Hahahaaaaaa!!! Leo sijui
FP umeamkia wapi dada yangu?
Vipi dada unaenda kwa shangazi au kwa kaka?
Back to topic.
Uaminifu umekuwa ni kitu hadimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Ni watu wachache sana ambao katika maneno yatokayo mdomoni mwao kila neno huwa la kweli. Watu tumekua na udanganyifu katika maisha yetu ya kila siku, hii inatokana na jinsi tulivyojichagulia kuishi.
Binafsi nimekua mdanganyifu pale ninapoona mambo yanakuwa magumu, ila naamini sio mimi tu, tupo wengi wenye tabia hii ya udanganyifu.
Mfano:Mmeahidiana na Boss wako mkutane mahali fulani kwaajili ya kitu fulani, ila muda unakwenda halafu unakuta Boss amefika kabla yako na anapokupigia simu kukuuliza uko wapi? Unamjinu upo maeneo ya karibu na pale mlipoahidiana mkutane, wakati unawezakuta hiyo simu aliyokupigia Boss wao ndo imekukumbusha kwamba mlikua na appointment.
Hapo tunaona udanganyifu unaweza kukusaidia kufanikisha dhumuni mlilokuwa mnataka mlikamilishe au inaweza kukufanya upoteze uhusiano mzuri na wenzako pale utakapomdanyanya na akakusubiri kwa kipindi kirefu nila wewe kutokea.
Tumuomba Mungu atuomdolee tabia ya udanganyifu akilini mwetu huku nasi tukihjitahidi kujifunza kusema kweli ambayo itatuweka huru.