Tujikumbushe: Ahadi/Vipaumbele vya Rais Magufuli

Tujikumbushe: Ahadi/Vipaumbele vya Rais Magufuli

Habari wanajamvi, ninaomba tukumbushane ahadi za mheshimiwa rais John Pombe Magufuli kwa wananchi alipokuwa katika mikutano ya kampeni maeneo mbalimbali ya nchi yetu.

Bado moja kubwa hajaitekeleza sijui kwa nini anaichelewesha na ni ile ya kulimia meno mbona hatujaanza mi naitaka
 
Alisema atamfunga yule fisadi aliyenunua kivuko kibovu na kuuza nyumba za serikali.
Hapo ndipo napasubiria
 
Aliahidi kila mwanafunzi atakayechaguliwa chuo kikuu atapata mkopo kwa asilimia mia
 
Kuifanya Tz kuwa ya viwanda

Kuifikisha uchumi wa kati

Maslahi ya wafanyakazi kuboreshwa

Mikopo kupatikana vyuoni

Maji kupatikana
 
Kuifanya Tz kuwa ya viwanda

Kuifikisha uchumi wa kati

Maslahi ya wafanyakazi kuboreshwa

Mikopo kupatikana vyuoni

Maji kupatikana
Mangapi yameshaanza kufanyiwa kazi. Hili la maji naona kabisa moyo wa dhati ya serikali ya awamu ya tano. Ila hili la wafanyakazi na maslahi yao, mhhh! Kuna ukakasi hapo
 
Kuivunja CDA

Kuanzisha mahakama ya mafisadi

Kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri

Elimu bure mpaka kidato cha nne

Ujenzi daraja la busisi

-Milioni 50 kila kijiji
-Nchi ya viwanda
-Mikopo elimu ya juu
-Kulala nao mbele mafisadi

Hivi kwani kila kilichoandikwa kwenye ilani ni ahadi yake???
 
Habari wanajamvi, ninaomba tukumbushane ahadi za mheshimiwa rais John Pombe Magufuli kwa wananchi alipokuwa katika mikutano ya kampeni maeneo mbalimbali ya nchi yetu.




kila kijiji kupewa sh 50000/=, elimu bure kuanzia shule za msingi, kidato cha kwanza mpaka cha nne, watumishi kuboreshewa maslahi ya kazi, n.k
 
Ujenzi wa kiwanja cha ndege chato, ununuzi wa Bombardier, kuzuia mikutano ya kisiasa, wasichana wanaopata ujauzito hamna kurudi shuleni, watu walioishi maisha ya kimalaika kuishi kishetani, makato ya 15% kutoka bodi ya mikopo kwa watumishi, kuteua na kutengua watu, kudorora kwa uchumi kunakopelekea maisha magumu mitaani na usumbufu wa uhakiki usioisha.

2020 hata sio mbali.
 
Back
Top Bottom