Hoja hii hailengi kuamsha chuki dhidi ya imani yoyote, bali kutahadharisha kuhusu hatari ya kuingiza udini kwenye siasa. Tanzania ni ya wote bila kujali dini, dhehebu, kabila au historia.
Kwa miaka mingi walikuwa na "access pass" ya moja kwa moja hadi juu kabisa ya mamlaka. Walizoea kumuona Rais kama mmoja wao alie juu ya kiti badala ya kumuona kama kiongozi wa taifa, Ukaribu huu waliutumia kama njia ya kutoa kauli nzito, kushinikiza maamuzi na sera za kitaifa, na wakati mwingine kujiamini kana kwamba taifa hili halisongi bila baraka zao.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania ya kisasa, hali imebadilika, Hakuna Rais, hakuna mstaafu na kuna kila dalili hawatampata hata yule ajaye kwasababu dini sio kigezo tena, Hili sio tatizo kwa mtanzania anaemuona rais kama kiongozi lakini kwa watu wanaoendeleza mambo ya udini ni pigo kwasababu ikulu waliyozoea kuitumia iko mbali sana nao
Hawana mtu wao wa ‘kuongea naye moja kwa moja.’ Hawana nguvu ya kushinikiza. Na ukweli mchungu ni huu: Hawana tena mamlaka waliyodhani ni yao milele.
Na kinachotia wasiwasi zaidi ni namna baadhi yao wanavyojaribu kuingiza udini kwenye siasa wakionesha hasira zao wazi kana kwamba Urais ni mali ya dhehebu fulani kwasababu pindi walipokuwa marais wanaotoka madhehebu yao hakukuwa na hizi kelele, ila sasa wameanza.
Hii ni hatari. Nguvu ya taifa hailali kanisani wala msikitini inajengwa kwa msingi wa uwezo, maadili na uzalendo. Wanaohangaika kwa sababu tu “sio wao tena,” wanapaswa kujiuliza: walikuwa wanahudumia taifa au taasisi yao?
Tukumbuke, Tanzania ni ya wote. Kiongozi bora anaweza kutoka popote – si lazima avae kanzu wala msalaba. Tuitaadhari nchi yetu isiingie kwenye udini.