Tujadili Umakini wa Walinzi wa JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujadili Umakini wa Walinzi wa JK

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ng'wanangwa, Nov 13, 2010.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa nikifuatilia na kuichunguza video inayoonesha JK akianguka pale viwanja vya Jangwani siku ya uzinduzi wa kampeni wa Chama Cha Mafisadi.

  Kabla ya kuanguka, JK alianza kwa kutamka maneno haya:

  "............tumetekeleza mengi, na tutafanya mengi zaidi..........seeee!! Baada ya hapo alijaribu kuongeza 'ahadi' nyingine, lakini akashindwa na kuporomoka.


  Hilo neno, "seeee!!" si la kawaida. Ni neno linalotamkwa na mtu anayehisi maumivu makali au anayehisi hali mbaya kimwili. Lakini walinzi wake walikuwepo wanakula pepo tu. Wanawaza ulaji badala ya kumlinda Mkulu. Wanawaza madem zao wakati hali ya mtu anayewaweka mjini ni mbaya.

  Upo wapi umakini wao? Bado wanamlinda au alishawatimua?

  Ndiyo sababu ninapoambiwa baadhi yao wameshiriki zoezi la kuchakachua kura za Watanzania sipati shaka kwa sababu hawako makini.

  Wanajamvi munasemaje??

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2010
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kwakweli huyu mzee anatia huruma. Hivi anamatatizo gani?
   
 3. Valid_Options

  Valid_Options Member

  #3
  Nov 13, 2010
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BAada ya kuulamba ukuu wa nchi na kishaunda serikali ataenda zake ughaibuni kula raha kurudisha mwili hivyo msihofu mkuu atarudi katika afya njema kabisa
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Shida utakuta nao wameajiriwa kiushkaji, sio professionals...Anajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe!
  Ila pale kwenye aiseeeeeeeeeee.!! panasikitisha sana, mkuu anaumwa huyu jamani!
   
 5. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Ukweli ni kwamba umakini ktk utendaji ndani serikali ya mkuu ni tatizo kubwa. Ukiacha swala la ulinzi wake binafsi kumbukeni swala la mganganyiko mkurugenzi kwenda ikulu kupokea gari ya wagonjwa wakati hawaintended subject.
   
 6. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Siyo seeeeeee ni aiseeeee ambalo ni neno la kawaida kwenye maongezi ya kiswahili, nadhani origin yake ni kiingereza " I say". Linapotumika kwenye kiswahili humaanisha kuwa mtumiaji anashangazaa kwa mfano akimkuta rafiki yake maeneo fulani fulani ambapo hukumtegemea atasema "aiseeee! kumbe na wewe huko hapa" au anastaajabu au aamini kilichotokea kwa mfano "aiseee kumbe ccm wamechakachua matokeo". Mtu anaweza kuushangaa mwili wake anapojisikia hauko sawa mafano "aiseee ninaumwa". Kutokana na matumizi mbalimbali ya neno aiseee, walinzi wa JK hataweza kumvaa kila anapotaja hilo neno, litakuwa ni scandal lingine tena. Kinachotakiwa hapa kwanza ni maelezo ya kidaktari kuhusu tatizo lake na walinzi wapewe mafundisho na madaktari jinsi ya kusoma dalili za tatizo hilo linapokaribia kutokea na pili ni kuchekiwa na daktari wake kabla ya kusimama majukwaani au kufanya shughuli nzito. Ameisha anguka mara kadhaa, hakuna data kuonyesha kuwa mara zote amekuwa akisema aiseee kabla ya kuanguka. Kwenye hii karne ya 21 watu hawafanyi vitu kwa hisia au kubahatisha bali kwa training (kufundishwa)
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Rejea context.

  Nini alisema kabla na baada ya kutamka "seeee!!". Kabla hajatamka hilo neno aliongea maneno ya kawaida tu ambayo mtu huwezi kutarajia kuwa yatafuatiwa na neno la mshangao. Hata baada ya kulitamka hilo neno alizungumza vitu vya kawaida tu visivyoashiria kuona, kusikia kitu chochote kisicho cha kawaida (kwa macho na masikio) kiasi cha walinzi wake kupuuzia. Kwa hiyo kama maana ya hilo neno ni mshangao walipaswa japo kutupa jicho na kujiuliza 'mkuu kaashiria kushangaa kitu mbona hakuna jambo lolote la kushangaza mahali hapa'?

  Kumbuka hawa walinzi wa Mkulu walishawahi kumuacha akapigwa picha na dummy cheque iliyokuwa inasomeka tofauti: "Figures" tofauti na "Amount in words". Na walikuwepo.

  That is why nikasema tujadili.
   
 8. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #8
  Nov 13, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mi naona yule body guard wake ambaye huvaa mavazi ya kijeshi, yupo makini sana kuliko wale wanaovaa kaunda suti ambao wamejaa mbwembwe.
  Ukichek hiyo video utamwona afande alimwahi mkulu kabla hajafika chini after hapo wale wengine ndio wakaja kutoa lawama.
  Lakini wote waliconcetrate kwenye kumnnyanyua hakuna aliyejihami pengine kuna shambulizi lolote la kigaidi.
  Just imagine angekuwa ni Obama.
   
 9. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,653
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Sheikh Njabr El Duder anajibu kama ifuatavyo:

  Hilo neno "seeeee" haliko kabisa katika vocabulary ya Kiswahili and sounds like a reptilian hissing sound. Which goes to show kwamba JK is an Alien-Human hybrid (kwa Kiswahili tunaweza kumwita "jini") kama alivyo G.W. Bush ambaye, by the way, walikuwa wakielewana sana na JK enzi zile.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #10
  Nov 14, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Alianza kwa kulalamika hivi "Aisee" Ilibidi walinzi wake wajue kuwa kule kujikanyaga kunaashiria mabaya na wangemwahi kabla hajalamba mzinga. Baada ya hapo maneno aliyokuwa akiongea yalikuwa hayana mpangilio wala maana. Alikuwa anaanguka huku akisema "tutafanya zaidi, tutafanya zaidi." Inaelekea kuwa ahadi zake nyingi huwa hazitoki moyoni mwake: zinatoka mdomoni bila kushauriana na ubongo.
   
 11. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Problem is hata hao maofisa usalama wanafikiria ki "hardware" "hardware" zaidi badala ya kufikiria pia kuna "software" threat
  Hawajui threat ya hatari na kubwa zaidi kwa rais JK ni afya na si risasi.Nadhani analysis ya threat kwa JK inayotumika ni ile ile aliyotumia nyerere.

  Matokeo yake wanaweka mkazo kwenye kumvalisha bullet proof na kuzuia asiguswe na watu Physical prtection( (Mimi naziita hardware protection) wanasahau kumlinda na kisukari ambacho ni obvious tena chenye probability kubwa ya kumshambulia rais wetu.
   
 12. e

  ejogo JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2010
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  neno "aisee" la kiswahili halitokani na sentence "I say" ya kiingereza bali linatokana na "I see!" na maana yake ni "I undestand" yaani naelewa au nimekupata au kumbee!!!!
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Mnichague niwe mlinzi tatizo hili ntalimaliza. Nimesomea ulinzi securicor.
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kwa wanyakyusa neno Seeee ni kama kukemea au kuonyesha dharau. Sijui kwa upande wa Wakwere au kiswahili.

  Ni kabila gani seee ni kuhisi maumivu?

  sioni uhusiano wa seee na uzembe wa walinzi labda kama kuna hoja umeificha hutaki kuweka wazi ili sote tuweze kuchangia
   
 15. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #15
  Nov 14, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapo umenena, asante kwa marekebisho, nilimaanisha"i see" lakini kidole ki ka miss si unajua tena mambo ya one finger typing!!!! lol
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Nov 14, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Tuliwakumbusha mapema wanaChadema wenzetu kwamba tukitumia kete ya afya ya JK kama sera yetu itatuangusha wakati wa kampeni kwani tutaonekana ni watanzania tusio na huruma. tutaonekana ni chama cha visasi tunaombea watu wafe ili tushike hatamu za kisiasa. Dr Slaa kasema hatutaki kumwaga damu hata moja ya watanzania ha hata ya kikwete pia.

  Ni hulka ya watanzania kuwa na huruma hata kwa adui linapokuja suala la ugonjwa.
   
Loading...