afe, kunapunguza nguvu ya sala zetu, huu sio Ubinaadamu, sio utu, ni ushetani!.

Hala hala kwa mashetani hawa, ingekuwa dua ls kuku linampata mwewe, saa hizi siku nyingi kuna watu tungekuwa ni historia, lakini Mungu sio Athumani, kila mtu atakufa siku yake Mungu aliyompangia tena kwa kifo kile kile mtu ulichopangiwa, kama mtu umepangiwa kufa kwa Corona, utakufa tuu kwa Corona and no one can do anything kuzuia, ili kitendo cha mtu kumwish mtu fulani afe kwa Corona, sheria ya karma my act kwa kanuni ya what goes around, comes around, wakati uki wish fulani afe kwa Corona, karma may act upon you na ku reverse your wishes on opposite directions, hiyo wish ikakurudia wewe na familia yako!.
Tupendane wandugu, na tuwishiane mema!.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu wasamehe Watanzania wenzetu waliomkaribisha shetani ndani yao na umtume Roho Mtakatifu wako, awasafishe na kuwatakasa with their evil thoughts and wickedness na kuliepusha taifa letu na janga la Corona.

Amen.

Paskali
 
Acha hao wanaoombea, hao ni cha mtoto, hao inaonyesha ni wanyonge na hawana cha kufanya hivyo wamebaki wakitegemea maombi tu. Kuna wanao kaa vikao kujadili nani apelekwe gerezani? lini? kwa kesi gani? kisha unapewa kesi. Mbaya zaidi hujadili nani afe? na afe lini? na namna gani? halafu wanakwenda kuua wenyewe.
 
Wafe tu kwa kweli... sitaki kuwa mnafiki; yeyote miongoni mwao akifa na kama bado mimi nitakuwa hai, sitaandika RIP bali RIH... yaani Rest In Hell.

Wa kazi gani?!

Hapa nazungumzia wale ambao muda wote wamesimama na serikali na Rais kutetea kila aina ya ujinga kwenye issue mzima ya coronavirus!!

Wakiambiwa nyungu inatibu corona, wanashabikia na kujifanya ni namna gani wanaifahamu nyungu na uwezo wake wakati siku zote hatukuwasikia wakizungumzia suala la nyungu kutibu corona hadi JPM alioposema!!

Ni wale ambao hata leo JPM akisema mkojo wa vikongwe ni tiba mujarabu ya corona, kama mazuzu vile yataunga mkono!!!

Hakuna namna kwa kweli... kama walikuwa wanaleta mizaha, wafe tu manake hata likija janga kubwa zaidi ya coronavirus, bado wataendelea watawala na mizaha yao kwenye serioous issues.

Hao watu ni useless, na ni coronavirus kwa jamii! Isitoshe, majority ni wale wale ambao walifurahi kweli kweli waliposikia Tundu Lissu kamiminiwa makumi ya risasi, na wakaja kununa waliposikia Mwamba kagoma ku-RIP!!

Wengi wao hawana ubinadamu wowote mbele ya siasa! Na ni hao hao wakisia fulani kafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na money laundering, watashangilia kweli kweli hata wakijua kesi yenyewe ni ya kubambikia!

Sasa mijitu kama hiyo nisikie imekufa na corona ndo nijisikie uchungu?! Sana sana nitawaone uchungu mbuzi na kuku watakaochinjwa kwa ajili ya matanga yake!!

Na ule utani wao wa kuwaambia watu wakajazane makanisani na misikitini eti kuomba corona iondoke, Mungu angetufanyia wepesi kuwaondoa wao manake ndio agents wakuu wa coronavirus... directly or indirectly kupitia wazimu wao!

Labda niwakumbushe tu kwamba, waliokufa na watakaokufa kwa coronavirus (probably nami ni mmoja wao), wengi wao ni victims wa mizaha iliyoletwa na JPM na Misukule yake!! Kila tuilipokuwa tunapiga kelele kuhusu mizaha inayofanywa na serikali, tuliishia kukejeliwa!!

Siku taifa litaanza kushambuliwa na mizinga, na mtatuambia "msiogope, ni vimondo tu hivyo" kwa sababu tu Rais kasema "ni vimondo tu hivyo"!
 
Hahahaha umeandika kwa kirefu sana but Kuna Watu wanakera sana!! Hasa CCM to be specific! Unakumbuka issue ya akina Halima Mdee na Esther Bulaya? Unakumbuka zile kebehi?

It pains na kama kweli kama hao watu wapo basi CCM ndio waasisi wa hayo mambo na wanavuna walichokipanda KARMA
 
Lakini mbona CCM wamekua wakifurahia watu kutekwa kuteswa na kupiga risasi......
Sasa wengine wakiwaombea mabaya wanakua na makosa gani.... Ccm ni chama Cha kishetani. Miaka mitano iliyopita wamefanya kazi ya kunljenga chuki kwenye jamii......

KITU AMBACHO NINA UHAKIKA NACHO NI KWAMBA KOLONA IKIISHA TU TUNARUDI KULEKULE KWENYE KUTESANA SI UNAONA VIONGOZI WA JUU BADO WASHUPAZA SHINGO NA WAMEJAA KIBURI HATA KTK VITA HII KUBWA YA KODUNIA
 
Back
Top Bottom