Tujifunze kidogo kuhusu ndege (airplane)

Tujifunze kidogo kuhusu ndege (airplane)

swal jingine kwann ndege zinaruka juu sana kwanini zisiruke chini chini ili iwe rahisi hata zikipta hitilafu kutua
 
Ndugu Shebbydo, engine ya gari inazungusha matairi ili yakimbie kwenye barabara lakini ndege haitumii matairi angani. Hebu naomba utujuze japo kidogo ni kwa jinsi gani engine ya TURBO PROP (nadhani ni kifupi cha propeller) na TURBO FAN za madege makubwa ya Boeing, airbus na Tupolev zinavyoiwezesha ndege kukimbia ardhini na angani wakati engine inajiungurumia yenyewe huko chini ya mabawa bila kuunganishwa na matairi. Natanguliza shukrani mkuu.
Asante mkuu kwa swali lako.

Kwa ujumla gas turbine engine yoyote bila kujali ni turboprop, turbofan, turbojet ama turboshaft zina sehemu tano ukiachilia mbali sehumu ya accesories na mifumo mingine inayohitajika kwenye ndege. Sehemu hizo ni: Air Intake section, Compressor section, Combustion section, Turbine section na Exhaust section.

AIR INTAKE SECTION; Hii ni sehemu inayohusika na kuingiza hewa kwenye injini.
COMPRESSOR SECTION; Hii ni section inayohusika na kuifanya hewa iliyoingizwa kuwa mgandamizo mkubwa (High pressure).
COMBUSTION SECTION; Hewa kutoka kwenye compressor section iliyo na mgandamizo mkubwa, huingia hapa. Hukutana na moto (flame) ambao unatokana kuchwa kwa mchanganyiko wa mafuta na hewa. Hewa iliyoingia hapa hupunguzwa spidi ili isiuzime moto huo. Hewa hiyo kutokana na kupokea joto basi huwa ni "hot gas" ambayo huingia TURBINE SECTION na kuizungusha GAS TURBINE.
EXHAUST SECTION; Gas hiyo ya moto huingia sehemu hii na kuongezwa spidi ili itolewe kwa spidi kubwa kwa ajili ya kuchangia nguvu ya kuisukuma ndege kwenda mbele.

TURBOJET engine yenyewe huzalisha nguvu ya kuisukuma ndege (Kani mjongeo-Thrust Force) kwa hiyo hot gas inayotolewa kwenye exhaust kwa kasi. Ndiyo maana ndege zenye injini hizi husifika kwa kula mafuta na makelele mengi. Ndege nyingi za kibiashara sasa hivi hazitumii injini hizi.

Nikirejea katika TURBINE SECTION, aina ya mfumo wa injini unaitwa kutokana Gas Turbine inaendesha nini baada ya kuzungushwa na hot gases.
TURBOPROP; Gas turbine kupitia shaft (shaft ni chuma ambacho kinaunganishwa ili kuzungusha kitu kingine) iliyounganishwa na Propeller, huizungusha propeller. Propeller husukuma hewa nyuma hivyo kusababisha ndege kwenda mbele ikishirikiana na ile hot gas inayotolewa kwenye exhaust kwa kasi.
TURBOFAN; Gas turbine huzungusha Fan kubwa iliyopo mbele ambayo nayo huvuta hewa na kuisukuma nyuma. Hivyo ndege hujongea mbele. (To every action, there is equal and opposite reaction- Newton's third law).

Nafikiri nitakuwa nimekujibu mkuu. Karibu sana.
 
mkuu hiyo artificial horizon ina umuhimu gani swal la pili je ndege inaweza operate kwa injin mojaikitokea nyingine imefeli
Mkuu hebu hata wewe fikiria tungekuwa hatuioni horizon, si tungehisi tunaenda kuporomoka? Ni kumuonesha tu yupo kiasi gani juu kutoka ardhini. Kuhusu injini moja kusaidia endapo nyingine itapata hitilafu, jibu ni ndiyo. Kuna watu wengine wana BIMA ambazo haziwaruhusu kupanda ndege yenye injini moja. Akipata ajali kwenye ndege yenye injini moja BIMA hawamlipi.
 
nazo ni za abiria ama za kitafiti?
Kuna za abiria na mizigo. Pia wakati mwingine unaweza kuona ni aina fulani za rocket zinatumika katika tafiti. Zinaitwa Sound rocket.
Unajua kinachoonekana ni moshi siyo moshi in reality. Ndege yoyote ambayo inatoa hot exhaust gases, kitu hicho kitaonekana. Nitajaribu kuweka picha tatu za rocket, Airbus 320 na Boeing 747 (Jumbo Jet au Queen of the sky) muone.
Kinachoonekana kama moshi ni matokeo ya exhaust hot gases ku-condense kutokana na baridi kali katika umbali huo. Hivyo baada ya ku-condense huganda.(Condensing ni hali ya mvuke kupozwa na kuwa kimiminika). Hiyo unayoita moshi inaitwa condensing trails kwa kifupi huitwa contrails.
 
Hii ni Boeing 747(Jumbo Jet)
IMG_20180122_182951.jpg
 
asante sana mkuu naomba niendelee na maswali
je speed ya ardhini na angani zinakua sawa ama kuna speed ya kutembelea ardhini(kipindi inapaa) na kuna speed kutembea angani

swali la pili
Ile taa ya mbele ina uwezo wa kumulika mbele kwa umbali gani

swali la tatu
ikitokea ndege imepata hitilafu ikadondokea baharini lakini haijaharibika wala kupata uwazi wowote je itazama au itaelea na je maji yanaweza kuingia ndani

swali la nne tunaaminishwa huku mtaani kwamba kuna gari zinazoweza kukimbia sambamba na ndege (on the runway) je hili ni kweli ,tusaidie pia na speed ya ndege ya juu kabisa

ASANTE
 
Asante mkuu

Kuhusu speed, speed ni tofauti. Ground speed(speed ya ardhini) ni ndogo kuliko ya angani. Speed ya angani nayo imetofautiana. Kuna; CLIMBING SPEED; Spidi wakati wa kupanda
CRUISING SPEED; Spidi wakati ipo level flight, kwenye level ambayo unaweza kuinuka ukaenda maliwatoni na
APPROACHING SPEED; Speed ambayo rubani anaanza kushuka kwa ajili ya kutua.

Kuhusu ile taa ya mbele kumulika umbali gani, kwa kweli sina takwimu halisi

Kuhusu ndege kuelea ndani ya maji, si kwamba itaelea muda mrefu itakuwa inazama taratibu. Ndiyo maana ni bora kuliweka majini kuliko kulidondosha nchi kavu. Maji kupenya, ndiyo yatapenya japo si kwa kasi kubwa. Na kuhusu magari kuwa na spidi sawa na ya ndege ardhini si kweli. Yale magari ya zima moto huifata ndege lakini hayawezi kupimana ubavu hata kidogo.
 
Swali langu ni fupi; ni nini tofauti ya Pilot, Captain, First Officer na wale Cabin Crews? La pili, kwanini ndege kubwa kama A380 wakati wa kupanda na kushuka ziko comfortable zaidi kuliko ATR za Precision?
 
Lingine za ziada, ukitazama ramani kwa haraka haraka, common sense inakuonyesha kuwa ili uende Bara la Marekani mfano kutokea DUbai, ni heri ungechanja mbuga, upasue Afrika (Misri, Sudan, Jangwa la Sahara nk) kisha uingie zako baharini mpaka unafika kwa wakubwa huko. Swali, kwanini mfano kutokea Dubai kwenda US, jamaa wanachanja, Europe karibu yote, mpaka kule North Pole halafu wanakuja kudondokea usawa wa kutoka Canada. Natanguliza shukrani za awali Mkuu.
 
Mkuu karibu sana
Tofauti ya Pilot, Captain, First Officer na Cabin Crew ni majukumu yao.

Nianze na Pilot, Captain na First Officer. Captain na First officer wote ni Mapilot ila tofauti iliyopo hapo mmoja ni Mwalimu mkuu mwingine ni mwalimu wa kawaida. Kwa maana kwamba. Captain ndiye Pilot In Command (PIC), yeye ndiye anatoa maamuzi yote na ndiye mkuu wa msafara. Hukaa kiti cha kushoto. First Officer ni Co-pilot(rubani mwenza). Kwa ndege ambazo zinatembea na Flight Engineer, yeye ni second officer. Lakini ndege za sasa haziitaji flight engineer hivyo it's a dying professional.

Cabin crew ni wahudumu wa ndani ya ndege.
Kuhusu utofauti wa kutikiswa kwa ndege kubwa na ndogo ni kama vile meli tu bahari dhidi ya mawimbi, kubwa nafuu kuliko ndogo. Baharii mitikisiko kutokana na maji, angani ni upepo( hewa inayotembea) na ukizingatia ndege kupanda angani hukinzana na upepo( hupaa kuelekea upepo unakotoka)
 
Jibu mujarabu kabisa, asante Mkubwa.
 
Lingine za ziada, ukitazama ramani kwa haraka haraka, common sense inakuonyesha kuwa ili uende Bara la Marekani mfano kutokea DUbai, ni heri ungechanja mbuga, upasue Afrika (Misri, Sudan, Jangwa la Sahara nk) kisha uingie zako baharini mpaka unafika kwa wakubwa huko. Swali, kwanini mfano kutokea Dubai kwenda US, jamaa wanachanja, Europe karibu yote, mpaka kule North Pole halafu wanakuja kudondokea usawa wa kutoka Canada. Natanguliza shukrani za awali Mkuu.
Kuhusu kukwepa kupitia huko nakokusema ni kukwepa sehemu fulani ambayo mikondo yake ya upepo siyo mizuri kabisa. Hii ni Bermuda Triangle. Eneo hili linachukua pembetu kwa point hizi; Florida, Puetto Rico na Kisiwa cha Bermuda. Maeneo hayo hayana historia nzuri kwa vyombo vya angani na majini.
 
Kuna ile taa uwa Inawaka na kuzima unaweza eleza umaanisha nin uwa ni kama kimuli muli
 
Sheria hizi zikoje!
(1)Eti mtoto aliezaliwa akiwa angani kwenye ndege Uraia wake unakuaje?
(2)kwanini unadhani Baba yangu anaogopa kupanda ndege kubwa!
 
Back
Top Bottom