Shukrani za dhati kwenu.
Mkuu
Shebbydo umenifurahisha sana uliposem kuwa uliona tunaanza kuchangayikiwa ulipoingia kwenye details za avionics pale kwenye VOR. Ni kweli kabisa, mimi nilikuwa najifunza kidogo kuhusu airplanes kwa kupitia MS Flight Simulator 9 na kulikuwa na training programmes mle. Nilikwamia kwenye navigation kwa kutumia VOR maana ile mistari miwili inavyomove kwenye ile instrument nilishindwa kabisa kuielewa.
Nitarudi tena kwenye ile post ili nipate kufahamu kwa uhakika namna VOR zinavyofanya kazi.
Swali langu la kwanza ni hili:
Mawasiliano kati ya controller na rubani yanatumia radio waves hizi za kawaida kama radio call? Transmission range yake ni kiasi gani?
Je, mimi kama mwananchi wa kawaida ninaweza kununua (au kutngeneza for the hardcore nerds) transmitter/receiver yenye uwezo wa kusikiliza transmissions hizi provided I know the frequency of the tower/control center? Na je, hili linaruhusiwa na sheria?
Vipi nikiamua na mimi nikawa natransmit. Na key-in naongea na control tower au pilot. I won't be stupid kuuliza kama naweza nikaimpersonate pilot au controller ilhali mhusika yuko kwenye same frequency, atanisikia na kusema kuwa si yeye aliyetuma transmission hiyo.
Lakini, core ya swali langu ni je,as a civillian, can I get my hands on radios zinazoweza kunipa transmissions hizi au hizo transmissions zinatumia technology ambayo haipatikani kwa mwananchi wa kawaida.