Fredwash
JF-Expert Member
- Oct 27, 2009
- 1,041
- 1,377
Naomba Kujuzwa yafuatayo
Rais anapofungwa Bunge, je Bunge ndio linakuwa limevunjwa rasmi kwa maana ya Ubunge wa Mbunge unakoma? ( kwa maana ninavyofahamu pamoja na mtu kushinda/kuteuliwa kuwa mbunge ubunge wange unaanza rasmi pale alipokasimiwa/apishwa rasmi Bungeni).
2. Kama Bunge linapofungwa na Rais sio kuwa linavunjwa, basi ni wakati gani mbunge anakuwa rasmi sio mbunge?
3. Je Ubunge wa Mbunge unakoma tu pale Bunge linapofungwa na rais.? Je vipi kuhusu mazawiri, maana katiba inasema Waziri lazima awe Mbunge ( nakiri sijasoma hicho kifungu ila ndio inavyosemekana ninaweza kusahihishwa katika hili). Je uwaziri nao si unakuwa automaticaly umefutwa, au kuna kifungu kinamlinda waziri hata kama Ubunge hana tena kikatiba.?
4. Rais anavunjwa lini baraza la mawaziri, je ikiwa Bunge linapofungwa na Rais ndio linakuwa limevunjwa rasmi, kifungu kipi kinamuongoz Rais kuendelea na baraza lake la mawaziri(najua serikali ilipo madarakani kikawaida inakoma utawala wake pale baraza la mawaziri linapovunjwa).?
5. Kutokana na point namba 4 ikiwa hakuna kifungu kinachotoa uhalali wa baraza kuwepo wakat Bunge limevunjwa, haionekani kuwa ni mkanganyiko wa kikatiba kwa kuendelea na baraza la mawaziri wakati sio wabunge tena. je kwa nini Rais asivunje baraza la mawazir halafu ndio Bunge likawa la mwisho kuvunjwa ( sababu Rais ndio anaanza kuingia madarakani kisha anawateua mawazir na kuwaapisha) kwa nini asiwe wa mwisho kutoka madarakani kwa kuanza kulivunja baraza la mawaziri then anamalizia na kuvunja Bunge, sababu kuvunja kwake baraza la mawaziri hakutamuondolea haki ya kuwa Rais, urais haufungwi na baraza la mawaziri)
Wajuvi wa mambo haya mwageni nondo