Matuta makubwa barabara za vumbi mitaani na vijijini yanavyo sababisha kero na uharibifu wa magari

HDP

Senior Member
Aug 22, 2015
163
93
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Kumekuwa na tabia ya kuweka matuta kwenye barabara za vumbi za mitaa au vijijini kwa nia ya kupunguza ajali katika mitaa husika hasa ajali za watoto zinazohusisha pikipiki.

Kufanya juhudi za kupambana na ajali ni jambo jema isipokuwa matuta hayo ambayo kuwekwa na raia wasio na taaluma ya uhandisi huwa makubwa na yasiyokidhi viwango vya aina za matuta barabarani.

Matuta haya husababisha kero na uharibifu wa magari madogo au ambayo yana uvungu wenye kimo kifupi.

Jambo baya ni kwamba kwa kuogopa kuharibu mahusiano siyo rahisi kuwafuata wahusika na kuwashauri au kuondoa matuta hayo maana wao hawana magari.

Nadhani kuna haja Serikali itoe muongozo wa matuta ya barabara za vumbi za mitaa/vijijini, na wawepo watu wenye mafunzo au uzoefu wa kuweka aina hiyo ya matuta.

Asante
 
Back
Top Bottom