Tujikumbushe Amri kuu za Mungu

Tujikumbushe Amri kuu za Mungu

Jifunze wenzio wanachosema,ni bahati mbaya tu unaona kama kanisa la roma linashambuliwa. Watu wanajaribu kueleza vitu ambavyo vinafanywa tofauti na biblia inavyoagiza. Tunahitaji tu majibu ,usituagize tuje kweye semina. Weka semina yako hapa hapa watu wote tuone.
Semina yako ianze na haya mambo mawili. Kwanini jumapili na siyo jumamosi na Kwanini sanamu zinaabudiwa(usitudanganye kuwa zipo tu hamziabudu) .Nakuomba uanze na semina ya hayo mambo mawili. Tunatamani kuwa wakatoliki lakini hayo mambo yanatukwaza hivyo tunahitaji msaada.
Kwa mtu mwenye akili timamu hawezi poteza muda wake kubishania masula yanayohusu imani kwenye mitandao. Huo ni ulimbukeni. Mimi siujui Ukatoliki kuna haja gani ya kushambulia imani yao ? Nyie ni wapumbavu, hamjitambui. Mungu awahurumie.
 
Amri namba 6 na 9 hii najaribu kupambana nayo hata shetani anaona kabisa.
Me 7 na 8 ndo zimenishinda,mbaya zaidi zimerandana yaani najikuta ili niivunje ya 7 lazima ya nane ihusike and vice versa!

Eeh Mungu nipe kile ninachokihangaikia ili niweze kurudi kwako nikiwa bado na ufahamu..Amen
 
Hizi ni Amri zilizochakachuliwa na kanisa la ROMA ,

Watu maelfu mmemezeshwa amri zilizochakachuliwa na kuwekwa kwenye katekisimo, Zile Amri kumi ORIGINAL alizopewa musa pale SINAI, zipo kwenye biblia hata hamtaki kuzifatilia ,mfananishe na hizo za PAPA
Mkuu AROON kama hizi hujazielewa waache wanaozielewa wajikumbushe nazo but pia wewe unaruhusiwa kuweka zile zako unazozijua ili wewe na wale mtakaozielewa mjifunze kwazo haina haja kuanzisha uzi ndani ya uzi wa mwenzako.
 
Mkuu wala sijapaniki ila hukubalian na hoja una kitu kichwan, hebu toka nje ya box tujadiliane, nimekupa had mfano,

Nimekwambia hiyo ni Amri na sio maelezo,

Amri zipo Kumi sio Kumi na moja

Walichofanya WAROMA, amri ya kuchonga SANAMU WAMEIONDOA KABISA

AMRI YA KUMI WAKAIGAWA MARA MBILI.ILI KUFIDIA ZIWE KUMI ,

Fananisha amri za Biblia na za katekisimu,

Amri nyingine walioibadilisha kabisa ni AMRI YA 4

Mbona simple tu na ipo wazi, angalia juu kule nimeziandika AMRI ZA MUNGU na ZA KATEKISIMU(ZA PAPA)

NIMEZIFANANISHA MOJA BAADA YA NYINGINE ,View attachment 904495
Kwa ufupi kabisa. Huna unachokijua kaka zaidi ya kukariri. Kifo cha Bwana wetu Yesu Kristo pale msalabani, kilihitimisha rasmi matumizi ya agano la kale, nenda kasome biblia vizuri. Ndio maana niliwakaribisha kwa maswali au semina ndani ya Kanisa Katoliki tuwafundishe neno la Mungu, sio huku mitandaoni. Mmeng'ang'ana na vimistari vya kuotea vya agano la kale mnabaki mnasumbua watu ! Uzuri tumewazoea. Maana huko kwenu inaonekana mmefundishwa kutukana na Kanisa mnaloshambulia kwa nguvu zote ni Katoliki. Mmapoteza muda, kajaribuni mahali pengine !
Huku kwetu kuna watu wametokea kwenye hicho kisacoss chenu wakaja kwenye mafundisho, baada ya kulishwa neno la Mungu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, wameamua kubaki ndani ya kanisa.
Hata hivyo, wewe ni mpumbavu kwa kuwa umejihesabia haki na kuona kama dhehebu lako ni Takatifu na litawafikisha peponi. Nani kakudanganya?
 
izo amri za kwenye chuo kidogo cha sara kwanza sio sahihi zimefupishwa soma kutoka na kumbukumbu latorati
 
Kutoka 20

1 Mungu akanena maneno haya yote akasema,
2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
7 Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
13 Usiue.
14 Usizini.
15 Usiibe.
16 Usimshuhudie jirani yako uongo.
17 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.
Mbona umezirudia zile zile mkuu?

Muwe mnaelewa mnachojifunza nyie wasabato maana kuna mda mnakua kama memory card..yaan ata ikipewa kisichofaa inapokea tu.
 
Mbona umezirudia zile zile mkuu?

Muwe mnaelewa mnachojifunza nyie wasabato maana kuna mda mnakua kama memory card..yaan ata ikipewa kisichofaa inapokea tu.
Akili yako fupi kweli, unaona zinafanana hizo AMRI na hizo za katekisimu?
 
Kwa ufupi kabisa. Huna unachokijua kaka zaidi ya kukariri. Kifo cha Bwana wetu Yesu Kristo pale msalabani, kilihitimisha rasmi matumizi ya agano la kale, nenda kasome biblia vizuri. Ndio maana niliwakaribisha kwa maswali au semina ndani ya Kanisa Katoliki tuwafundishe neno la Mungu, sio huku mitandaoni. Mmeng'ang'ana na vimistari vya kuotea vya agano la kale mnabaki mnasumbua watu ! Uzuri tumewazoea. Maana huko kwenu inaonekana mmefundishwa kutukana na Kanisa mnaloshambulia kwa nguvu zote ni Katoliki. Mmapoteza muda, kajaribuni mahali pengine !
Huku kwetu kuna watu wametokea kwenye hicho kisacoss chenu wakaja kwenye mafundisho, baada ya kulishwa neno la Mungu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, wameamua kubaki ndani ya kanisa.
Hata hivyo, wewe ni mpumbavu kwa kuwa umejihesabia haki na kuona kama dhehebu lako ni Takatifu na litawafikisha peponi. Nani kakudanganya?
Hujui biblia wewe, lenda andiko Yesu alikomesha NEW TESTAMENT

Niletee andiko,
 
HIVI KWANINI KANISA LA ROMA LIMEDANGANYA MAELFU YA WATU KIASI HIKI?

YAANI WATU TOKA WATOTO WANAMEZESHWA AMRI ZA KATEKISIMU , BADALA AMRI ZA MUNGU KUTOKA KTK BIBLIA

KATIKA KIPENGELE HIKI TUTATUMIA
USHAHIDI WA BIBLIA NA, KITABU
CHA KATEKISIMU NDOGO YA
KANISA KATOLIKI UK 56, ILI
KUTIBITISHA;

A. Amri kumi katika biblia KUTOKA
20:1-17 na Amri kumi katika
katekisimu ndogo ya kanisa katoliki;

I. AMRI YA KWANZA KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:1-3
Mimi ni Bwana, Mungu wako,
niliyekutoa katika nchi ya Misri,
katika nyumba ya utumwa.Usiwe na
miungu mingine ila mimi

AMRI YA KWANZA KATIKA
KATEKISIMU
Ndimi Bwana Mungu wako,
usiabudu miungu wengine

II. AMRI YA PILI KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:4-6
Usijifanyie sanamu ya kuchonga,
wala mfano wa kitu cho chote
kilicho juu mbinguni, wala kilicho
chini duniani, wala kilicho majini
chini ya dunia.Usivisujudie wala
kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana,
Mungu wako, ni Mungu mwenye
wivu; nawapatiliza wana maovu ya
baba zao, hata kizazi cha tatu na
cha nne cha wanichukiao, nami
nawarehemu maelfu elfu
wanipendao, na kuzishika amri
zangu

AMRI YA PILI KATIKA KATEKISIMU
Usilitaje bure jina la Mungu wako

III. AMRI YA TATU KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:7
Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu
wako, maana Bwana hatamhesabia
kuwa hana hatia mtu alitajaye jina
lake Bure

AMRI YA TATU KATIKA KATEKISIMU
Shika kitakatifu siku ya Mungu

IV. AMRI YA NNE KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:8-11
Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
Siku sita fanya kazi, utende mambo
yako yote; lakini siku ya saba ni
Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku
hiyo usifanye kazi yo yote, wewe,
wala mwana wako, wala binti yako,
wala mtumwa wako, wala mjakazi
wako, wala mnyama wako wa
kufuga, wala mgeni aliye ndani ya
malango yako. Maana, kwa siku sita
Bwana alifanya mbingu, na nchi, na
bahari, na vyote vilivyomo,
akastarehe siku ya saba; kwa hiyo
Bwana akaibarikia siku ya Sabato
akaitakasa.

AMRI YA NNE KATIKA KATEKISIMU
Waheshimu Baba na Mama, upate
miaka mingi na heri Duniani

V. AMRI YA TANO KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:12
Waheshimu baba yako na mama
yako; siku zako zipate kuwa nyingi
katika nchi upewayo na Bwana,
Mungu wako.

AMRI YA TANO KATIKA KATEKISIMU-
Usiue

VI. AMRI YA SITA KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:13
Usiue.

AMRI YA SITA KATIKA KATEKISIMU
Usizini

VII. AMRI YA SABA KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:14
Usizini

AMRI YA SABA KATIKA KATEKISIMU-
Usiibe

VIII. AMRI YA NANE KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:15
Usiibe

AMRI YA NANE KATIKA KATEKISIMU
Usiseme uongo

IX. AMRI YA TISA KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:16
Usimshuhudie jirani yako uongo

AMRI YA TISA KATIKA KATEKISIMU
Usitamani mwanamke asiye mke
wako

X. AMRI YA KUMI KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:17
Usiitamani nyumba ya jirani yako,
usimtamani mke wa jirani yako; wala
mtumwa wake, wala mjakazi wake,
wala ng'ombe wake, wala punda
wake, wala cho chote alicho nacho
jirani yako

AMRI YA KUMI KATIKA KATEKISIMU
Usitamani mali ya mtu mwingine
View attachment 901465
Ishu ni namba au ni ufupi maana naona maana ni moja tu except kwenye sabato kidogo wamechakuchua
 
Hujui biblia wewe, lenda andiko Yesu alikomesha NEW TESTAMENT

Niletee andiko,
Hatuna tendency ya kulumbana na watu waovu, ilinididi nikujibu sababu uzalendo ulinishinda. Ndio maana nikasema sio lazima utetee unachokiamini kwa kushambulia Kanisa Katoliki, na hapo nimediriki kukuita wewe ni mpumbavu. Hata kiingereza hukijui. Siku hizi new testament imekuwa agano la kale ? NARUDIA KUSEMA, nendeni mkasome maandiko vizuri, msikariri vifungu, na mkiishapata ukweli kwa mujibu wa tafsiri yenu, hakuna haja ya kudhihaki wengine wenye mitazamo tofauti na ya kwenu. Sijui hata unaabudu wapi. Sitaki kuamini kama huko unakoabudu mnamuhuburi Mungu huyu anayehubiriwa na watu wote au mnafundishwa matusi. Badilika Brother. You seem to be much know but i want to assure you, spiritually, you are empty minded ! Kanisa Katoliki ni kisima cha maarifa, na hutakaa ujue ni nini tunakifanya kwa kuwa akili yako imefungwa, na huko tayari kudadisi. Mtabaki kusema wanaabudu sanamu, mara ho wanasali jumapili n.k, ili mpate wafuasi wapya. Wapo waliokuja na matusi kama wewe na walipojua ukweli wamebaki kimya na wapo wanaendelea kumtukuza Mungu.
Pointi yangu ni kwamba jaribuni kuwa wastaarabu, mnaudhi sana mnapotetea hoja zenu kwa njia ya matusi na tena mbaya wenu ni Kanisa Katoliki. none sense ! Mnakiuka hata sheria za Nchi. Ni kweli Serikali haina dini, lakini watu wa aina yako ndio mnaosababisha chuki katika jamii pasipo kujua kwa kuwa hamjui impact ya mnachokifanya.

Baaada ya kusema hayo, nimefunga rasmi mjadala na wewe. Ikiwa u uchi halafu kichaa akachukua nguo zako na kuanza kukimbia nazo, ukianza kumfukuza kichaa ili akurudishie nguo, wapita njia watadhani wote nyie ni vichaa. Nakutakia tafakuri njema !
 
Kutoka 20

1 Mungu akanena maneno haya yote akasema,
2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
7 Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
13 Usiue.
14 Usizini.
15 Usiibe.
16 Usimshuhudie jirani yako uongo.
17 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.
Aksante sana mkuu kwa kutiririka. Kumbe amri za "Mungu" ni 17!!!?
Lakini mkuu napata shida kidogo kama kweli Musa alikuwa akiongea na Mungu wakati akipewa amri hizo. Kulingana na nukuu yako hapo juu amri hizi za 5, 7, 10, 11 na 12 zinanichanganya, ni kama vile Musa alikuwa akipewa amri hizo na mtu mwengine!
 
Hatuna tendency ya kulumbana na watu waovu, ilinididi nikujibu sababu uzalendo ulinishinda. Ndio maana nikasema sio lazima utetee unachokiamini kwa kushambulia Kanisa Katoliki, na hapo nimediriki kukuita wewe ni mpumbavu. Hata kiingereza hukijui. Siku hizi new testament imekuwa agano la kale ? NARUDIA KUSEMA, nendeni mkasome maandiko vizuri, msikariri vifungu, na mkiishapata ukweli kwa mujibu wa tafsiri yenu, hakuna haja ya kudhihaki wengine wenye mitazamo tofauti na ya kwenu. Sijui hata unaabudu wapi. Sitaki kuamini kama huko unakoabudu mnamuhuburi Mungu huyu anayehubiriwa na watu wote au mnafundishwa matusi. Badilika Brother. You seem to be much know but i want to assure you, spiritually, you are empty minded ! Kanisa Katoliki ni kisima cha maarifa, na hutakaa ujue ni nini tunakifanya kwa kuwa akili yako imefungwa, na huko tayari kudadisi. Mtabaki kusema wanaabudu sanamu, mara ho wanasali jumapili n.k, ili mpate wafuasi wapya. Wapo waliokuja na matusi kama wewe na walipojua ukweli wamebaki kimya na wapo wanaendelea kumtukuza Mungu.
Pointi yangu ni kwamba jaribuni kuwa wastaarabu, mnaudhi sana mnapotetea hoja zenu kwa njia ya matusi na tena mbaya wenu ni Kanisa Katoliki. none sense ! Mnakiuka hata sheria za Nchi. Ni kweli Serikali haina dini, lakini watu wa aina yako ndio mnaosababisha chuki katika jamii pasipo kujua kwa kuwa hamjui impact ya mnachokifanya.

Baaada ya kusema hayo, nimefunga rasmi mjadala na wewe. Ikiwa u uchi halafu kichaa akachukua nguo zako na kuanza kukimbia nazo, ukianza kumfukuza kichaa ili akurudishie nguo, wapita njia watadhani wote nyie ni vichaa. Nakutakia tafakuri njema !
Acha bla blaa nyingi,

Kwanini usijibu hoja

Nimekuomba vifungu ,unakuja na porojo na kuaga ,

Uvimilivu unakushinda maaana huna aya bali una MAPOKEO YA WANADAMU
 
Aksante sana mkuu kwa kutiririka. Kumbe amri za "Mungu" ni 17!!!?
Lakini mkuu napata shida kidogo kama kweli Musa alikuwa akiongea na Mungu wakati akipewa amri hizo. Kulingana na nukuu yako hapo juu amri hizi za 5, 7, 10, 11 na 12 zinanichanganya, ni kama vile Musa alikuwa akipewa amri hizo na mtu mwengine!
Hazipo 17 ,1-17 hizo ni Aya

Mfano kutoka 20:8-11 hiyo ni amri 1

Hizo Amri Musa alipewa na MUNGU MLIMAN SINAI
 
Ishu ni namba au ni ufupi maana naona maana ni moja tu except kwenye sabato kidogo wamechakuchua
Sio kwenye sabato tu, amri ya kukataza KUCHONGA SANAMU UMEIONA HAPO?

amri ya 10 wameigawa vipande viwili kufidia hiyo ILIYOKATAZA KUCHONGA SANAMU,

YA SABATO wameichakachua kabisa
 
MBINGU ZITAPITA ILA MANENO HAYA HAYATAPITA KAMWE...........

“Msidhani [wengi mno leo wanadhani] ya kuwa nalikuja kuitangua torati [Sheria] au manabii;” akasema, “sikuja kutangua [kuifutilia mbali], bali kutimiliza [kuitekeleza]. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka [bado zipo], yodi moja [,] wala nukta moja [.] HAITAONDOKA hata yote yatimie [yaani, mpaka hapo mbingu na nchi
zitakapoondoka]. Basi [kwa hiyo] mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo [Yak.2:10-12], na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa [mnyonge hataingia – Ufu.21:27] katika ufalme wa mbinguni; bali mtu ATAKAYEZITENDA [Amri Kumi] NA KUZIFUNDISHA, huyo ataitwa mkubwa [mtawala/mfalme – Ufu.20:4; Dan. 7:27] katika ufalme wa mbinguni.” Mathayo 5:17-19.

HAYA ENDELEENI KUKUMBATIA AMRI ZA KWENYE KATEKISIMU
FB_IMG_1540120406498.jpeg
 
UPAPA KUZIFANYIA MAREKEBISHO TENA AMRI KUMI ZA MUNGU. .

Baada ya Upapa kuzibadili Amri kumi za Mungu kipindi cha nyuma, sasa Wanazifanyia marekebisho tena. . .
Sasa zitakuwa 11, kwa mujibu wa Taarifa ya msemaji wa kanisa katoriki Fr. FEDERICO LOMBARDI amesema amri hizi 11 kwasasa zinaandikwa kwenye jiwe na mtaalamu wa maandishi wa kiitaliano na baada ya kumaliza kazi hiyo, Amri hizo zitaoneshwa kutoka kwenye Uwanja wa St.PETER'S SQUARE kwa njia ya Tv ili dunia nzima ipate Kutazama.

http://realnewsrightnow.com/2015/07...instructed-me-to-revise-the-ten-commandments/
FB_IMG_1540123568316.jpeg
 
Back
Top Bottom