Tufundishe vijana wetu utaalamu wa kuongea kama Rais Samia Suluhu

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,749
Watanzania hatuna utamaduni wa kufundisha vijana wetu jinsi ya kujieleza na kuongea mbele ya watu. Hii inasababisha sana hata wataalamu wetu wengi kuonekana kama vile hawana utaalamu. Wenzetu kuanzia mtoto akiwa mdogo shuleni wanafundishwa jinsi ya kuwasiliana na hii inasababisha wanaweza kufanikiwa na kujiamini zaidi.

Yaani imefikia wakati unaona wazi kabisa wale wataalamu ambao wamesoma au nje na wale waliosoma Tanzania pekee. Lakini ukikuta mtu anajua sana kuwasiliana utakuta kafanya kazi kampuni ya nje za kimataifa au kufanya kazi na watu wa nje.

Mawasiliano mazuri sio kupiga tu kelele. Mfano mzuri ni Rais Samia Suluhu. Mimi naona watoto wetu wafundishwe zaidi mawasiliano. Hata Watanzania diaspora wengine wanapata wakati mgumu wa kazi kwa sababu ya mawasiliano.
 
Hii kitu ipo wazi kabisa LUGHA inaweza kuwapa nguvu waliokata tamaa, ukitumia lugha yenye ustaarabu hata watu hawatakuona kama kero na wanauwezo wa kuvumilia hata baadhi ya kasoro zako.
 
Watu wa zanzibar hao
Kama umewahi kuishi zanzibar hupati tabu kumuelewa
Hawana unafiki,nyeusi atakuambia hii nyeusi
Sio mijitu ya bara nyeusi itakukazia hii nyeupe!!!
Nashauri akimaliza muhula wake aje mwingine tena wa Zanzibar
Wa huku bara tupumzike kidogo sisi tusilaze zege tu,ili kazi iendelee
 
Hahhaa Wazanzibar wasipofanikiwa kutatatua kero za muungano awamu ya mama ssh basi ndio hawatatua tena.
 
Huyu Mama Mtamu wa mawasiliano, na macho yake ya urembo malegevu utadhani hurul ain,
Tunamuelewa sana, na anatusuuza nyoyo zetu
IMG-20210406-WA0058.jpg
 
Back
Top Bottom