Tujifunze kidogo kuhusu ndege (airplane)

Tujifunze kidogo kuhusu ndege (airplane)

kuna mandege ya jeshi naona huwa yanaruka kwenye distance fupi na wakati wa kutua yanazuiliwa kwa kamba nyuma juu ya mkia wa ndege (ulisema huna expirience lakini naomba hata adea tu Mkuu) then zinasimama
 
mkuu vipi kuhusu yale maji taka ya toilet hua inakuaje juu ya umwagaji wake?
 
naona watu wengi wamestic kwenye technical issues...naomba niulize kiabiria zaidi....(sijawahi kupanda ndege) je endapo ndege itapata hitilafu angani tofauti na kufunga mkanda hamna option yoyote ya kujiokoa either kwa parachuti ni kusubiri tu mpaka ianguke?
Ndege za abiria hazina parachute mkuu. Ukipanda ndege wahudumu wa ndege huwapa maelezo ya vifaa vilivyopo kwa ajili ya kujiokolea.

Sent from my itel it1508 using JamiiForums mobile app
 
Ndege za abiria hazina parachute mkuu. Ukipanda ndege wahudumu wa ndege huwapa maelezo ya vifaa vilivyopo kwa ajili ya kujiokolea.

Sent from my itel it1508 using JamiiForums mobile app
Shukrani Mkuu ....nimewahi kuambiwa pia ukipanda ndege ndogo inausumbufu na mtikisiko sana kuliko ndege kubwa hivyo kupelekea vichefuchefu na kutapika ..Mkuu kuna ukweli wowote ?( nimepitia karibu uzi wote kama nimerudia nisamehe)
 
Kuyamwagia wapi kwa maana ipi mkuu sijakuelewa.

Sent from my itel it1508 using JamiiForums mobile app
Anazungumzia suala la rubani kumwaga mafuta ya ndege ili arudi uwanjani kutua kama amepata hitilafu.

Mimi nadhani atatafuta eneo lisilo la makazi (pori, etc) ndio afungulie mataki amwage kiasi cha mafuta ili abakize Kiasi ambacho hakimzuii kutua kwa usalama
 
Yaani yanamwagika huku chini au??
Mkuu hiki kitu kipo; ndege ina maximum take off weight na maximum structural landing weight. Ambapo siku zote hii max landing weight huwa ndogo kuliko max take off weight kwa sababu ya fuel consumption. Sasa ikitokea emergence arudi alipotoka na mafuta hayajatumika kwa kiasi cha kupunguza uzito, ni lazima afanye kitu kinaitwa fuel dumping ili kumpunguza uzito. Hivyo rubani ataona ni maeneo gani anaweza kufanyia hiyo fuel dumping.

Ahaa nmekuelewa mkuu.....maana nlikua nawaza hapa kwamba ipo siku tutamwagikiwa mafuta kutoka juu!!
 
Shukrani Mkuu ....nimewahi kuambiwa pia ukipanda ndege ndogo inausumbufu na mtikisiko sana kuliko ndege kubwa hivyo kupelekea vichefuchefu na kutapika ..Mkuu kuna ukweli wowote ?( nimepitia karibu uzi wote kama nimerudia nisamehe)
Ni kutokana na ndege ndogo kutikiswa sana. Ni kama boti ndogo baharini dhidi ya mawimbi.

Sent from my itel it1508 using JamiiForums mobile app
 
kuna mandege ya jeshi naona huwa yanaruka kwenye distance fupi na wakati wa kutua yanazuiliwa kwa kamba nyuma juu ya mkia wa ndege (ulisema huna expirience lakini naomba hata adea tu Mkuu) then zinasimama
Apa utakua unazungumzia zile ndege zinazoruka na kutua kwenye meli za kivita(Aircraft carrier). Ni hivi ndege zinahitaji umbali mrefu wa runway kwa ajili ya kufikia ile speed itayoiwezesha kuruka around 1 hadi 3km, lakini hizi meli za kivita haziwezi kutengenezwa zikawa na urefu huoo. Meli kubwa za kivita nyingi kwa urefu hua ni chini ya 400 Metre, hivyo basi ili ndege ya kivita iweze kuruka inapewa msaada na kifaa kimoja kinaitwa Catapult. Hichi kifaa kinafanya kazi ya kuifyatua ndege kama vile manati inavyofyatua jiwe. Kwenye tyre la mbele la ndege ya kivita wakati wa kuruka linaunganishwa na ile catapult. Hii Catapult inafanya kazi kwa kutumia pressure kubwa ya upepo pamoja na mvuke(steam). Kabla ya kuruka Catapult operator anacheki uzito wa ndege ili ajua ataweka pressure ya kiwango gani kwenye ile Catapult ili ndege iweze kufikia ile speed yake ya kuruka katika ule umbali mfupi ambao hua ni less than 100Metre. Baada ya kupima uzito anaset presure, then ana anaruhusu ule mvuke na upepo ukiwa kwenye pressure ya juu ile aliyoweka kwenda kusukuma piston mbili zilizopo kwenye airtight tube na ambazo zimeunganishwa na ile Catapult. Kwa kuwa ile pressure ya air+steam iko juu sana bac ndege inafyatuka na kufikia take-off speed yake ndani ya umbali mfupi na hatimae kuruka. Mfano kwenye aircraft carrier kama Nimitz class ya U.S Catapult inanguvu na uwezo wa kuifyatua na kurusha Landrover kwa umbali wa KM 1. Wakati wa kutua pia ndege inadakwa na kamba ambayo kwa ndani ya meli ile kamba imeunganishwa na system ya piston pamoja na oil cylinder, kwa hiyo rubani akija kutua anatakiwa engine iwe kwenye full power ili ikitokea ile hook ya kwenye mkia wa ndege imeikosa ile kamba pale kwenye meli basi hapo hapo rubani anaruka na kuzunguka ili atue tena. Mara tu ndege inapotua na kuikamata ile kamba,ile kamba inasukuma zile piston na zenyewe zinakuwa zina icompress ile oil kwenye cylinder kwa ajili ya kupotesha ile nguvu ya mwendo wa ndege na hatimae ndege inasimama.
images+%283%29.jpeg
Catapult
images+%284%29.jpeg
ndege ikiwa imeunganishwa na catapult
 
mkuu vipi kuhusu yale maji taka ya toilet hua inakuaje juu ya umwagaji wake?
Yale maji taka hua ndege ikifika airport kuna gari linakuja kuyafyonza yote kutoka kwenye matank yaliko hifadhiwa ndani ya ndege na kwenda kuyamwaga sehemu salama. Hii huduma inaitwa Toilet Service
images+%285%29.jpeg
gari ya kufyoza uchafu kutoka kwenye matank ya uchafu ndani ya ndege.
 
Mkuu mimi nilikuuliza kuhusu namna ambavyo unjini zinavyofanya kazi kwenye high altitude kusipokua na oxgyjen
 
Swali lingine ni kua je ndege inaweza kuelea angani kutokana na kua mbali na gravitation force na kupelekea kutumia mafuta kidogo mkuu..assante..
 
Mkuu mimi nilikuuliza kuhusu namna ambavyo unjini zinavyofanya kazi kwenye high altitude kusipokua na oxgyjen
Mkuu kama sijasahau swali lako hili nilishalijibu. Lakini siyo mbaya nikijibu tena. Ndege hizi za kawaida hazivuki tabaka la hewa (atmosphere). Ingawa ukweli ni kwamba unene wa hewa (air density) hupungua kadri unavyozidi kwenda juu zaidi bado Oxygen huweza kupatikana japo kwa kiwango kidogo. Kuna mfumo katika injini ambao unahusika na kuhakikisha uwiano wa mafuta na hewa upo katika kiwango kinachotakiwa.
 
Back
Top Bottom