Mkuu Twahil, japo kweli kwa kiasi fulani ni propagandist, lakini hatungi uongo na sio poyoyo, huyu ni ex spy secret agent, hawa kazi yao ni kupewa tuu taarifa nyingine za ukweli na nyingine ni za uongo, kikawaida taarifa hizo hupokelewa toka sehemu mbalimbali kisha zinachakatwa, kuchujwa na kupepetwa, mchele unachukuliwa, pumba zinatupwa, sasa kinachofanyika ni Chahali bado ana wale colleague wake ndani ya system ambao wana muibia info, na kumlisha, sasa miongoni mwa info hizo pia yapo matango pori wao wanamlisha tuu na yeye anameza jumla kama hilo la CCM, wamemdanganya bado kuna ile CCM aliyoijua yeye, kumbe hajui kuwa sasa hakuna tena CCM, sasa kuna mtu, ndio chama, ndio serikali, ndio katiba, ndiye jeshi, ndiye polisi, ndiye Mahakama, who would dare challenge him?!, unless ni mwendawazimu!. Chahali hapo kalishwa tango pori akaingia mazima.
Sio tuu ndani ya CCM, bali hata nje, kwa mwaka 2020 Magufuli hana mpinzani, hana mshindani ni Magufuli tuu.
Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au Ni Magufuli tu?!. - JamiiForums
P