Tujikumbushe: Ahadi/Vipaumbele vya Rais Magufuli

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,951
29,532
1. Umoja wa Taifa
2. Kulinda Muungano wa Tanzania.
3. Ulinzi na usalama
4. Kuheshimu mihimili ya Dola.
5. Mahakama maalum ya mafisadi na majizi
5. Utawala bora
7. Ataheshimu mawazo yote ya kuleta maendeleo hata yakitoka upinzani
8. Ataimarisha vyombo vya usalama
9. Vita dhidi ya ubadhirifu
10. Kodi ilipwe na wote
11. Ataongeza ajira kwa kuimarisha viwanda vya ndani
12. Sekta ya kilimo itaimarishwa
13. Sekta ya mifugo itaimarishwa ili iwe na tija kwa kujenga viwanda
14. Madini yatadhibitiwa ili yalete maendeleo.
15. Maji yatapelekwa Vijijini na mijini
16. Zahanati kila kijiji, Hospitali ya rufaa kila mkoa, kuboresha maslahi ya wauguzi
17. Elimu bure hadi kidato cha nne, nyumba za walimu zitajengwa.
18. Wanafunzi wa vyuo vikuu, atahakikisha mikopo inakwenda mapema ili wasome
19. Kujenga hostel za mwana vyuo
20. Maslahi ya watumishi, kila mtu anayefanya kazi atapata haki yake.
21. Gesi itasimamiwa vyema ili isaidie nchi
22. Barabara zitaboreshwa, flyovers kujenga ya kwanza salander, tazara
23. Msongamano Dsm utashughulikiwa
24. Reli itajengwa upya
25. Bandari, anga zitaboreshwa
26. Maslahi ya maliasili yataboreshwa ili watalii wengi waje ili tupate pesa
27. Serikali itakuwa rafiki kwa wawekezaji wenye nia njema
28. Maslahi ya wafanyakazi yatalindwa
29. Walemavu watalindwa na haki zao zitalindwa
30. Uhuru wa Habari utalindwa na atakuwa na waandishi karibu
31. Wasanii na wanamichezo haki zao zitalindwa, kutakuwa na Mfuko maalum kwa ajili hiyo
32. Reli ya Dar itajengwa.

Tunapojadili bajeti bungeni, tujikite kwenye haya. Tunapopingana na hoja za Rais, tukumbuke haya.

[HASHTAG]#HAPAKAZITU[/HASHTAG][l
 
Mwisho wa siku tutampima kwa hayo, lkn pia asiharibu misingi ya utaifa iliyojengwa na waasisi
 
Mtazamo wangu hadi kufikia unaandika haya ni huu:
1. Umoja wa Taifa - Fail, taifa linazidi kuparaganyika
2. Kulinda Muungano wa Tanzania. Pass, japo nguvu ya dola kwa wananchi imezidi
3. Ulinzi na usalama - 50% Ulinzi upo usalama hakuna
4. Kuheshimu mihimili ya Dola. Fail, anatawala mihili yote kwa kutumia usalama wa taifa. simpi ya mahakam kwa kuwa kwa maneno yake bado hafurahii maamuzi yao.
5. Mahakama maalum ya mafisadi na majizi - Pass - Sema ndio hajafungwa hata mmoja, means so far hawapo.
5. Utawala bora - Fail from day one
7. Ataheshimu mawazo yote ya kuleta maendeleo hata yakitoka upinzani - Fail from day one
8. Ataimarisha vyombo vya usalama - Pass, I think kwa kuwa anavitumia yeye kwa faida zake
9. Vita dhidi ya ubadhirifu - Sina hakika
10. Kodi ilipwe na wote - Sina hakika na hili
11. Ataongeza ajira kwa kuimarisha viwanda vya ndani - Hii bado sana
12. Sekta ya kilimo itaimarishwa - Bado sana, na asipoangalia kwake kilimo kitakuwa sio uti wa mgongo tena
13. Sekta ya mifugo itaimarishwa ili iwe na tija kwa kujenga viwanda - Bado
14. Madini yatadhibitiwa ili yalete maendeleo - Bado, kwenye mchakato
15. Maji yatapelekwa Vijijini na mijini - Labda baada ya kuingia Professor yule
16. Zahanati kila kijiji, Hospitali ya rufaa kila mkoa, kuboresha maslahi ya wauguzi - Bado sana
17. Elimu bure hadi kidato cha nne, nyumba za walimu zitajengwa. 50% the former yes, the later hamna kitu
18. Wanafunzi wa vyuo vikuu, atahakikisha mikopo inakwenda mapema ili wasome - Bado haijakaa sawa
19. Kujenga hostel za mwana vyuo - 25% UDSM yes, the rest bado
20. Maslahi ya watumishi, kila mtu anayefanya kazi atapata haki yake. - Sina hakika na hili, kwangu mashahara wangu napokea kama zamani tu vilevile
21. Gesi itasimamiwa vyema ili isaidie nchi - Haieleweki bado
22. Barabara zitaboreshwa, flyovers kujenga ya kwanza salander, tazara - Kinadharia tayari kiutekelezaji bado
23. Msongamano Dsm utashughulikiwa - Bado sanaaa, tunalala kila siku njiani
24. Reli itajengwa upya - bado ipo katika wakati ujao
25. Bandari, anga zitaboreshwa - 50% Ndege zimenunuliwa, sina hakika na maboresho mengine mana anga si kununua ndege tu
26. Maslahi ya maliasili yataboreshwa ili watalii wengi waje ili tupate pesa - Takwimu zilizotolewa za watalii kuongezeka sijazipitia bado kupata ukweli wake. Ila walio sehemu za utalii bado wanalalamika
27. Serikali itakuwa rafiki kwa wawekezaji wenye nia njema - Ukiacha Dangote ambaye aliletwa na Kikwete, bado sana, ndio kwanza mazingira tunayotengeza yanawafanya wawekezaji wajiulize mara mbilimbili
28. Maslahi ya wafanyakazi yatalindwa - Sina hakika alimaanisha maslahi gani hapa, kwangu sioni tofauti na utawala uliopita
29. Walemavu watalindwa na haki zao zitalindwa - Bado, ameteua walemavu kwenye wizara, tunampongeza kwa hilo, lakini sijaona mabadiliko
30. Uhuru wa Habari utalindwa na atakuwa na waandishi karibu - Fail Fail Fail
31. Wasanii na wanamichezo haki zao zitalindwa, kutakuwa na Mfuko maalum kwa ajili hiyo - Hadi sasa bado hakieleweki ndio mana wanamlilia Mwakyembe na mkuu wa mkoa
32. Reli ya Dar itajengwa. - Kinadharia tumeona leo, utekelezaji bado, wakati ujao
 
NAWAKUMBUSHENI TU AHADI KUBWA SITA ZA RAIS MAGUFULI (CCM), KWA WATANZANIA WAKATI ANAGOMBEA.

Naomba tusaidiane kukumbushana hapa yaliyotekelezwa kwa ufanisi mpaka sasa, kati ya hizi ahadi kubwa sita (06) kwa Watanzania.

1. Milioni 50 kwa kila kijiji

2. Kujenga vituo vya Afya kwa ngazi za Kata zote na Zahanati ngazi za Vijiji.

3. Ufufuaji wa viwanda

4. Ununuzi wa meli mpya

5. Kuanzisha mahakama maalum ya mafisadi na kuanza kufanya kazi baada ya tu ya kuchaguliwa.

6. Kutoa Elimu bure kuanzia chekechea hadi kidato cha nne.

NIKUMBUSHENI HATA AHADI MOJA TU ILIYOFANYIKA KIKAMILIFU.

Joseph Mohonia Politician
 
Muda ni muamuzi mzuri sana....nitakuja kukurudisha kwenye uzi huu mapema 2020
 
Mgombea wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, akihutubia mkutano wa kampeni mjini Tunduma mkoa wa Songwe jana.

PICHA: ADAM MZEE
Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amewapooza wagombea wa chama hicho waliodondoshwa kwenye kura za maoni kwa kuwaahidi atawapa ajira hivyo kuwataka wasikikimbie chama hicho.

Hali kadhalika, Dk. Magufuli amewataka wana-CCM hao kutoendeleza makundi kwa kuwa yatahatarisha ushindi wa chama hicho. Aidha, amewaombea msamaha wagombea wa Majimbo ya Sumbawanga Mjini, Kwela, Kalambo mkoani Rukwa na Momba mkoani Sogwe.

"Nawaomba muwasamehe saba mara sabini kwa kuwa hawachagui malaika bali binadamu ambaye siyo mkamilifu," alisema Dk. Magufuli.

Alisema yawezekana yapo ambayo hawakuyatekeleza kama inavyotakiwa na makosa mengine ambayo yamekuwa kinyume na matarajio ya wananchi, lakini anawahitaji afanye nao kazi na ahadi zote watakazoahidi watazitekeleza kwa maendeleo endelevu ya wananchi.
ATAKA MAKUNDI YAVUNJWE

Akiwa Jimbo la Kwela ambalo mgombea wake ni Ignus Malocha, alisema kura za maoni zimeisha na kinachotakiwa ni kuvunja makundi na kufanya kazi ya kuipa ushindi CCM.

"Inawezekana mbunge wenu hakufanya hadi mlipotarajia, namuombea msamaha kweli kweli, nipeni, huyu ni binadamu hatuchagui malaika, mchagueni Malocha msihadaishwe na maneno mengi," alisisitiza.

Akiwa Jimbo Kalambo ambalo mgombea wake ni Josephat Kandege, alisema waliobwagwa kura za maoni hawapaswi kulalamika na kuacha kuunga mkono mgombea aliyepita, kwani akiwa rais nafasi za kazi zitakuwa nyingi kila mmoja atapata.

"Nakwenda kuwa rais, nafasi za kazi ni nyingi sana. Mligombea kwa kuwa mnataka kufanya kazi, nitawapa kazi, lakini hakikisheni huyu anashinda," alisema.

Katika Jimbo la Momba ambalo mgombea wake ni Dk. Lucas Siyame, alirejea ombi la msamaha kwa wananchi hao kwa kuwa mgombea huyo alihimiza ujenzi wa barabara ya Sumbawanga hadi Tunduma, lakini kwa sababu ambazo hazieleweki walimuangusha.

"Tunaambiwa tusamehe saba mara sabini, kama kuna dhambi aliifanya msameheni na ikifika Oktoba 25, mmpe kura za ndiyo," alisema.

Alisema wagombea wengine wasiwe na shaka kwani serikali ya awamu ya tano itakuwa na nafasi nyingi za wachapakazi na waadilifu na kutokana na nia yao ya kutumikia watu, hawatakosa nafasi hizo.
"Licha ya jitihada za wakati huo, lakini mkampiga chini, ila namuombea msahama, mrudisheni wakati huu nifanye naye kazi, tunahitaji maendeleo bora kwa wote na hayo yataletwa na mafiga matatu kwa maana ya diwani, mbunge na rais," alisema.

Dk. Magufuli alisema kufanya kosa siyo kosa bali kosa kurudia kosa.
Akiwa Jimbo la Sumbawanga Mjini ambalo mgombea wake ni Aeshi Hilary, pia aliwaomba wananchi wafute makosa na kuanza upya kwa kumpa kura za ushindi.

Akiwa Jimbo la Mpanda Mjini, alitoa ahadi ya kazi kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kipindi kilichopita kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Said Arfi, na kuangushwa kwenye kura za maoni za CCM, huku akisema alikokuwa alikuwa amekosea njia.

"Kazi zipo nyingi nitakuwa rais wa nchi hii, kazi zipo nyingi wala usiwe na shaka, sitakosa nafasi ya kukupa, najua uwezo wako katika kazi," alisistiza.

Akihutubia wananchi wa eneo la Nzokala, Lusaka na Laela, alisema katika mchakato wa kumsaka mgombea urais wa CCM walikiwa 38, lakini alichaguliwa kupeperusha bendera ya chama hicho lakini wamevunja makundi na kumuunga mkono.

Aliagiza wagombea hao kupeleka orodha ya wagombea wote wa kura za maoni kwenye majimbo yao kwangu ajili ya kuwapatia kazi baada ya kuingia Ikulu.

Aidha, alisema ahadi zote anagomba atatekeleza na kwamba kubwa kwake ni utekelezaji wa huduma za jamii kama ujenzi wa zahanati vijiji vyote, vituo vya
afya afya kwenye kata, hospitali wilayani na hospitali za rufaa mikoani na kuhakikisha dawa zinakuwapo na siyo maduka binafsi kuwa na dawa na maeneo ya umma kukosa dawa.

Alisema atahakikisha huduma ya umeme, majisafi na salama vinapatikana kwas kuwa kama aliweza katika ujenzi wa barabara, hivyo mengine hatashindwa.

Nachowakumbusha CCM mshaurini Dkt JPM juu ya ahadi hizo vinginevyo naona kama atasahau.
 
Huyu mzee tumempigania sanaa ila ametugeuka, anawapa mkate wetu wapinzani wetu, kwa matusi na udhalilishaji niliofanyiwa leo hapa sirudi tena Lumumba , sirudi hata kufanya kazi ya chama mitandaoni. Nina vyeti vyagu halali, lakini bado sionekani ninachofanya, nafasi nzuri kama hizi wanapewa wapinzani wetu. Nasema hivii.....Acha niangalie utaratibu wangu mwingine wa Maisha.
 
Back
Top Bottom