Huu hapa ukweli kuhusu majini (eneo ambalo wanapatikana kwa wingi jijini Dar es Salaam)

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,120
27,126
Katika ulimwengu wa roho, Dar es salaam ni jiji ambalo wanaishi binadamu na majini.

Majini ni nini?

In my personal opinion which is based upon my personal understanding of the spiritual world, majini ni viumbe ambao kwa ujumla wao wapo more advanced in technology kuliko binadamu kwa ujumla wetu.

Ninapo sema kwa ujumla wao, majini wapo more advanced in technology kuliko binadamu simaanishi kwamba majini wote wapo more advanced in "technology" kuliko binadamu wote.

La hasha.

Ni sawa na tunaposema Marekani ndio taifa lililo endelea kiteknolojia kuliko mataifa yote duniani, hatumaanishi kwamba every individual american is more advanced in technology than every person who is not an American.

La hasha. Wapo raia kutoka nje ya Marekani ambao wao kwa sababu ya mahaba yao kuhusu teknolojia wame yatafuta kwa kina maarifa kuhusu teknolojia kadha wa kadha na uki walinganisha katika ufahamu wao juu ya teknolojia na wamarekani wengi, utakuta raia hao wa mataifa nje ya Marekani Wana ufahamu mkubwa kuhusu teknolojia kuliko idadi kubwa tu ya Wamarekani.

Wapo wahindi ambao wame ajiriwa Marekani kama wataalamu wa IT, Nuclear etc. Vivyo hivyo kwa upande wa majini na binadamu. Wapo binadamu wengi ambao Wana maarifa mapana kuliko majini.

Ninasema wao majini wameendelea kiteknolojia kuliko binadamu kwa maana ya kwamba uki chukua kiwango cha juu cha teknolojia kinacho milikiwa na majini ukalinganisha na kiwango cha juu cha teknolojia kinacho milikiwa na binadamu Basi kile kiwango cha juu cha teknolojia kinacho milikiwa na majini kipo juu zaidi ya kiwango kinacho milikiwa na binadamu wanao ishi katika sayari ya dunia. (Nimesema binadamu wanao ishi katika sayari ya dunia kwa sababu ufahamu wangu unaniambia kwamba wapo viumbe wenye kufanana na binadamu "humanoids" ambao wanaishi kwenye sayari na makundi nyota (galaxies) mengine.

Mungu ali tengeneza a billions of ADAM and EVE couples, ambao ali waplant kwenye mashamba (sayari) yake mbalimbali yaliyopo katika galaxies tofauti tofauti kwa sababu ambazo nitazielezea wakati mwingine.

Marekani ndio taifa lenye teknolojia ya juu duniani lakini wamarekani wenye access na maamuzi juu ya hiyo teknolojia itumike vipi wanaweza wasizidi elfu mbili.

Vivyo hivyo kwa majini. Pamoja na kwamba Ufalme wa kijini kwa ujumla wake (kuna falme nyingi sana za kijini) una hodhi teknolojia ambayo ipo juu kuliko teknolojia tunayo hodhi binadamu lakini majini wenye access na hiyo teknolojia au wanao weza kutumia hiyo teknolojia wapo wachache sana.

Katika.matrilioni ya majini wanao ishi katika sayari ya dunia pamoja sayari mama yao katika mfumo wetu wa jua (solar system) majini wenye access na teknolojia ya juu ya majini wapo chini ya elfu ishirini.

Sayari mama ya majini katika mfumo wetu wa jua ni VENUS. Huko ndipo yalipo makao makuu ya majini katika ukanda huu wa kinyota.

Majini hawaishi BAHARINI. Tunafikiri majini wanaishi BAHARINI KWA sababu kwenye bahari yetu upande wa bahari ya Hindi ndipo kulipo na short cut ya kwenda kwenye sayari ya Venus. Duniani yapo maeneo saba katika ulimwengu wa roho ambayo ni njia panda zinazo ikutanisha sayari ya Venus na sayari ya dunia.

Maeneo hayo yapo katika bahari ya Hindi katika mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Lindi, Mtwara, eneo la Unguja, Pemba na eneo jingine lipo nchini India.

Katika maeneo hayo ndipo ulipo njia ya short cut kutoka kwenye sayari ya dunia HADI ilipo sayari ya Venus yalipo makao makuu ya majini katika ukanda huu wa kinyota. Kikawaida/kisayansi (kwa teknolojia ya binadamu) safari kutoka duniani HADI ilipo sayari ya Venus huchukua siku 109.

Lakini kwa teknolojia ya kijini safari kutoka duniani HADI kwenye sayari Venus kupitia BAHARINI, hutumia dakika saba.

Ndio zile habari ulizo kuwa ukisimuliwa utotoni kwamba mtu akienda bahari saa tisa usiku na mayai saba ya ndege mmoja wa porini yaliyo fanyiwa vitu fulani fulani halafu akatamka Maneno fulani kisha akayatupa mayai hayo BAHARINI BASI bahari hupasuka na huonekana jiji zuri la dhahabu ambalo limeendelea kuliko duniani na kuna viumbe kama watu wanaishi huko plus kuna watu maarufu kutoka duniani wapo huko.

Huko ndipo ambapo wanadamu hupaita kuzimu. Ndio maana husemwa umbali kutoka duniani HADI kuzimu ni kilometa sifuri.

ITAENDELEA KESHO. MAHALI AMBAPO MAJINI WANAPATIKANA KWA WINGI JIJINI DAR ES SALAAM.

Jijini Dar es salaam yapo maeneo kumi na moja ambako hawa viumbe majini WANAPATIKANA KWA wingi sana.

Kati ya maeneo kumi na moja lipo eneo moja ambalo viumbe hao hupatikana kea wingi zaidi.

Huko bara Mizimu ni roho za watu walio fariki zamani au majini wa watu walio fariki. Yani kwamba KILA mtu anakuwaga na jini wake kwenye mwili wake. Huyu mtu akifa roho yake hurejea mbinguni lakini huyu jini wake hubaki duniani kuendeleza mahusiano na ndugu wa marehemu.

Lakini kwa washirikina na wachawi wa pwani, mizimu ni majini walio kusanyika sehemu moja kwa wingi.

Sasa kwa washirikina na wachawi wa viwango vya juu waliopo jijini Dar es salaam, eneo hili ninalo lisema hujulikana kama Mizimuni (sio Kawe Mzimuni). Huitwa Mizimuni kwa sababu katika eneo hilo kuna.idadi kubwa sana ya majini. There is an active djinn city in the area.

Kama umewahi kupewa dawa yoyote ile ya kichawi ukaambiwa nenda kaichome au kaifanye hivi vile nakadhalika ukafanya hivyo ukiwa ndani ya jiji la Dar es Salaam na dawa hiyo isifanye kazi bas probably hukufanya jambo hilo katika eneo ambalo majini wapo active..

Ukifanya uchawi wowote ndani ya eneo hilo uchawi huo hupata majibu ya papo kwa papo. Kwa mfano watu wengi hawajui kuhusu kazi ya mafusho mbalimbali. Kazi kubwa ya mafusho ni kufungua anga la majini husika.

Chochote cha kishirikina unacho kifanya katika eneo hilo hutoa majibu ya papo kwa papo kwa sababu majini wapo active sana katika eneo hilo. Chochote kuanzia mafusho, kafara nakadhalika.

Je, ni wapi mahali hapo? Usisumbuke kuni dm kwa sababu sitokwambia chochote ingawa nina pajua.

Ni mwiko kutoa siri hii. Unacho takiwa kufanya ni wewe mwenyewe kuanza kutembelea KILA kata ya jijinla dar es salaam na kufanya hizo kafara au kuchoma mafusho kupingana na siku husika. Mwisho wa siku utapajua ni wapi kupitia majibu utakayo yapata katika sehemu husika.

Kuisaidia tu muda mzuri wa kufanya hivyo ni usiku kuanzia saa tisa.

JE, MAJINI HUFA? Ndio majini HUFA.

JE, MAJINI WATAIONA PEPO?

(Jibu langu halitokani na ulicho fundishwa kwenye dini yako Ila linatokana na ufahamu wangu kuhusu majini)

Majini wote wazuri KWA wabaya hawata iona pepo.

Kwanini? Pepo wamehaidiwa binadamu tu. Majini wamenyimwa pepo kwa sababu GANI?

Kwa mujibu wa elimu halisi ya majini. Majini wamenyimwa pepo kwa sababu huishi kwa maelfu ya miaka.

Kwa mujibu wa elimu ya majini. Viumbe wanao ishi miaka mingi wakisha kufa ndio wamekufa. Hawapewi nafasi ya kuishi tena kwa mara nyingine. Kwa hiyo majini na viumbe wengine ambao wanaishi miaka mingi sana hawana pepo KWA mujibu wa elimu ya majini.

Majini walipata wapi teknolojia yao?

Tofauti na watu wengi wanavyo fikiria kwamba eti majini waliumbwa wakiwa na ufahamu wa KILA kitu, majini hawa kuumbwa wakiwa Wana ufahamu wa kila kitu.

They started with a very humble beginning. When they start to live in this planet they were as dumb and ignorant as Adam and Eve.

Walijifunza mambo yote wanayo yafahamu leo hii kupitia challenges walizo kutana nazo..

Hata sisi binadamu hatu kuanza kurusha ndege. Tulijifunza kurusha ndege.

Binadamu bado tunayo nafasi ya kujua mambo mengi sana kuhusu hii dunia.

KWA mtazamo wangu. Binadamu watako kuja kuishi hapa duniani miaka elfu kumi ijayo watakuwa wanatucheka binadamu tunao ishi SASA hivi KWA kushindwa kwetu kupata maarifa yakutufanya tuishi milele.

JE, MAJINI WANAJUA KILA KITU?

Hapana majini hawajui KILA kitu. Ila miongoni wapo majini wanao jua vitu vingi kutushinda sisi binadamu. Tofauti baina yetu sisi binadamu na majini katika maarifa ni kwamba huyu jini ambae hajui KILa kitu lakini anawajua majini ambao WANAJUA vitu vingi.

Anawajua sio kwamba ana access nao au anaweza ku interact nao. Ni kama vile wewe unavyo jua kwamba wapo watu wenye teknolojia ya nuclear lakini huna access nao.

Majini wengi hasa hawa wanao interact na waganga na wachawi ni majini wanao toka katika madaraja ya chini sana miongoni mwa majini na wengi wao hawana access na baadhi ya majini walio katika madaraja ya juu.

Wapo binadamu ambao KWA sababu ya maarifa yao Wana access na majini wa madaraja ya juu ambao hawa majini wa madaraja ya chini hawana access nao.

JINSI MAJINI WA UGANGA WANAVYO SHIRIKIANA NA BINADAMU.

Hii naiweka kwenye comment. Usi comment KWANZA mpaka ni ielezee hii
 
LIKUD

Mada kama hizi zimemfanya Mshana Jr àkapendwa sana, nimeshangaa hadi mwanamke mzuri kama Mamndenyi akamkubali huyu mtu kisa mada za uchawi na uganga.
 
JINSI MAJINI WA UGANGA/UCHAWI WANAVYO SHIRIKIANA NA BINADAMU.

Nimesha sema hapo juu kwamba sio kila jini anajua KILA kitu.

Sio kila jini anaweza kufanya KILA kitu.

Sio kila jini ana maarifa makubwa kuliko KILA.mtu.

Sio kila jini anaweza kufanya KILA kitu KWA KILA mtu.

Sio KILA jini anajua yatakayo tokea siku za usoni. Mfano Mfalme Suleiman alifanya kazi zake KWA kishirikina na majini.

Miongoni mwa walinzi wake walikuwa ni majini.

Mfalme Suleiman alipo fariki, HADI inafika siku ya tatu tangu Mfalme Suleiman afariki bado jini anae mlinda alikuwa hajui kama bwana wake amesha fariki toka enzi za Pontyo wa Pilato.

So inakuwaje kwenye uganga.

Bwana Kiranga Wewe ndo huyo umeenda KWA mganga Mshana Jr unataka kumuua kichawi ndugu DeepPond kea sababu amekuchukulia nyumba ndogo YAKO.

Bwana Mganga atawapa majini wake wa uganga kazi ya kumuua deep pond.

Tatizo ni kwamba majini wa Mshana hawana maarifa ya kuua mtu.

Lakini wanajuana na majini ambao Wana maarifa ya kuua mtu na wapo tayari kuua mtu.

Jini wa uganga wa Mshana, atamwambia Mshana nitakuletea taarifa ya kitu gani cha kufanya ifikapo saa saba usiku.

Jini wa uganga wa Mshana ataenda KWA majini wenzake ambao Wana maarifa ya kuua atawaambia ndugu zangu eeh nisaidieni kufanya kazi ya kumuua mwanadamu.

Hao majini wauaji wataomba majina ya huyo mtu anae takiwa kuuwawa.

Tatizo kwao nao ni moja hawana maarifa ya kupiga ramli na hawazijui details zote kuhusu binadamu wao wanacho jua ni kuua.

Ila na wao anajuana na jini mwenye maarifa ya falakh.

Wata enda KWA jini mwenye maarifa ya falakh.

Kazi ya huyu jini mwenye maarifa ya falakh ni kusoma nyota ya huyo mtu anae takiwa kuuwawa ILI kuangalia ILI operation ya kumuua mtu huyo ifanikiwe inatakiwa ifanyike siku GANI saa ngapi na eneo gani ( ardhini, angani, au kwenye maji)

Pia atatazama kama mtu huyo ana kinga na je kinga hiyo ni ya kijini au ya Mungu. Na kama.ni ya kijini wanatakiwa wafanye kitu GANI ILI kuidhoofisha hiyo kinga au kuua hiyo kinga kabla ya kupeleka shambulizi.

Huyu jini wa ramli huheshimiwa sana na hawa majini wauaji kama anavyo heshima gun supplier na ma armed robbers.


Huyu jini wa falaq akisha fanya intelligence analysis kuhusu mtu husika anatoa intelligence report ambayo itatumiwa na hao majini wauaji kama road map ya kwenda kumuua huyo binadamu husika

(Mara nyingi majini wanapo enda kumshambulia mtu bila kumconsult jini wa falaq huwa wanakuwa defeated na wanapokuwa defeated hurudisha taarifa KWA aliye watuma kwamba wamemshindwa mhusika. Hii HUTOKEA mara nyingi KWA WATU ambao kinga zao hazionekani na macho ya kichawi au macho ya kijini.. hapa hawa majini wataenda kichwa kichwa na mwisho wa siku wanakuwa defeated. The defeat is always not a good one for the djinn most of the time huwa ni kifo..ndio maana majini wakitumwa kumshambulia mtu wakakuta kinga yake ni kali BASI humrudia alie watuma na kumuua/ kufa nae)

SASA BASI huyu jini wa falaq anaweza kutoa report kwamba ili huyu deep pond auwawe lazima shambulizi dhidi yake KIFANYIKE akiwa ndani ya maji.

Na hawa majini walio pewa kazi ya kumuua deep pond wao territory yao ipo nchi kavu. Hawawezi kufanya chochote ndani ya maji

Watarudisha taarifa KWA jini wa uganga wa Mshana kwamba hiyo kazi hawawezi kuifanya wao KWA sababu mhusika anatakiwa auwawe akiwa ndani ya maji na wao hawana nguvu ya kufanya chochote ndani ya maji so wata mtefer jini wa uganga wa Mshana kwa jini muuaji ambae anaishi ndani ya maji.

Jini muuaji wa majini atachukua hiyo kazi lakini tatizo yeye hana uwezo wa kumvuta Deep Pond HADI pwani au majini.

Atatafutwa jini mwingine mwenye uwezo wa kumvuta Deep pond HADI ndani ya maji.

Jini wa falaq KWA sababu anakuwa tayari amemsoma Deep Pond anapenda vitu gani, atatoa ushauri kwamba jini pekee anaeweza kumvuta Deep pond HADI BAHARINI ni jini ashkhi majununi/ jini wa askhi na mapenzi.

Kumbuka hapo jini wa falaq alisha soma nafsi ya deep pond na kubaini kwamba Deep pond anatamani sana penzi la Nifah . Amesha omba mara kibao kutoka na Nifah lakini Nifah anamzingua.

KWA hiyo Jini wa Falaq atashauri kwamba huyu jini wa Mahaba aombe kuingia ndani ya moyo wa Hanifa amuwekee wazo la kutaka kukutana na Deep Pond lakini lazima wakutane Coco Beach.

Jini askhi akiingia ndani ya moyo wa Nifah, Nifah atapata ghafla wazo la Mahaba kwa Deep Pond.

Kwa kuwa nature ya mwanamke sio kutongoza mwanaume na majini hawana uwezo wa kufanya kazi kinyume na nature, Nifah atamtext Deep Pond kwamba ana hamu ya
Kula mihogo ya Coco Beach.

Deep pond hatoamini anacho kiona, KWANZA atanitumia Nifah hela ya nauli na ya kutolea halafu atawasha gari fasta kwenda coco Beach.

Wakifika coco Beach kea furaha ya kukutana na.Nifah, Deep Pond atalewa sana halafu baadae ataomuomba Nifah waende kuogelea.

Kumbuka kule ndani ya bahari kuna jini muuaji ametegwa anamsubiri Deep pond aingie BAHARINi.

Deep pond akiingia BAHARINi huyo jini muuaji wa BAHARINi ata mzamisha deep pond ndani ya bahari na habari utaishia hapo.

KWA hiyo umeona hapo kwenye task moja wamehusika zaidi ya majini watano.

Uliza chochote unacho taka kukijua kuhusu majini.
 
JE, MAJINI NI VIUMBE WABAYA?

JIBU NI HAPANA? Majini sio viumbe wabaya. Ila miongoni mwao wapo majini waovu.

Majini kwa ujumla. Wao ni viumbe Wema ila miongoni mwao wapo majini wabaya.

Majini walio Wema ni wengi kuliko majini walio wabaya.

Sisi tunafikiri majini wabaya ni wengi kuliko majini Wema KWA sababu binadamu Wana interact zaidi na majini wabaya kuliko Wema.

Kama Ng'ombe wangekua wanaongea halafu akatokea n'gombe mmoja aka shuhudia kile binadamu wanacho wafanyia ng'ombe pale vingunguti basi ng'ombe huyo akienda kwao u ng'ombeni atapeleka taarifa kwamba binadamu ni viumbe waovu sana.

Majini Wema ni wengi sana kuliko majini wabaya na wanachukizwa sana na namna majini wabaya wanavyo haribu taswira ya majini miongoni mwa binadamu.

Uliza chochote kuhusu majini
 
Uzi mtamu sana huu..

Nautabiria kufikisha views 1k..

On serious note, tupe jina la hilo eneo lenye majini wa kutosha japo kwa codes, tupe code tupambane nayo...
Ni mwiko kutaja. Unatakiwa ufanye utafiti mwenyewe KWA kwenda KILA kitaa ya Dar usiku kufanya ulozi. Siku utakayo fika kwenye eneo husika utaona utofauti hata wa hicho ambacho una kifanyia ulozi
 
Wenzetu wanashindana computer chips gani zinakwenda kuongoza Artificial Intelligence dunia ijayo.

Sisi bado tunajadili majini?
Majini ni viumbe ambao wapo more developed in technology kuliko binadamu. Look at them from this perspective and not from the spiritual perspective. May be we learn from their technology.. Refer to the mystery of Area 51 in Nevada.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom