Tuelimishane kuhusu Mbunge, kuvunjwa kwa Bunge na Baraza la Mawaziri

Fredwash

JF-Expert Member
Oct 27, 2009
649
500
Naomba Kujuzwa yafuatayo

Rais anapofungwa Bunge, je Bunge ndio linakuwa limevunjwa rasmi kwa maana ya Ubunge wa Mbunge unakoma? ( kwa maana ninavyofahamu pamoja na mtu kushinda/kuteuliwa kuwa mbunge ubunge wange unaanza rasmi pale alipokasimiwa/apishwa rasmi Bungeni).

2. Kama Bunge linapofungwa na Rais sio kuwa linavunjwa, basi ni wakati gani mbunge anakuwa rasmi sio mbunge?

3. Je Ubunge wa Mbunge unakoma tu pale Bunge linapofungwa na rais.? Je vipi kuhusu mazawiri, maana katiba inasema Waziri lazima awe Mbunge ( nakiri sijasoma hicho kifungu ila ndio inavyosemekana ninaweza kusahihishwa katika hili). Je uwaziri nao si unakuwa automaticaly umefutwa, au kuna kifungu kinamlinda waziri hata kama Ubunge hana tena kikatiba.?

4. Rais anavunjwa lini baraza la mawaziri, je ikiwa Bunge linapofungwa na Rais ndio linakuwa limevunjwa rasmi, kifungu kipi kinamuongoz Rais kuendelea na baraza lake la mawaziri(najua serikali ilipo madarakani kikawaida inakoma utawala wake pale baraza la mawaziri linapovunjwa).?

5. Kutokana na point namba 4 ikiwa hakuna kifungu kinachotoa uhalali wa baraza kuwepo wakat Bunge limevunjwa, haionekani kuwa ni mkanganyiko wa kikatiba kwa kuendelea na baraza la mawaziri wakati sio wabunge tena. je kwa nini Rais asivunje baraza la mawazir halafu ndio Bunge likawa la mwisho kuvunjwa ( sababu Rais ndio anaanza kuingia madarakani kisha anawateua mawazir na kuwaapisha) kwa nini asiwe wa mwisho kutoka madarakani kwa kuanza kulivunja baraza la mawaziri then anamalizia na kuvunja Bunge, sababu kuvunja kwake baraza la mawaziri hakutamuondolea haki ya kuwa Rais, urais haufungwi na baraza la mawaziri)

Wajuvi wa mambo haya mwageni nondo
 
Kitaturu

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
6,073
2,000
Maswali mazuri ya kuelimishana japo nadhani katiba ya JMT ya mwaka 1977 inayo majibu ya yote hayo....

Lakini tukubali kuwa these are very challenging questions kuhusu mfumo wetu wa utawala wa kikatiba kuwa una mapungufu makubwa....

Mfano kwa kipindi cha kuanzia sasa hadi serikali nyingine kuundwa ni takribani miezi 6 au 7 hivi....

Kama kukitokea jambo hapa katikati linalohitaji maamuzi ya ushiriki wa wananchi kupitia bunge, nini kitafanyika? Je, serikali itaamua tu bila kupitia bunge? Au Rais atalazimika kuitisha bunge maalumu (la hawahawa waliokwisha vunjiliwa mbali) ili kuamua?
 
MakaDik

Member
May 31, 2019
75
95
Wana jamvi naomba kujua.

Hivi baada ya bunge kuvunjwa maana yake mbunge nafasi yake imefikia ukomo.

Je, Kwa aliye na nafasi ya uwaziri inakuwaje kuendelea na kazi au ndo mwisho wa uwaziri pia?

Kama ni ndivyo Rais anabaki kufanya kazi na nani?
 
Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,544
2,000
Wataalam wa sheria na katiba naomba msaada kufahamu hawa wanaozunguka mitaani na kujiuta mawaziri na manaibu wanauhalali gani na hali sio wabunge?
 
mandolo

Senior Member
May 21, 2020
124
250
Uwaziri mpaka baraza la mawaziri livunjwe nalo linataratubu zake
Waziri lazima awe mbunge tena kwa kiapo cha ubunge, kiapo kile kimevunjwa jana. Labda tuambie unatumia kipengele gani cha katiba kuhalisha uwaziri wa mtu asiyekuwa mbunge.
 
Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
520
1,000
Poleni na msiba wa Benjamini Mkapa.

Kuna jambo linanisumbua mimi sio mjuzi wa mambo ya katiba ila kwa kiasi fulani najua kwa uchache.. nashangazwa na akina Jenista Mhagama kuendelea kujiita Mawaziri huku bunge limevunjwa. Sasa wajuzi wa sheria na katiba mnijuze.
 
GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
3,209

Ndio bado ni mawaziri mpaka watakapoapishwa mawaziri wapya na kukabidhi ofisi

Serikali lazima iendelee na kazi
 
Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
520
1,000
Ndio bado ni mawaziri mpaka watakapoapishwa mawaziri wapya na kukabidhi ofisi

Serikali lazima iendelee na kazi
Nashukuru comrade kwa kunipa uelewa...sasa naomba unijuze katiba inasemaje kuhusu nafasi ya mtu kuwa waziri?
 
Hazchem plate

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
9,052
2,000
Hata mm nashangaa

Mtu kuwa Waziri anaanza kwanza kuwa Mbunge then ndo awe waziri

why anatolewa sifa ya ubunge (sifa ya awali) na anaendelea kuwa na kofia ya pili?? ( Uwaziri)
 
Katiba yetu inashida sana..nami kichomi changu kipo hapo. Ukiwa mbunge ndio unakuwa Waziri ubunge umekwisha kwa mujibu wa katiba lakini bado mtu anakuwa waziri
 
Hazchem plate

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
9,052
2,000
Katiba yetu inashida sana..nami kichomi changu kipo hapo. Ukiwa mbunge ndio unakuwa Waziri ubunge umekwisha kwa mujibu wa katiba lakini bado mtu anakuwa waziri
For the time being, makatibu wakuu ndio walitakiwa wawe top until Kuna baraza jipya la mawaziri. ila hakuna ubaya sana maana Watendaji wakuu wa wizara ni Makatibu wakuu ambao wengi wao ni proffesionals wa taaluma husika na ndio waidhinishaji wakuu
 
Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
7,337
2,000
For the time being, makatibu wakuu ndio walitakiwa wawe top until Kuna baraza jipya la mawaziri. ila hakuna ubaya sana maana Watendaji wakuu wa wizara ni Makatibu wakuu ambao wengi wao ni proffesionals wa taaluma husika na ndio waidhinishaji wakuu
Hii mambo ya kuchukulia mambo kimzaha na kienyeji ndio maana mambo hayanyooki, unasema sio mbaya sana, taifa zima linachukulia kupindishwa kwa sheria na taratibu hivi kuwa si mbaya sana. Kielezwe kipi ni kipi na kifuatwe.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom