Tujikumbushe: Ahadi/Vipaumbele vya Rais Magufuli

Tujikumbushe: Ahadi/Vipaumbele vya Rais Magufuli

Habari zenu familia ya JF.
Naomba niwakumbushe ahadi nazokumbuka kipindi kile Magufuli akituomba kura.

1. Wanafunzi watapata mikopo bila kuchelewesha: PESA yenyewe mkopo kwanini ichelewe, alisema.
2. Nitamaliza kero za MAJI.
3. Nitamaliza tatizo sugu la dawa hospitalini.
4. Million 50 kila kijiji.
5. Meli kubwa ziwa Victoria, Tanganyika, Rukwa nk nk.
6. Zahanati kila kijiji, kituo cha AFYA kila kata na hospital ya rufaa kila MKOA .
7. Nitaigeuza Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.
8. Tanzania haitakuwa ombaomba kwenye utawala wangu
9. Nitatengeneza nafasi nyingi za ajira kwa vijana.
10. Nitaunda MAHAKAMA maalum ya majizi na mafisadi ili niwafunge.
11.Serikali yangu itawajali sana wakulima na wafugaji ili wainuke kiuchumi.

Nawe tiririka kama unakumbuka alikuombaje kura
 
Wapinzani wengi hawataki kukosoa katika eneo hili la ahadi kwa kuwa wanajua magufuli anatekeleza ahadi zake kwa kiwango kikubwa.
 
Habari zenu familia ya JF.
Naomba niwakumbushe ahadi nazokumbuka kipindi kile Magufuli akituomba kura.

1. Wanafunzi watapata mikopo bila kuchelewesha: PESA yenyewe mkopo kwanini ichelewe, alisema.
2. Nitamaliza kero za MAJI.
3. Nitamaliza tatizo sugu la dawa hospitalini.
4. Million 50 kila kijiji.
5. Meli kubwa ziwa Victoria, Tanganyika, Rukwa nk nk.
6. Zahanati kila kijiji, kituo cha AFYA kila kata na hospital ya rufaa kila MKOA .
7. Nitaigeuza Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.
8. Tanzania haitakuwa ombaomba kwenye utawala wangu
9. Nitatengeneza nafasi nyingi za ajira kwa vijana.
10. Nitaunda MAHAKAMA maalum ya majizi na mafisadi ili niwafunge.
11.Serikali yangu itawajali sana wakulima na wafugaji ili wainuke kiuchumi.

Nawe tiririka kama unakumbuka alikuombaje kura
Ongeza ile ya kuyatwaa mashamba yasiyoendelezwa kama ya kina Sumaye
 
Wiki hii ilikuwa ni ya ufunguzi wa miradi mbakimbali ukiwemo mradi mkubwa wa Reli ya kiwango
 
Ahadi alizotoa magufuli kipindi anaomba kura ikiwemo milioni 50 kila kijiji endapo atachaguliwa kuwa rais wa Tanzania

Mgombea huyo alitoa ahadi mbalimbali ikiwamo ajira akisema: “Ninataka Watanzania wapate ajira, kazi ya Serikali itakuwa kukusanya kodi tu. Viwanda vinaweza kutengeneza ajira kwa asilimia 40 hasa kwa vijana wanaohitimu vyuo mbalimbali nchini.”

Kuhusu ubinafsishaji, alisisitiza: “Kuna viwanda vilibinafsishwa sasa wahusika wasipoviendeleza wajiandae kuvirudisha haraka.”

Mbali na kurejesha viwanda vilivyobinafsishwa, alisema akipewa ridhaa hiyo atahakikisha chini ya uongozi wake, anajenga viwanda vingi vipya, akiainisha vile mahsusi kwa shughuli za kilimo, mifugo, kusindika nyama na madini.

Alitaja kipaumbele kingine kuwa ni kilimo na kwamba atahakikisha sekta hiyo ambayo ndiyo mhimili wa uchumi inaendelezwa.

“Tutaleta vitendea kazi, pembejeo na vifaa vingi vya kisasa na vya kutosha kwa wakulima… kama nilivyosema hapo awali, tutajenga viwanda kwa ajili ya wakulima pia.

Mbunge huyo wa zamani wa Chato alisema pia kipaumbele kingine katika Serikali yake ni kuhakikisha kuwa wananchi wa mjini wanapata majisafi na salama kwa asilimia 95 na wananchi wa vijijini wanapata maji kwa asilimia 85.

Kuhusu afya alisema: “Tutahakikisha tunakuwa na vituo vya afya, zahanati na hospitali katika maeneo mbalimbali kwa sababu tunaamini maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana kama wananchi hawana afya bora.”

Kipaumbele kingine ni mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu akisema watakuwa wanapata mikopo kwa wakati bila kuchelewa na kwamba watajikita pia katika kujenga hosteli kwa wanafunzi wa vyuo.

“Mishahara ya walimu na wafanyakazi wote tutaishughulikia. Hata madereva haki zao za msingi lazima ziangaliwe,” alisema huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho.

Mgombea huyo alisema anafahamu kero ya msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam na kwamba maendeleo ya kweli yatapatikana kama changamoto hiyo itafanyiwa kazi.

“Tutaunganisha mikoa yote kwa barabara zenye viwango vya lami na pia tutajenga barabara za juu saba jijini hapa,” alisema Magufuli.

Alisema akipewa ridhaa hiyo itashughulikia suala la reli kwa kujenga reli ya kisasa kwa viwango vya Standard Gauge” na kuboresha bandari na usafiri wa anga.

Kuhusu maliasili, alisema ni kipaumbele katika Serikali yake endapo akipewa ridhaa ya kuongoza nchi huku akieleza kukerwa na ujangili... “Ninapata shida sana ninapoona meno ya tembo yanauzwa Ulaya halafu unaambiwa yanatoka Tanzania… sasa unajiuliza yanapitaje?”

Alisema ili kushughulikia suala hilo atahakikisha watendaji wa sekta hiyo wanaboreshewa masilahi yao ili wachangie mapato ya nchi.

Aliahidi Serikali yake kuwa rafiki wa wawekezaji na kwamba italinda masilahi ya wafanyabiashara.

Mgombea urais huyo aliahidi kuwa atalinda uhuru wa habari na atafanya kazi na waandishi wa habari siyo tu wakati wa kipindi cha kampeni, bali hata baada.

Katika ahadi zake, Dk Magufuli hakuwaacha wasanii, alisema atahakikisha wanapata hakimiliki na kuhakikisha wao pamoja na wanamichezo wanaanzishiwa mfuko kwa ajili ya kuwasaidia katika mambo mbalimbali.
 
Wajameni miaka mitano haijesha bado,tuvute subra,mie nasubiri utekelezaji wa kugawa laptop kwa waalimu inchi nzima.
 
Habari wandugu.

Wakati Ule Tuliambiwa Gesi Ndio Muarobaini Wa Tatizo La Umeme, Tena Tukaambiwa Ipo Ya Kutosha Hadi Kuuza Nje, Sasa Gesi Imezikwa Agenda Ni Stiglers, Tujiulize Tumeshapata Faida Ya Uwekezaji Kwenye Gesi? Kwann Tumebadili Mawazo?Je badae Hawataikana Stiglers Kama Walivyoikana Gesi?

Mpk sasa hatujui tunataka nini na kwa wakati gani na vipaumbele vyetu ni vipi? Tatizo linaanzia hapa.

mr mkiki.
 
Najua Mheshimiwa ni msomaji mzuri wa hii mitandao.
Mimi naanza na ahadi hii;

Mheshimiwa ni miaka miwili na kidogo imebaki ili umalize muda wako wa Uraisi kwa "Mujibu wa Sheria", Vipi ile ahadi ya SHILINGI MILIONI HAMSINI kila kijiji? Tupatie basi hata nusu yake kwanza!
 
Zahanati kila kijiji na kujenga daraja kutoka mwanza mpaka sengerema
 
Back
Top Bottom