Tujadili kuhusu matuta barabarani

Tujadili kuhusu matuta barabarani

Kwa jinsi ya uendeshaji wa magari wa Tanzania ulivyo mimi naona hayo matuta yaliyopo hayatoshi kabisa.

Ingekuwa juu yangu ningeweka matuta kwenye barabara kila baada mita moja ili kutia watu akili.

Upo sahihi kabisa mkuu, lakini shida ni pale viwango vya hayo matuta vinavyotofautiana...

Kuna aina fulani za matuta ni kama zinaharibu magari tu, yaani yainuka ghafla na ni marefu kwa kimo...

Kwa watu wenye kutumia magari madogo basi huwa wanapata tabu na baadhi ya parts za chini hukwanguliwa...
 
aisee umepoteaje ? nasikia huko mo town kumegeuga uwanja wa tigo ...wachaga wanakula tigo balaa kwa mabeki 3 wao....hebu nirushie hiyo cd nione maana siamini mie

nipo my dear, na mie nimefanya kusikia sikia tu juu juu, weekend hii ntapata full picture, kaa mkao wa kunyumba.
 
Kwa jinsi ya uendeshaji wa magari wa Tanzania ulivyo mimi naona hayo matuta yaliyopo hayatoshi kabisa.

Ingekuwa juu yangu ningeweka matuta kwenye barabara kila baada mita moja ili kutia watu akili.

The reckless driving and the reckless disregard for the safety of others shown by many of the drivers is beyond words!

I say we need more speed humps on just about every road, street, highway, expressway, and any other motor-vehicle passable way.

mkuu Nyani Ngabu nashukuru kwa mchango wako hapa.....umeshayaona aina ya matuta wanayoweka lakini?

BAsi tufike mahali, tutembee tu kwa miguu.....
 
Last edited by a moderator:
Wakuu habari ya Ijumaa?

Kwa wale watumiaji wa vyombo vya moto hususani kwenye bara bara kuu yaani highway, iwe kwa usafiri wa public au wa binafsi, kuna hii ninayoona binafsi kama kero ya matuta:

Kwanza, yapo mengi katika umbali mdogo
Pili, yapo matuta 'yasiyokidhi viwango' kwa maana ya kwamba matuta yote kwenye bara bara zetu hayana kiwango kinachofanana, mwengine makubwa, mwengine madogo, membamba lakini yamechongoka, ya lami na yasiyokuwa ya lami, ili mradi hakuna raha/comfort tena ya kusafiri

Najiuliza kwa nini serikali iingie garama kuweka lami kwa mfano, bara bara nzuri tu, kisha ije "iharibu" kwa kuweka matuta tena makubwa mno? Kwa mfanio bara bara kuu kutoka minjingu kwenda hadi dareda kuna matuta yamewekwa siku hizi, nahofia kiwango chake cha ubora na hivyo usalama wa watu na magari yao.

Ningeomba na wengine wenye uzoefu wa hii makitu watupie hapa tujadili huenda Magufuli akasikia maana kuna wakati nishamsikia akisema kuwa matuta kwenye highway yaondolewe

Niseme kwamba hii sio disrespect kwa waenda kwa miguu au wananchi wanaoishi kando kando mwa sehemu hizo....hapana...ni suala la aina na sehemu matuta yenyewe yanapowekwa...yanakidhi viwango? Kuna standards? kwa nini yanatofautiana hivi?

cc Bigirita watu8 KakaKiiza Mtambuzi Nyamayao Chocs neggirl Asprin Madame B @@amu Kipaji Halisi Remote Rejao Preta PakaJimmy Mzee wa Rula Filipo marejesho LiverpoolFC Lily Flower Eeka Mangi Kimey Teamo
Shikamoo shemeji.Siku hizi una maswali magumu kweli.Ni kwa vile serikali imeshindwa kusimamia taratibu na sheria ilizojiwekea ndio maana inaingia gharama zaidi kujaribu kutafuta usalama wa barabarani.Ni bora hayo matuta yaongezeke mpka hapo tutakapopata akili nzuri.
 
Lakini kwanini uvunje sheria?

sawa huwa navunja sheria coz nikiona hilo tuta hapo mbele yangu naona otee kabisa, lakini sijawahi kukamatwa kwa kuvunja sheria, nakamatwa na mambo yasiyoeleweka kabisa, ndio mana nikasema kuna wakati nagoma kuwapa chochote kabisa wataning'ang'ania, kuna siku wamenishindisha kituoni coz nilikataa/niligoma kuwapa kitu kidogo, kuna wanawake wawili wananichukia kabisaaa coz hao ndio niliowagomea kuwapa kitu kidogo so siku hizi nikikutana nao popote ni malumbano tu, watanitafutia sababu tu, siku nikiwa na haraka zangu inabidi niwape niendelee na safari, "nchi ya kitu kidogo"
 
ajali nyingi nilizozishuhudia na kusikia ni uzembe wa madereva[refer ajali za mabasi].....kwani hayo matuta si yanawekwa kwenye sehemu zenye watu wengi[karibu na vijiji/shule etc] ?huko mnakosema hamna matuta HIGHWAY zao mnazijua?kwanza zinapita mbali na residential areas au zikipita karibu zinawekwa fence na hakuna pedestrian anaruhusiwa kupita karibu[ni kosa la jinai]....hizi zetu tunazibatiza jina HIGHWAY hizi ni country lanes tu ndio maana zinapita vijijini....kuna watu,mifugo,wanyama pori so lazima waweke matuta kulinda usalama wa watumiaji wengine....msiangalie magari na comfortability zenu....fikirieni madereva[wengi] wa kibongo wanavyoendesha na watoto wa huko vijijini hizo "highway" zinapopita.....

mkuu I like your line of thinking kuhusu Highway...kumbe huku hakuna highway kabisa sio....
 
Shikamoo shemeji.Siku hizi una maswali magumu kweli.Ni kwa vile serikali imeshindwa kusimamia taratibu na sheria ilizojiwekea ndio maana inaingia gharama zaidi kujaribu kutafuta usalama wa barabarani.Ni bora hayo matuta yaongezeke mpka hapo tutakapopata akili nzuri.

Asee Zion Daughter.....apo umeongea kwamba wote hatuna akili nzuri eee? duh

Yaani kimsingi ni kwmaba sheria na hali halisi vitu viwili tofauti!
 
Last edited by a moderator:
mkuu Nyani Ngabu nashukuru kwa mchango wako hapa.....umeshayaona aina ya matuta wanayoweka lakini?

BAsi tufike mahali, tutembee tu kwa miguu.....

Nimeshayaona ndiyo.

Na mimi binafsi ni mwoga sana wa kuendesha gari Dar. Ni kero na hatari tupu. Si bodaboda, si bajaji, si vipanya, si vi coaster, si mikokoteni...ni hatari mwanzo mwisho.

Nikiendeshaga gari Dar, tuseme natoka nyumbani kwenda mjini nikirudi nyumbani bila kupatwa na road rage ntashangaa sana.

Yaani huwa ni lazima nimpe mtu finger na lazima nitukanwe na lijitu jingine ambalo halijui kuendesha kwa usalama na kistaarabu.

Unakutana na jitu linaendesha wrong way halafu ukilipigia honi eti wewe ndo unaishia kutukanwa. Gademu it.
 
mkuu I like your line of thinking kuhusu Highway...kumbe huku hakuna highway kabisa sio....

kwa maoni yangu...this is a HIGHWAY....huwa haina na haiwekwi matuta.....hapo kwenye fensi ya mbao kuna access wamezuia pedestrian wasikatize ingawa sheria ipo kwazuia ila usipodhibiti wanakula short cut

m1_1873351c.jpg
 
hahaah Kipaji Halisi unamaanisha nje ya nchi? kama nje ya nchi sawa hawana hii makitu bana,,,kule ni sheria mtindo mmoja na watu wako conscious, huku majanga

kama ni hapa mitaa ya bongo utakuwa umeona hii
avatar11959_12.gif
hivi anko@Kaizer unaweza kupita road zetu bila kukutana na matuta km si nje?...hii kitu uliyoweka ina wahusu KakaKiiza na Asprini...hahahahahahahahaha
 
Last edited by a moderator:
Katika pita pita zako huko nje umeona hao madereva wa nje wanavyotii sheria? huwezi kulinganisha na wakwetu
hapa yaani kwenye Zebra crossing mtu ndo anapisha gari.. wakati huko nje unakosema yaani ukikanyaga tu zebra dereva anaanzia kilometa kufungu break !
hahahahaha..mkuu hii kitu huwa nashangaa sana..mfano uliotoa ni wa ukweli sana...unafika zebra dereva ndio kwanza anaongeza mwendo....halfu huyo derva kumbuka ana leseni ujue..
 
Bongo hakuna highways za maana.

Kwa wenzetu kuna hadi mi freeways, expressways, interstates yenye lanes hadi kumi!

4887495099_f251e887a6_b.jpg


Halafu cheki hiyo concrete median. Kwa maoni yangu husaidia sana kupunguza head-on collisions.

14thin2004.jpg

huku mbali sana kaka....hata DUAL CARRIAGEWAY ingetosha.....halafu ikipita around built up area inawekewa fence...strictly no pedestrian....sasa single lane track inapita katikati ya kijiji/shule bila matuta si mnataka wanakijiji/wanafunzi wateketee.
 
Achia mbali kuharibu magari...kutingishwa ndo usiseme hasa kwa kinamama!!

Yani wameweka matuta kama vile wote watumiao muundo mbinu huo wana cruza tu kumbe kuna na Vitz!!
Sioni umuhimu wa kuweka matuta kwenye highways,dereva akiona kibao cha mwendo kasi chini ya km 50 anaelewa kabisa anatakiwa apunguze mwendo na ndo mana dereva anatakiwa awe zimetimia kichwani.
 
Mi nafurahi kwamba TBS sasa wako mbioni kuja na stanfards za matuta..kwamba yawe aina gani hasa...tunacholalamika ni kwamba hakuna kabisa standards kwenye hii kitu

Haya mambo lazima yawepo kisheria haki na wajibu wa kila.mmoja vianishwe
Chocs naomba kutambua mchango wako
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom