Tujifunze kidogo kuhusu ndege (airplane)

Tujifunze kidogo kuhusu ndege (airplane)

Mkuu, inawezekana kujua VOR radial uliyopo (assume unaenda "delta victor") bila kutumia VOR display?
 
Je ni kweli ndege utengenezwa kwa kuungwA ungwa kama inavosemekana
Je ndege iwapo angan ikatokea ndege(kiumbe) kikajigonga ubavuni ama sehemu yyt inaweza pata ajari
 
Elimu nzuri, nina maswali mawili matatu!! Hivi zile horse au mapanga kazi yake kubwa nn? Na kwa nn ndege hua ikishapaa inaingiza ndani zile tairi!! Na swali jingine inasemekana kua ndege safari zake hua inaongozwa na mawasiliano!! Je ikitokea imepoteza mawasiliano angani rubani anaweza kutua mkiwa salama??
Mkuu sijaelewa vizuri kuhusu horse zipi au mapanga unayozungumzia. Lakini unamaanisha propeller; propeller huifanya ndege injongee mbele kwa aina za ndege zinazotumia propeller. Kuhusu matairi kuingizwa ndani, hii ni kwa sababu ya kupunguza sehemu za ndege ambazo zitakinzani na upepo hivyo kusababi kani inayoitwa "DRAG". Drag ni kani inayoivuta ndege nyuma kutokana na msuguano wa molecule za hewa dhidi ya surface structure ya ndege. Kuhusu ndege kupoteza mawasiliano na rubani kutua inategemea na rubani kulifahamu vizuri eneo hilo. Rubani mzuri anaweza kutua japo si rahisi sana ndege kupoteza kabisa mawasiliano kwa sababu vifaa vingi vina mbadala wake.
 
Mkuu, inawezekana kujua VOR radial uliyopo (assume unaenda "delta victor") bila kutumia VOR display?
Sasa mkuu utajua je bila VOR display? Kumbuka VOR, DME Localizer na ADF ni vifaa vinavyomsaidia rubani kutua.
 
Je ni kweli ndege utengenezwa kwa kuungwA ungwa kama inavosemekana
Je ndege iwapo angan ikatokea ndege(kiumbe) kikajigonga ubavuni ama sehemu yyt inaweza pata ajari
Mkuu sijaelewa unamaanisha kuungwa ungwa vipi! Kama unamaana ya kuunganishwa sehemu zake, ni kweli. Haitokei tu yote kwa mara moja ikiwa ni complete.
 
Mi nitagusia kwenye ndege aina za ANTONOV, tofauti na ndege zingine zinaendeshwa na marubani wawili mpaka za Cargo, lkn ANTONOV zinaendeshwa na wengi watu kama 7 hivi au 8, kwanini ANTONOV uendeshaji wake ni wa watu wengi na upo manually zaidi?
 
Yawezekana mkuu. Mimi tukio ambalo najua linaweza kufanya mafuta ya mwagwe ni ambapo ndege imesharuka ikiwa angani ikapata hitilafu na kutakiwa kutua tena. Hapo rubani lazima amwage mafuta kupunguza uzito.
Inaitwa Belly landing kama sikosei.
 
Shukrani Mkuu ....nimewahi kuambiwa pia ukipanda ndege ndogo inausumbufu na mtikisiko sana kuliko ndege kubwa hivyo kupelekea vichefuchefu na kutapika ..Mkuu kuna ukweli wowote ?( nimepitia karibu uzi wote kama nimerudia nisamehe)
kweli kabisa nina ushahidi mara nyingine unatua ukiwa na homa kabisaa.
 
Mi nitagusia kwenye ndege aina za ANTONOV, tofauti na ndege zingine zinaendeshwa na marubani wawili mpaka za Cargo, lkn ANTONOV zinaendeshwa na wengi watu kama 7 hivi au 8, kwanini ANTONOV uendeshaji wake ni wa watu wengi na upo manually zaidi?
Hili mkuu ngoja nilifanyie kazi, sina uzoefu na Antonov kama kweli ina crew wengi kiasi hicho.
 
Mkuu unaweza nipa somo hapo kwenye kasi zaidi ya sauti? pia engines za hizi ndege mbona ñi ndogo kuliko za Boeing au Airbus?
Engine za ndege vita ni turbojet engine; yaan thrust yake inatokana na kuzitoa exhaust gases kwa speed kubwa lakini ingini za Boeing na Airbus ni Turbofan; thrust inatokana na fan kubwa iliyopo mbele ya injini na kiasi kingine cha thrust kinatokana hot exhaust gases. Utofauti katika ukubwa ni kutokana component zilizopo kwenye engine.
 
Mkuu niliona makala moja YouTube kwamba helicopter kubwa na yenye nguvu kuliko zote duniani iliundwa na umoja wa nchi za USSR wakati huo. Nilishangaa kuona ikinyanyua ndege kubwa mithili ya bomdadier Q400 hivi mkuu hii kitu ni kweli, yani hii helicopter ipo mpaka saizi??
Bila kukudanganya sina ufahamu na hicho kitu mkuu
 
mkufunzi hii elimu unayotoa hapa ni kubwa mno kiasi kwamba kila anaechangi anapenda kujua na siyo kujua tu wengine wana ndoto zakuwa rubani na uhandisi ama wanapenda watoto wao siku moja awe rubani na mhandisi lakini pia hii ni taaluma ya sayansi ambayo unatakiwa kama una ndoto yakuwa rubani lazima uwe umesoma masomo ya sayansi yatakayokupeleka kwenye taaluma hii ya urubani na uhandisi , sasa ni vigezo au nimwaandaeje mtoto au mm mwenyewe kuwa na sifa ya kujifunza urubani na uhandisi? zaidi ya chuo cha NIT hakuna vyuo vingine bora zaidi ndani au nnje ya nchi kwenda kusoma? nawasilisha kwako mkufunzi najua nitapa majibu mazuri toka kwako.
 
Asante sana ndugu.

Kukipenda kitu ni hatua ya kwanza ya kwenda mbele hata kama hicho ulichokipenda kinachangamoto zake.
Mambo haya ya elimu ya ndege hasa kwa urubani na uhandisi yanachangamoto katika kumudu gharama zake. Gharama zake ni kubwa sana.

Fani ya urubani inagawanyika katika leseni zifuatazo;
1: Private Pilot Licence (PPL); hii ni leseni ya chini katika urubani. Ili upate leseni hii lazima uwe na masaa ya kuwa angani 40 (flying hours). Leseni hii inakuruhusu kuongoza ndege ambayo si abiria. Yaani ni wewe na familia yako na jamaa zako ndani ya ndege. Kwa hapa Tanzania, pale airport kuna mzungu anafundisha leseni hii kwa mli. 35 Tsh. Nilisikia NIT walitaka kuanzisha course ya urubani sijui waliishia wapi.

2:Commrcial Pilot Licence (CPL); Hii ni leseni inayokuruhusu kuongoza ndege za kukodiwa lakini si abiri. Lakini pia ukiwa na leseni unaweza kuajiliwa kwenye kampuni ya ndege kama Co-pilot wakati ukifukuzia masaa. Chuo cha Soroti flying school kinatoa mafunzo ya leseni hii kwa 62_000 USD. Hii leseni ni lazima uwe na masaa ya angani 200. Kwa mfano yule mzungu pale airport JNIA anatoza saa moja 200 USD.

3: Airline Transport Pilot Licence (ATPL); Hii ndo leseni inayokuruhusu kuongoza ndege za abiria. Na ili upate leseni lazima uwe na masaa yasiyopungua 1000.Lakini uzuri wa leseni utafikisha hayo masaa ukiwa ni Co-pilot ilimradi upate sehemu ya kujishikisha. Ukishafikisha masaa 100 mwanga unaanza kuonekana.
Ili niwezekusoma hizo cozi natakiwa elimu yangu iwe ya kuanzia kidato cha ngapi na ufaulu gani? Au hata wa kidato cha nne anaweza kusomea?
 
Ili niwezekusoma hizo cozi natakiwa elimu yangu iwe ya kuanzia kidato cha ngapi na ufaulu gani? Au hata wa kidato cha nne anaweza kusomea?
Sorry mkuu ni siku nyingi sikuwa na access na Jamii forum, kuna kipindi ilikuwa inasumbua. Ili uweze kusoma uhandisi wa ndege ni kuanzia elimu ya kidato cha sita, mchepuo ulio na fizikia na hesabu. Lakini chuo kama Ethiopia Aviation Academy wao wanataka uende pale na degree yoyote ya uhandisi, halafu ndege unasoma miaka miwili tu unatoka na leseni ya FAA.
 
mkufunzi hii elimu unayotoa hapa ni kubwa mno kiasi kwamba kila anaechangi anapenda kujua na siyo kujua tu wengine wana ndoto zakuwa rubani na uhandisi ama wanapenda watoto wao siku moja awe rubani na mhandisi lakini pia hii ni taaluma ya sayansi ambayo unatakiwa kama una ndoto yakuwa rubani lazima uwe umesoma masomo ya sayansi yatakayokupeleka kwenye taaluma hii ya urubani na uhandisi , sasa ni vigezo au nimwaandaeje mtoto au mm mwenyewe kuwa na sifa ya kujifunza urubani na uhandisi? zaidi ya chuo cha NIT hakuna vyuo vingine bora zaidi ndani au nnje ya nchi kwenda kusoma? nawasilisha kwako mkufunzi najua nitapa majibu mazuri toka kwako.
Mkuu samahani sikuweza kujibu swali lako kwa wakati ni kwa sababu sikuwa na access na JF kwa muda mrefu kuna wakati ilikuwa inasumbua kulog in.

Ili mtu aweze kusoma uhandisi wa ndege ni muhimu kumaliza kidato cha sita katika michepuo ya sayansi iliyo na fizikia na hesabu. Kwa upande wa urubani ni vile vile lakini akiwa na Jiografia ni vizuri zaidi. Japo hata aliyemaliza vizuri kidato cha nne anaweza kusoma urubani ila akiwa amemaliza kidato cha sita hatasumbuka sana na masomo kama flight physics.
 
Sorry mkuu ni siku nyingi sikuwa na access na Jamii forum, kuna kipindi ilikuwa inasumbua. Ili uweze kusoma uhandisi wa ndege ni kuanzia elimu ya kidato cha sita, mchepuo ulio na fizikia na hesabu. Lakini chuo kama Ethiopia Aviation Academy wao wanataka uende pale na degree yoyote ya uhandisi, halafu ndege unasoma miaka miwili tu unatoka na leseni ya FAA.
hapo nimekuelewa mkuu ila endapo unahitaji kusoma uhandisi kipi chuo ambacho unaweza kwenda kusoma uhandisi na urubani kwa pamoja? maana Ethiopian aviation academy inatoa urubani tu ila sifa uwe na degree yoyote ya uhandisi
 
Ethiopia Avition Academy ni uhandisi wa ndege pekee. Chuo kinachotoa Urubani na Uhandisi ni Embry Riddle Aeronautical University (ERAU) kipo Marekani. Uhandisi ni kama dola elfu 90 na Urubani ni dola elfu 70, unatoka leseni ya CPL. Kwa upande wa Uhandisi unatoka na leseni FAA ya Airframe and Power plant.
 
Back
Top Bottom