Tujikumbushe Amri kuu za Mungu

Tujikumbushe Amri kuu za Mungu

Mkuu siyo ww tu hata mm amri no 6 na 9 zimenishinda kabisa nadhani shetani akiniona nazivunja huwa anakaa pembeni huku akipiga K Vant yake tenza hiz chupa mpya..
 
mm ninachojua amri kuu ni upendo....mpende jirani yako kama unavyojipenda ww na wala usimteke.......NEIGHBORHOOD PRINCIPLE.....Neighbor principle is a principle of English law which says that a person should take reasonable care to avoid acts or omissions that s/he can reasonably foresee as likely to cause injury to the neighbor. Lord Atkin....
 
Kuchonga sanam ambapo katka maana usiabudu miungu wengne (miti, ng'ombe, shetan)
Lakn unaweza kujiulza sanam za kanisa katorik zinakuaje sasa? Ule n utamadun tu wa watu wa Israel ambapo kuweka sanamu haimaanisha kwamba maombi yanaenda kwa hzo sanam n mapambo tu ya kikanisa zaid
Ulishawahi kujiuliza kwanini Amri inayokataza kuchonga sanamu waliiondoa?
 
Nashangaaga sana watu wanasema amri ya 6 ni USIZINI, yaani roma ndio maana BIBLIA INAMUITA MAMA WA MAKAHABA, ambaye amewanyweshwa mataifa mvinyo wa uasherati wake,

Yaani mtu utamkuta ana biblia kubwa jimapili anakaa siti ya mbele, anakwambia AMRI YA 6 USIZINI, hapo ndipo nasemaga ACHA ROMA IITWE ROMA
We ulitaka iwe ipi kama sio hiyo?!
 
Wasabato, Wa napenda vitabu vdogo dogo vilivyoandikwa na wenyewe wanaita" UNABII" ( huwaambii chochote juu hilo)

HGW ni kiumbe bora kwao, kanisa Catholic ktk miongozo yake halishughuliki na chochote kinachohusu UNABII fake Wa SDA.

LKN SDA kila kukicha hawawezi kusimama bila CATHOLIC .

Zama na Zama Leo hii uzungumzie kueneza injili kwa farasi? Au utupe jiwe ndio safari yako iwe mwisho?

Mengine yaliwahusu Wanaisrael, mengine ni simulizi kujiongeza na kukubali mmejiongeza ni sadaka.
 
Hizi ni Amri zilizochakachuliwa na kanisa la ROMA ,

Watu maelfu mmemezeshwa amri zilizochakachuliwa na kuwekwa kwenye katekisimo, Zile Amri kumi ORIGINAL alizopewa musa pale SINAI, zipo kwenye biblia hata hamtaki kuzifatilia ,mfananishe na hizo za PAPA
Unasema zimechakachuliwa, lakini huna na huzijui! Huoni kuwa wewe ni punguani?
 
1.Usiabudu miungu wengine.
2. Usiape bure kwa jina la Mungu wako.
3. Shika Kitakatifu Siku ya Mungu wako
4. Waheshimu Baba na Mama, upate miaka mingi na heri duniani.
5. Usiue
6. Usizini
7. Usiibe
8. Usiseme uongo
9. Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10. Usitamani mali ya watu.
Uliye andika hizi amri Nina mashaka nawe
Wapi katika Biblia wameandika shika kitakatifu siku ya Mungu???!!!!
Soma Biblia nanukuu maandiko

kutoka 20:1-17

Amri kumi za MUNGU

20 Mungu akanena maneno haya yote akasema,2Mimi ni BWANA Mungu wako niliyekutoa katika nchi ya misri,katika nyumba ya utumwa.
3Usiwe na miungu mingine Ila mimi.
4Usijifanyie sanamu ya kuchonga,wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni,wala kilicho chini duniani,wala kilicho majini chini ya dunia.
5Usivisujudie wala kuvitumikia;kwa kuwa Mimi,BWANA,Mungu wako,ni Mungu mwenye wivu;nawapatiliza wana maovu ya baba zao,hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao,na kuzishika amri zangu
7Usilitaje bure jina la BWANA,
Mungu wako,maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajae jina lake bure.
8Ikumbuke siku ya sabato uitakase
9Siku sita Fanya kazi,utende mambo yako yote;10lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA,Mungu wako,siku hiyo usifanye kazi yoyote,wewe,wala mwana wako,wala binti yako,wala mtumwa wako,wala mjakazi wako,wala mnyama wako wa kufuga,wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
11Maana,kwa siku sita BWANA alifanya mbingu,na nchi,na bahari,na vyote vilivyomo,akastarehe siku ya saba;kwahiyo bwana akaikaribia siku ya sabato akaitakasa.
12Waheshimu baba yako na mama yako;siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA,Mungu wako.

13Usiue
14Usizini
15Usiibe
16Usimshuhudie jirani yako uongo
17Usitamani nyumba ya jirani yako,usimtamani mke wa jirani yako;wala mtumwa wake,wala mjakazi wake,wala ng'ombe wake,wala punda wake,wala chochote alicho nacho jirani yako.
 
HIVI KWANINI KANISA LA ROMA LIMEDANGANYA MAELFU YA WATU KIASI HIKI?

YAANI WATU TOKA WATOTO WANAMEZESHWA AMRI ZA KATEKISIMU , BADALA AMRI ZA MUNGU KUTOKA KTK BIBLIA


KATIKA KIPENGELE HIKI TUTATUMIA
USHAHIDI WA BIBLIA NA, KITABU
CHA KATEKISIMU NDOGO YA
KANISA KATOLIKI UK 56, ILI
KUTIBITISHA;

A. Amri kumi katika biblia KUTOKA
20:1-17 na Amri kumi katika
katekisimu ndogo ya kanisa katoliki;


I. AMRI YA KWANZA KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:1-3
Mimi ni Bwana, Mungu wako,
niliyekutoa katika nchi ya Misri,
katika nyumba ya utumwa.Usiwe na
miungu mingine ila mimi

AMRI YA KWANZA KATIKA
KATEKISIMU
Ndimi Bwana Mungu wako,
usiabudu miungu wengine

II. AMRI YA PILI KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:4-6
Usijifanyie sanamu ya kuchonga,
wala mfano wa kitu cho chote
kilicho juu mbinguni, wala kilicho
chini duniani, wala kilicho majini
chini ya dunia.Usivisujudie wala
kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana,
Mungu wako, ni Mungu mwenye
wivu; nawapatiliza wana maovu ya
baba zao, hata kizazi cha tatu na
cha nne cha wanichukiao, nami
nawarehemu maelfu elfu
wanipendao, na kuzishika amri
zangu

AMRI YA PILI KATIKA KATEKISIMU
Usilitaje bure jina la Mungu wako

III. AMRI YA TATU KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:7
Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu
wako, maana Bwana hatamhesabia
kuwa hana hatia mtu alitajaye jina
lake Bure

AMRI YA TATU KATIKA KATEKISIMU
Shika kitakatifu siku ya Mungu

IV. AMRI YA NNE KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:8-11
Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
Siku sita fanya kazi, utende mambo
yako yote; lakini siku ya saba ni
Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku
hiyo usifanye kazi yo yote, wewe,
wala mwana wako, wala binti yako,
wala mtumwa wako, wala mjakazi
wako, wala mnyama wako wa
kufuga, wala mgeni aliye ndani ya
malango yako. Maana, kwa siku sita
Bwana alifanya mbingu, na nchi, na
bahari, na vyote vilivyomo,
akastarehe siku ya saba; kwa hiyo
Bwana akaibarikia siku ya Sabato
akaitakasa.


AMRI YA NNE KATIKA KATEKISIMU
Waheshimu Baba na Mama, upate
miaka mingi na heri Duniani


V. AMRI YA TANO KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:12
Waheshimu baba yako na mama
yako; siku zako zipate kuwa nyingi
katika nchi upewayo na Bwana,
Mungu wako.

AMRI YA TANO KATIKA KATEKISIMU-
Usiue

VI. AMRI YA SITA KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:13
Usiue.

AMRI YA SITA KATIKA KATEKISIMU
Usizini

VII. AMRI YA SABA KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:14
Usizini

AMRI YA SABA KATIKA KATEKISIMU-
Usiibe

VIII. AMRI YA NANE KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:15
Usiibe

AMRI YA NANE KATIKA KATEKISIMU
Usiseme uongo

IX. AMRI YA TISA KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:16
Usimshuhudie jirani yako uongo

AMRI YA TISA KATIKA KATEKISIMU
Usitamani mwanamke asiye mke
wako

X. AMRI YA KUMI KATIKA BIBLIA
KUTOKA 20:17
Usiitamani nyumba ya jirani yako,
usimtamani mke wa jirani yako; wala
mtumwa wake, wala mjakazi wake,
wala ng'ombe wake, wala punda
wake, wala cho chote alicho nacho
jirani yako

AMRI YA KUMI KATIKA KATEKISIMU
Usitamani mali ya mtu mwingine
View attachment 901465
God bless you umewafunulia wengi upeo wa kuona

Upande wa pili hawapendi kuambiwa ukweli
 
Back
Top Bottom