Mtukutu wa Nyaigela
JF-Expert Member
- Sep 4, 2018
- 8,011
- 14,334
mm ninachojua amri kuu ni upendo....mpende jirani yako kama unavyojipenda ww na wala usimteke.......NEIGHBORHOOD PRINCIPLE.....Neighbor principle is a principle of English law which says that a person should take reasonable care to avoid acts or omissions that s/he can reasonably foresee as likely to cause injury to the neighbor. Lord Atkin....
Upendo Kwa Mungu :Ukimpenda Mungu utashika amri 4 za kwanza.(Amri kuu ya upendo)
20 Mungu akanena maneno haya yote akasema,2Mimi ni BWANA Mungu wako niliyekutoa katika nchi ya misri,katika nyumba ya utumwa.
3Usiwe na miungu mingine Ila mimi.
4Usijifanyie sanamu ya kuchonga,wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni,wala kilicho chini duniani,wala kilicho majini chini ya dunia.
5Usivisujudie wala kuvitumikia;kwa kuwa Mimi,BWANA,Mungu wako,ni Mungu mwenye wivu;nawapatiliza wana maovu ya baba zao,hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao,na kuzishika amri zangu
7Usilitaje bure jina la BWANA,
Mungu wako,maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajae jina lake bure.
8Ikumbuke siku ya sabato uitakase
Ukimpenda mwanadamu mwenzio :utashika amri sita zinazofuata ,maana zote zinadhihirisha upendo kwa mwanadamu.-utapenda baba na mama,hautaua,hautaiba,hautazini,hautasema uongo na hautatamani vitu vya jirani yako
12Waheshimu baba yako na mama yako;siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA,Mungu wako.
13Usiue
14Usizini
15Usiibe
16Usimshuhudie jirani yako uongo
17Usitamani nyumba ya jirani yako,usimtamani mke wa jirani yako;wala mtumwa wake,wala mjakazi wake,wala ng'ombe wake,wala punda wake,wala chochote alicho nacho jirani yako.
Wakakatolic wamegawanya amri ya kumi ya kutamani zikawa 2 na kufuta ya pili