Trust katika Mahusiano

Trust katika Mahusiano

hahahahaha haya ndio mambo ya kusikia jina la yule motto nisiyempenda yaani ukiuliza tu utaambiwa sijui mama. Na kweli ukimkazia macho na kuonyesha msimamo utaambiwa ni kweli mama nimesema uongo hapo itabidi ianze risala tena. Naamini uongo wa kitoto huwa una mwisho sababu wanaogopa sana kuchapwa ndio maana wanasema uongo. Na wakati mwingine hawapendi ujisikie vibaya
ni kweli rafiki huwa una mwisho...
halafu watoto wana stage, mwanzo wanakuwa honest sana, yaani ukitaka stori za home wewe kamata mtoto atakuhadithia kila kitu..... a
akikua kidogo yaani unaweza tamani kulia kwa uongo, anadanganya mpaka unashangaa huyu mtoto katokea wapi.
baadae akiacha ndo basi tena
 
Ujue FP, kinachosumbua kwanza ni dhamira

Je, umedhamiria kuficha ama ni kitu ambacho hujakipa umuhimi wowote? Kama kweli k=hukukipa umuhimu wowote sawa, ila kama umeficha kwa kusudi mie nitakuwa na tatizo.

Ulishawahi sikia kuwa wapenzi 'talks about everything and nothing'?

mi naomba unifundishe hapa maneno ya kusema....
yaani mf nimekutana na x njiani, tunapishana fulani hivi, sababu tunafahamiana tunasalimiana then kila mtu anaenda na hamsini zake. nikifika home naanzaje kusimulia hiyo hadithi? mbona simhadithii habari za watu wote niliokutana nao siku nzima njiani ambao anawafahamu? Kongosho naomba mwongozo kwa hili, naanzaje kuisimulia? I am serious
 
Unajua mie tatizo linaanza pale mtu anapokuwa na wasi wasi wa kusema

Kama ulikutana naye benki kwa bahati, na wewe uliporudi wala hukumbuki sina tatizo

Ila kama unaficha kwa makusudi hapo tatizo linakuwepo

Yaani tuseme yeye wakati anaingia benki mimi ndo namalizana na bank teller - tuseme pale NBC Mlimani.

Aliponiona akanipungia mkono na mimi nikampa head nod halafu huyo nikasepa zangu (bila hata kuongeleshana).

Ina maana nikirudi nyumbani ni lazima niripoti kwako kwamba nimeonana na ex wakati niko benki?

That to me is very petty. Na sioni umuhimu wala ulazima wa kukumbuka kuja kukwambia. Na hata ukiniuliza nitakwambia ndiyo kwa sababu hakuna baya nililotenda na hivyo hakuna la kuficha na sikuona umuhimu wala ulazima wa kukwambia kwa sababu tumekutana/kuonana kama vile ambavyo nimekutana/nimeonana na wateja wengine waliokuwemo benki kwa wakati huo.
 
Nilishasema sisemi uongo usio na tija, maana nikikudanganya ni sign kwamba nakuogopa; so kama kungekuwa na uwezekano wa kumdanganya Mungu (ninayemuogopa) huenda ningefanya hivyo lakini there is now way naweza mdanganya yeye anijuaye kuliko ninavyojijua mwenyewe.

Hivyo sioni na sitakaa kuona umuhimu wa uongo uso na faida. halafu kwenye mahusiano, mimi naamini ni vyema mtu akujue tangia mapema udhaifu na mapungufu yako ili afanye informed decision lakini pia inakusaidia wewe usiishi maisha ya kupretend.

Lakini kuna wakati UONGO huokoa mahusiano yasivunjike!!!
 
Kama wamekutana bila kupanga sitaumia

Nilidhani wamekusudia kuonana, hata kama walikusudia kuonana kwa sababu muafaka, bora tu nijue

Ile kuficha itanifanya nianze kuwa na maswali
hapo kwenye kupanga kuonana ningependa sana niambiwe kabla hawajakutana kuliko baada.
wewe niambie tu, leo nimepanga kukutana na fulani, wala huna haja ya kuniambia sababu ya kukutana kwenu, kama sipendi ukutane naye basi nitakuambia nakuomba usikutane naye.
lakini ukipanga kukutana naye halafu usiniambie, ukaja kuniambia baada ya kukutana naye huo pia naona upo kwenye group la uongo. kwa nini hukuniambia before?
ila hilo la kukutana foleni ya bank then kila mtu akatambaa alikotoka, wala huna haja ya kuniambia
 
Ha ha ha ha ha, jamani!

Au umemuona ex wako anapanda daladala la Makumbusho - Bagamoyo wakati unaelekea pale CRDB kuchukua hela kwenye ATM.

Hii nayo lazima uiripoti kwa habibi wako? 'Habibi leo wakati navuka barabara kwenda pale benki CRDB Makumbusho karibu na kituo cha mabasi nimemuona ex wangu akipanda daladala' :becky:
 
mi naomba unifundishe hapa maneno ya kusema....
yaani mf nimekutana na x njiani, tunapishana fulani hivi, sababu tunafahamiana tunasalimiana then kila mtu anaenda na hamsini zake. nikifika home naanzaje kusimulia hiyo hadithi? mbona simhadithii habari za watu wote niliokutana nao siku nzima njiani ambao anawafahamu? Kongosho naomba mwongozo kwa hili, naanzaje kuisimulia? I am serious

Kama hukumbuki ukifika nyumbani, manake halimo kabisa akili mwako. Kwa hiyo hulazimiki kuhadithia

Ila kama lipo kichwani mwako na huhadithii hilo ndo ninapoliona tatizo
 
Au umemuona ex wako anapanda daladala la Makumbusho - Bagamoyo wakati unaelekea pale CRDB kuchukua hela kwenye ATM.

Hii nayo lazima uiripoti kwa habibi wako? 'Habibi leo wakati navuka barabara kwenda pale benki CRDB Makumbusho karibu na kituo cha mabasi nimemuona ex wangu akipanda daladala' :becky:
ha haaa, ntakutimua kabla hujamalizia sentensi, lol!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Jamani, tunasema kuonana nilidhani tunamaanisha watu kukutana na kuongea mawili matatu

Hii ya kukutana bank na kupungia sio kitu

Yaani tuseme yeye wakati anaingia benki mimi ndo namalizana na bank teller - tuseme pale NBC Mlimani.

Aliponiona akanipungia mkono na mimi nikampa head nod halafu huyo nikasepa zangu (bila hata kuongeleshana).

Ina maana nikirudi nyumbani ni lazima niripoti kwako kwamba nimeonana na ex wakati niko benki?

That to me is very petty. Na sioni umuhimu wala ulazima wa kukumbuka kuja kukwambia. Na hata ukiniuliza nitakwambia ndiyo kwa sababu hakuna baya nililotenda na hivyo hakuna la kuficha na sikuona umuhimu wala ulazima wa kukwambia kwa sababu tumekutana/kuonana kama vile ambavyo nimekutana/nimeonana na wateja wengine waliokuwemo benki kwa wakati huo.
 
Ujue FP, kinachosumbua kwanza ni dhamira

Je, umedhamiria kuficha ama ni kitu ambacho hujakipa umuhimi wowote? Kama kweli k=hukukipa umuhimu wowote sawa, ila kama umeficha kwa kusudi mie nitakuwa na tatizo.

Ulishawahi sikia kuwa wapenzi 'talks about everything and nothing'?
ha haaa, hiyo verse sijui nimeielewa? lol!
yes, dhamira inahusu hapa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
On point

Ndio maana nikasema, kama hakumbuki ni kwamba hata dhamira yake iko clear
Ila kama la kusema lipo ila anaogopa kusema sababu sitopenda tatizo lipo

Kama hukumbuki ukifika nyumbani, manake halimo kabisa akili mwako. Kwa hiyo hulazimiki kuhadithia

Ila kama lipo kichwani mwako na huhadithii hilo ndo ninapoliona tatizo
 
ha haaa, huyo shosti kabobea kwa kamba? maana mashosti wengine ni wazuri kwenye hizo anga! mpaka unachoka kuwasikiliza yaani
Nina rafiki yangu nampenda sana . Huyo akikwabia yuko njiani anakuja basi wewe tafuta kitu kingine ufanye maana huenda anakuambia hivyo bado yuko kitandani. Sasa kama mmepanga kwenda mahala flani lazima akucheleweshe na mpaka hamu ya safari itaisha. Lkn kwa vile nilishamjua hanipi shida naendelea kumpenda na kumvumilia. Unajua kila mtu ana mapungufu yake na mara nyingi mapungufu haya hufunikwa na mema mengi. Huyu rafiki yangu ni mtu mwema sana na ni zaidi ya ndugu.
 
ha haaa, kweli dhamira itanisuta kama tulisubiriana, lakini kama tulikutana kwa bahati mbaya........
hapo sasa ndo nitamwambia kuwa tulikutana kwenye daladala

Unamwambia so what?

What if na kesho coincidentally mnakutana tena utamwambia?

Haya mambo mengine hana tija kabisa na nikutaka kuwaharibia wenzenu mood...

Na akishindwa kazi unaanza kumlaumu wakati wewe mwenyewe ndiye mchawi...

Naomba mtu asinambie mambo ambayo hayana tija na wala hayagusi uhusiano wetu...!

Babu DC!!
 
Yaani unakuta wapenzi wanaongea kwa muda mrefu, wanaongelea kila kitu vya muhimu na visivyo muhimu
Ngoja niweke maana yake nisije kuichakachua bure

'A conversation in which two or more people talk for hours, discussing everything under the sun, and yet some of the topics were so random and pointless that it seems like they talked for hours about nothing.'

ha haaa, hiyo verse sijui nimeielewa? lol!
yes, dhamira inahusu hapa.
 
Kama hukumbuki ukifika nyumbani, manake halimo kabisa akili mwako. Kwa hiyo hulazimiki kuhadithia

Ila kama lipo kichwani mwako na huhadithii hilo ndo ninapoliona tatizo
naweza nikawa nakumbuka kabisa lakini siyo kwa feelings.... yaani ni kama ambavyo nimepita mtaani nikakutana na Jane na jioni nakumbuka kuwa nilikutana na Jane lakini siyo muhimu kumwadithia hubby kuwa leo nilikutana na Jane, after all Jane is just a person. sasa iweje nimwadithie kuwa nilikutana na Ali wakati kwa sababu zile zile za kutokumwadithia kukutana kwangu na Jane zina-apply hapa?
 
Jamani, tunasema kuonana nilidhani tunamaanisha watu kukutana na kuongea mawili matatu

Hii ya kukutana bank na kupungia sio kitu

Okay, basi tuseme maongezi yenu yaliishia kuambiana 'mambo?' na 'poa' halafu kila mtu akashika hamsini zake. Hilo nalo ni lazima kuliripoti?
 
ni kweli rafiki huwa una mwisho...
halafu watoto wana stage, mwanzo wanakuwa honest sana, yaani ukitaka stori za home wewe kamata mtoto atakuhadithia kila kitu..... a
akikua kidogo yaani unaweza tamani kulia kwa uongo, anadanganya mpaka unashangaa huyu mtoto katokea wapi.
baadae akiacha ndo basi tena
Yaani umenichekesha sana na umenikumbusha habari ya nyumbani kwangu yaani mtot anakudanganya mpaka unajiuliza walinibadilishia nini nilipojifungua unatamani sijui hata umfanye nini tu. Kwangu mimi hii issue ya kupiga mswaki huyu wa mwisho bwana anaoga vizuri , sasa muulize je umepiga mswaki atasema ndio mama . Huwa namwita ili nimkague nakuta amenidanganya basi utamsomea hapo risala lkn akisahau anarudia tena sasa siku hizi kuna mkakati nimemuwekea akisema uongo tu hakuna kwenda kucheza. Naamini akikua ataacha nae ana mazuri yake mengi sana kiasi kwamba nampenda sana.
 
Back
Top Bottom