Tujenge kuta za kifikra

Tujenge kuta za kifikra

daima takwita mzee wa WISDOM, namna ulivyoliandaa hili bandiko, namna ya kuwasilisha, lugha uliyotumia na jinsi ulivyolifinyanga hadi kwa mlaji/msomaji imenionesha kuwa wewe n mtu mwenye uelewa mkubwa sana, hongera mkuu sizonje ajui haya. Wameunda vitengo vya kutafta watu wanaokosoa mhimil mkuu mtandaon, walau wangeunda ktengo maalum cha watu wachache wakuchukua mawazo njet na mazuri mtandaon kama haya tungepga hatua. JF IDUMU DAIMA. Long life kapten MSHANA
 
umeandika wewe? au umedesa? ha ha (natania)

kama umeandika wewe, lina heri tumbo lililokubeba na abarikiwe aliyekukuza

mabandiko kama haya yenye kulisha brain yamepotea sana na leo unaiweka hadhi ya JF mahali pake
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Watu wa ujerumani walijikuta kwenye mtanziko mkubwa wa kuhitilafiana mitazamo, wa magharibi wakawa na mitazamo inayokinzana na wa mashariki... Wakashindwa kabisa kupatana..... Na mwisho wakaja na wazo la kujenga ukuta wa kuwatenganisha.... Ukuta ule haupo tena, ulikuja kubomolewa baada ya miaka mingi kupita lakini ni baada ya kujitambua kwamba ukuta wa mawe hauwezi kuondoa tofauti zao bali ukuta wa kifikra ukuta wa kimtazamo... Walivunja kuta hizi kwanza kabla ya kuvunja ukuta ule unaoonekana
Waisrael wanajenga ukuta kuzunguka ukanda wa Gaza kujikinga na Wapelistina... Hii ni dhana iliyojengeka mioyoni mwao.... Kuna siku ule ukuta utavunjwa....
Trump anataka kujenga ukuta mpakani na Mexico ni dhana iliyo mawazoni mwake anataka kuifanya halisi... Atajenga sasa lakini kuna siku itafika utabomolewa
Ukuta ni kitu kisicho na uhai.. Ukuta ni kitu kinatokana na dhana... Dhana huzaliwa hukua hubadilika na hata kufa pia
Ni wazo jema kabisa kujenga ukuta kuzunguka machimbo ya TANZANITE kule mererani... Ni kuonyesha jinsi tulivyoguswa na wizi wa madini yetu adimu, lakini Mererani ni sehemu ndogo tu ya tatizo kubwa halafu sugu... Tutajenga kuta ngapi Tanzania nzima ?
Ukuta bila UZALENDO ni kazi bure hujuma zitaendelea bila kukoma, rushwa itatamalaki.... Ukuta kuzunguka Mererani sio suluhisho.. Watu watafanya mtobozano.. Zitachimbwa njia chini ya ardhi na biashara itafanyika kama kawa binadamu halindiki... Baki na ukuta wako na makamera yako wanaume wanapiga kazi chini ya ardhi kwa raha zao... Chini ya ukanda wa Gaza kuna njia mamia zimetobolewa kuingia Israeli
Ukuta wa mawe hapana, tujenge ukuta wa fikra za kizalendo, huu ni ukuta imara zaidi na usio na gharama kubwa, ni ukuta usio na mtobazano.... Ukuta huu si kwenye madini tu bali kwenye kila tunu na rasilimali za taifa letu tukuka

Twendeni tukajenge sasa.....

#UKUTA#
hivi madini hayo yapo hapo tu? ina maana simanjiro nzima madini yatakuwa yamejirundika katika eneo litakalojengwa ukuta?
 
Mshana jr ktk ubora wake.
Hautahitaji kuta ktk Zama hizi, tunahitaji kujenga madaraja ya kuunganisha upendo, Utu, uzalendo nk ambavyo kwavyo vitasaidia kuthaminiana na kila mmoja kumuona mwingine kuwa ana thamani sawa na yeye.
Tukijenga madaraja hayo ya kuunganisha vitu hivyo, jamii itaishi Kwa amani Na itastawi.
Umenena vyema sana, kama tanzanite inaibwa kwaninj hatuujengi kuta kuzunguka migodi ambayo tumekuwa tukipigwa pengine zaidi ya huko mererani?
Tutajenga kuta ngapi ktk nchi hii, kwani kulingana Na mkulu kila sekta kuna madudu huko pia tujenge kuta?
Tujenge madaraja ambayo pia yatatuweka karibu kwani kuta zinatenga. Tukiwa karibu, tutapata fursa ya kusikia mawazo mbadala ambayo yamekuwa yakitolewa kila kukicha kuwa tunahitaji kujenga MIFUMO imara badala ya kuta.
Hongera mshana Kwa chakula vizuri cha ubongo.
 
Watu wa ujerumani walijikuta kwenye mtanziko mkubwa wa kuhitilafiana mitazamo, wa magharibi wakawa na mitazamo inayokinzana na wa mashariki... Wakashindwa kabisa kupatana..... Na mwisho wakaja na wazo la kujenga ukuta wa kuwatenganisha.... Ukuta ule haupo tena, ulikuja kubomolewa baada ya miaka mingi kupita lakini ni baada ya kujitambua kwamba ukuta wa mawe hauwezi kuondoa tofauti zao bali ukuta wa kifikra ukuta wa kimtazamo... Walivunja kuta hizi kwanza kabla ya kuvunja ukuta ule unaoonekana
Waisrael wanajenga ukuta kuzunguka ukanda wa Gaza kujikinga na Wapelistina... Hii ni dhana iliyojengeka mioyoni mwao.... Kuna siku ule ukuta utavunjwa....
Trump anataka kujenga ukuta mpakani na Mexico ni dhana iliyo mawazoni mwake anataka kuifanya halisi... Atajenga sasa lakini kuna siku itafika utabomolewa
Ukuta ni kitu kisicho na uhai.. Ukuta ni kitu kinatokana na dhana... Dhana huzaliwa hukua hubadilika na hata kufa pia
Ni wazo jema kabisa kujenga ukuta kuzunguka machimbo ya TANZANITE kule mererani... Ni kuonyesha jinsi tulivyoguswa na wizi wa madini yetu adimu, lakini Mererani ni sehemu ndogo tu ya tatizo kubwa halafu sugu... Tutajenga kuta ngapi Tanzania nzima ?
Ukuta bila UZALENDO ni kazi bure hujuma zitaendelea bila kukoma, rushwa itatamalaki.... Ukuta kuzunguka Mererani sio suluhisho.. Watu watafanya mtobozano.. Zitachimbwa njia chini ya ardhi na biashara itafanyika kama kawa binadamu halindiki... Baki na ukuta wako na makamera yako wanaume wanapiga kazi chini ya ardhi kwa raha zao... Chini ya ukanda wa Gaza kuna njia mamia zimetobolewa kuingia Israeli
Ukuta wa mawe hapana, tujenge ukuta wa fikra za kizalendo, huu ni ukuta imara zaidi na usio na gharama kubwa, ni ukuta usio na mtobazano.... Ukuta huu si kwenye madini tu bali kwenye kila tunu na rasilimali za taifa letu tukuka

Twendeni tukajenge sasa.....

#UKUTA#

Ushauri mzuri sana, tatizo ni dhana walioijenga kwenye nafsi na akili zao kuwa ukuta ndio utatatua matatizo yote bila ya kuahughulikia matatizo yenyewe.
 
Umeyawakilisha vizuri mawazo yangu, umeongea vizuri sana na sina cha kuongezea ili nisiharibu mawazo mujaarabu.

Historia itatuhukumu ni suala la muda tu.
 
Mkuu nimekusoma,umenipa kitu...
Ukuta wa kifikra.

Watanzania huwa hawashindwi kuiba,hakuna kitu kikaanza na security watanzania wakashindwa kuishinda hyo security.

Njia ni kuhimiza uzalendo,anatangaza kujenga ukuta wezi wako wanatabasamu wakijipanga kwa njia mpya.
 
Watu wa ujerumani walijikuta kwenye mtanziko mkubwa wa kuhitilafiana mitazamo, wa magharibi wakawa na mitazamo inayokinzana na wa mashariki... Wakashindwa kabisa kupatana..... Na mwisho wakaja na wazo la kujenga ukuta wa kuwatenganisha.... Ukuta ule haupo tena, ulikuja kubomolewa baada ya miaka mingi kupita lakini ni baada ya kujitambua kwamba ukuta wa mawe hauwezi kuondoa tofauti zao bali ukuta wa kifikra ukuta wa kimtazamo... Walivunja kuta hizi kwanza kabla ya kuvunja ukuta ule unaoonekana
Waisrael wanajenga ukuta kuzunguka ukanda wa Gaza kujikinga na Wapelistina... Hii ni dhana iliyojengeka mioyoni mwao.... Kuna siku ule ukuta utavunjwa....
Trump anataka kujenga ukuta mpakani na Mexico ni dhana iliyo mawazoni mwake anataka kuifanya halisi... Atajenga sasa lakini kuna siku itafika utabomolewa
Ukuta ni kitu kisicho na uhai.. Ukuta ni kitu kinatokana na dhana... Dhana huzaliwa hukua hubadilika na hata kufa pia
Ni wazo jema kabisa kujenga ukuta kuzunguka machimbo ya TANZANITE kule mererani... Ni kuonyesha jinsi tulivyoguswa na wizi wa madini yetu adimu, lakini Mererani ni sehemu ndogo tu ya tatizo kubwa halafu sugu... Tutajenga kuta ngapi Tanzania nzima ?
Ukuta bila UZALENDO ni kazi bure hujuma zitaendelea bila kukoma, rushwa itatamalaki.... Ukuta kuzunguka Mererani sio suluhisho.. Watu watafanya mtobozano.. Zitachimbwa njia chini ya ardhi na biashara itafanyika kama kawa binadamu halindiki... Baki na ukuta wako na makamera yako wanaume wanapiga kazi chini ya ardhi kwa raha zao... Chini ya ukanda wa Gaza kuna njia mamia zimetobolewa kuingia Israeli
Ukuta wa mawe hapana, tujenge ukuta wa fikra za kizalendo, huu ni ukuta imara zaidi na usio na gharama kubwa, ni ukuta usio na mtobazano.... Ukuta huu si kwenye madini tu bali kwenye kila tunu na rasilimali za taifa letu tukuka

Twendeni tukajenge sasa.....

#UKUTA#
Yes...I was just thinking, ujenzi wa kuta ni miradi ya viongozi wajinga!
 
Mawazo mazuri ya kujenga, yenye mtazamo wa kifalsafa. Hizo ni hekima, nimechota kidogo ili kuimarisha fikra zangu. Hivi kwa nini watu wanatumia nguvu kupigana badala ya kushindana kwa hoja? Hoja ya kimtazamo ina nguvu kushinda nguvu ambazo hazina mtazamo. All the best
 
hivi madini hayo yapo hapo tu? ina maana simanjiro nzima madini yatakuwa yamejirundika katika eneo litakalojengwa ukuta?
Kule kijijini kwetu kuna madini aina zaidi ya 4. Ila yanachimbwa kienyeji. Nategemea ukuta na huko Siki ikiundwa tume. He tutajenga kuta ngapi. Amkeni watanzania sio kilakitu kipongeza, vakukosoa tukosoe. Na vyakusifia tukosoe japo kwa umakini sababu ya uongozi uliowekwa na Lubuva
 
Fikra ni kitu muhimu sana. Hata ile kamata kamata ya wabunge mfano zito na kubenea kupelekwa kwa ndege dodoma ni kukosa fikra. Kwa nini serikali iharibu mafuta na kodi za wananchi eti kumpeleka kubenea dodoma, nini faida yake? Je, akisha hojiwa, bunge au sisi wananchi tunabaki na faida gani? Fikra ni kitu muhimu sana, wala si kutumia nguvu wala kuweka miukuta.
Hongera mshana kuyakumbusha matanzania dhana hii.
 
Back
Top Bottom