Siyo kirahisi hivyo. Kuna mambo ya haki za binadamu na kina UN wataingilia kati.Sasa nani kakubana?
Ardhi mnamiliki.
Biashara mnafanya.
Na Hambaguliwi.
HESLB mnakopeshwa kwa Kodi za watanganyika.
Na Ajira mnapata huku Tanganyika
Wazanzibari ndo wanafaidika na huu muungano, ukivunjwa, ardhi zote mnanyanganywa, ajira zote mnapokonywa na hamtasomeshwa kwa hela za walipa Kodi wa Tanganyika.
Maana huko Zanzibar, Mtanganyika hawezi miliki ardhi, hawezi Jenga nyumba, biashara kule ni ngumu kufanya kwa Mtanganyika, Kuna ubaguzi wa kidini na wa kikabila kwa Watanganyika .
Sasa Muungano una Faida gani kwa Mtanganyika?
Siku muungano ukivunjika inawezekana kukawa na kipindi cha mpito ambapo inawezekana Wazanzibar waliopo bara wakapewa uhuru wa kuchagua, kubaki bara na haki zao zote zikalindwa mfano kupewa uraia wa Tanganyika au kurudi Zanzibar na kinyume chake. Rejea kuvunjika kwa Sudani. Wapo weusi waliamua kubaki Sudan ya Khartoum
Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app