Trump launches military strike against Syria

Trump launches military strike against Syria

Kwanini mnasema Urusi alizima defence zake?
Nani mwenye uhakika?
Je kama angezima angejitokeza leo kupiga kelele?
Ninavyojua ingetokea kama angefunga mitambo yake basi angeongea leo kuwa yeye alikubali

Mkuu Russia hajazima defence zake bali amezima njia ya mawasiliano ya salama au "preliminary comms."

Hiyo sehemu iloshambuliwa ni kama vile ile sehemu ya Kipawa pale Air wing kwwamba ndege zinafanyiwa ukarabati.

Ila Russia amewekeza kwa vifaa mbalimbali vya kisasa na ndipo ndege nyingi za kivita za Syria zinatokea hapo kwenda kufanya mashambulizi.
 
Unajua huwa sielewi namna wanavyohalalisha haya mambo!! Yaani Assad kaua kwa sumu raia, anakuja Marekani na suluhisho la kuua raia walewale kwa mabomu?!! Hii inasaidia nini sasa, kwa sababu kama ni Assad ndiye aliyeua si bado yupo?!! Halafu unakuta kilaza anashangilia. Hii proxy war ya US na Russia inawaumiza zaidi raia wa Syria kuliko huyo Assad.
Kweli kabisa! Wangemlenga mahali Asaad alipo wangeonekana wa maana!
 
Watu wanauliza kama makombora 23 kati ya 36 yenye thamani ya dola milioni 54 hayajulikani yametua wapi,au ndo kamchezo kama kale ka kina bashite unapiga mkwara mzito kisha unawafuata waarabu kuwatoa ngawira na magari kwa lazima.
Makombora yameyukia hewani,

hivi makombora 59 yatazikosakosa vipi ndege ambazo zilikuwa zimepaki peupe na wala si ndani ya hangar lao,?

April 7, 2017
“Where Did They Go?” AsksRussiaAfter 36USMissiles Fired AtSyriaFail To Arrive
By: Sorcha Faal, and as reported to her Western Subscribers
An interestingMinistry of Defense( MoD) report circulating in the Kremlin today states that Federation military commanders have failed to receive an explanation from their US military counterparts on the whereabouts of 36 Tomahawk cruise missiles( valued at $54 million) said by the Americans to have been fired into the Levant War Zone(Syria)—but as of now appear to have just disappeared.[Note:Some words and/or phrases appearing in quotes in this report are English language approximations of Russian words/phrases having no exact counterpart.]
According to the official MoD statement about this incident:
“ On April 7, from 3.42 to 3.56 (MSK), two destroyers of the US Navy (USS Ross and USS Porter) made a massive strike with 59 Tomahawk cruise missiles from the area near Crete Island against the Syrian Shayrat Air Base (Homs province).
According to the objective monitoring data, 23 missiles reached the Syrian Air Base.
As a result, an equipment depot, a training building, a mess, six MiG-23 aircraft in repairing hangars as well as a radar station were destroyed. The runway, taxiways and aircraft of the Syrian Air Force at parking places were not damaged. According to the information received from the Air Base Command, two Syrian servicemen are missing, 4 were killed and 6 got burning wounds during firefighting.
Therefore, the combat effectiveness of the American massive missile strike on the Syrian Air Base is extremely low.”.

“Where Did They Go?” Asks Russia After 36 US Missiles Fired At Syria Fail To Arrive
Naona mkuu unajifariji... Kibabu putin Jana kimevuliwa pajama
 
Hakuna vita kati ya Russia na USA Russia atahangaika kuipa silaha Syrian army tu ila hatosubutu kuingia vita na usa
Hali kadhalika Marekani hatothubutu kuingia vitani na urusi! Ndio maana ubabe wa urusi kwa Ukraine na kumega Crimea marekani aliishia kutoa mapovu tu na kuweka vikwazo vya kiuchumi lakini hakusogeza pua yake kijeshi!
 
Mkuu, Marekani waliwapa Russia warning la shambulizi dakika 30 in advance lakini Russia hakuwa na muda wa kujibu au kuruhusu shambulizi hilo.

Njia hii ya mawasiliano yaitwa "preliminary communication" au PRECOM yaani kunapokuwa na sintofahamu katika anga kama la Syria kunakuwa na kuhakikisha vifaa, eneo linaloegeshwa ndege au facility lipo OK.

Majeshi ya anga ya Marekani na Russia, wanayo hii njia ambayo wanatumia kuambizana kuepusha ndege kugongana au kama kuna tatizo kama la makombora kutupwa.

Pili, Russia wamezima njia hii ya mawasiliano leo baada ya shambulizi hili na siyo kabla na hii imethibitishwa na KREMLIN.

Kwa sasa hakuna njia ya mawasiliano na yoyote atakaefanya chochote atakutana na Russia amejiandaa vizuri zaidi.
Unafanya uchambuzi kwa pande zote Bila mihemko
 
Mkuu, Russia hawajapeleka S400 walipeleka S300 hata hivyo ziko kwenye kambi za kirusi ambazo wanaopereti warusi, haziko kwenye kambi za wasiria, huo mfumo uliwekwa kwa ajili ya warusi pindi ikitokea kitisho cha mashambulizi kwenye maeneo ya warusi nasio maeneo ya wasiria.
Leo mnabadirisha maneno... Bado itafika sehemu mtasema hizo s300 hazikuwahi kufungwa Syria....
 
Hakuna aliyekuwa na nguvu na ubabe kama Goliath wa kwenye bible. Lakini aliuawa na Daudi kijana mdogo sana tena kwa jiwe dogo. Kwa hiyo diplomasia ni bora zaidi kuliko kutumia nguvu. US isidhani ndo yenye nguvu kijeshi peke yake
Mkuu Daudi huyu Bashite wa kolomije au daudi mwingine unamzungumzia
 
You are extremely wrong! Kwa sasa hutaiona marekani ikishambulia Syria tena! Warusi wametoa red warning na wakazima mawasiliano ya moja kwa moja ya kijeshi na marekani nchini syria! Maana yake ni kuwa kama wakishambulia tena watafanya hivyo bila kutoa taarifa kwa urusi na wajiandae kwa kujibiwa mashambulizi!
Hiyo habari nimeipata mkuu,

Nazani sasa tuone kitakacho ajiri
 
Aaah mimi nilifikiri ni website ya CIA... Sasa hii link ulioweka Si kiblog kama cha miladiayo watu wanachangia kwa utashi wao..
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ila ww jamaa bhana et MillardAyo[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Leo mnabadirisha maneno... Bado itafika sehemu mtasema hizo s300 hazikuwahi kuelewa Syria....
Mkuu, nime make mistake kwenye hiyo statement ila syria kuna air defense s-200, s-300, s400 na ina nyengine za defence ila kwa s-300 na s-400 zilizoletwa na russia ni kwa ajili ya rassian base tu na sio kwa syrian base, hakuna makubalian ya hizo efence kulinda syria ni kulinda base za kirussi pindi ikitokea hatari na ndio maan unaona israil na america bado wanashambulia syria na sio wanashambulia base za kirusi.

The S-300 missile systems were deployed at Syria’s port of Tartus in 2016, to provide protection for both the base and Russian military ships in Syrian waters.

Source rt.
 
Kwanini mnasema Urusi alizima defence zake?
Nani mwenye uhakika?
Je kama angezima angejitokeza leo kupiga kelele?
Ninavyojua ingetokea kama angefunga mitambo yake basi angeongea leo kuwa yeye alikubali
Hivi unajua kingetokea nini kama asingezima mitambo yake?
Ni kuwa Marekani aidha wangeamua wasishambulie au wangeanza kwanza kuishambulia mifumo ya ulinzi wa anga ya urusi! Wakifanya hivyo maana yake ni kuwa wameanzisha vita na urusi! Hakuna kichaa marekani mwenye ubavu wa kuanzisha vita na urusi!
SAA hii sehemu kubwa ys ulaya na marekani ingekuwa ni majivu!
 
mkuu zote zipo,yaani S-400 na S-300,
na zote zinacover karibu syria yote kuachia mashariki ya syria,zimecover mpaka israel karibu yote kwa maana kuwa ndege ikiwa bado kwenye runway kule uwanja wa ben gurion israel rada zake zinaiona,
ishu hapa marekani,na russia na pia russia na israel wana memorandum of understanding kuwa killa marekani akitaka kufanya operation lazima kuitaarifu Russia ili kuepuka kutokea ajali,
na vilevile israel hawezi kufanya operation syria bila kuitaarifu russia.

Sasa russia akitaarifiwa inabidi astand down,

ndo maana hata jana nusu saa kabla ya shambulio marekani akatoa taarifa ,ila akawa mjanja kutoa taarifa kwa kamanda wa russia aliepo syria,lakini russia kama kawaida akawapa warning syria,kisha akastand down,

ndo maana leo mrusi alipoamua kujitoa katika makubaliano marekani wameshinda wanambembeleza kwani wanajua sasa itakuwa ngumu kufanya kazi zao syria kwa usalama,
russia imerudisha mawasiliano hayo jioni hii
Acha fix mkuu mbona mapuvu yanakutoka sana
 
9f12b672c8bc01eaefd03fc0ee0f4237.jpg
kinachoendelea sasa hv huko UNSC
Baloz wa US kasema wanaweza kuendelea kupiga mda wowote pale inapobidi.
Thubutu! hawezi kurudia tena! Marekani keshapewa red warning that "strike at your own risk"!
 
Watu mko kishabiki zaidi, hebu soma kwnye hiyo italic bold mark.

The S-400 Triumph missile system and the Pantsir complex, which is a short to medium range surface-to-air missile and anti-aircraft artillery weapon system, are ensuring the protection of Russia’s Air Force at the Khmeimim airbase in Syria, Defense Ministry spokesman Major-General Igor Konashenkov told the media on Friday.

The S-300 missile systems were deployed at Syria’s port of Tartus in 2016, to provide protection for both the base and Russian military ships in Syrian waters.

Source rt.
Leo mtaongea yote... Ukweli mchungu bwana mkubwa kamvua pajama kibabu putin
 
Hivi unajua kingetokea nini kama asingezima mitambo yake?
Ni kuwa Marekani aidha wangeamua wasishambulie au wangeanza kwanza kuishambulia mifumo ya ulinzi wa anga ya urusi! Wakifanya hivyo maana yake ni kuwa wameanzisha vita na urusi! Hakuna kichaa marekani mwenye ubavu wa kuanzisha vita na urusi!
SAA hii sehemu kubwa ys ulaya na marekani ingekuwa ni majivu!
Hahahaha ushabiki mwingine bhana!!!
 
kwanza si kweli kuwa marekani iliarifu urusi kabla ya shambulio. zipo nchi zilizoarifiwa moja wapo ni Israel. urusi hakuarifiwa na marekani wamesema shambulizi limetekelezwa 'without russia approval'

kuhusu kurudia au kutokurudia kwa shambulizi hiyo itategemea na mienendo ya huyo dem wa urusi (syria).
Naona wewe hii habari hujaifuatilia au lugha ya malkia inakupiga chenga! Fatilia habari hii aidha CNN au BBC! kama chanzo cha habari! Kusema kuwa marekani hawakuwaarifu urusi kabla ya shambizi kila mtu atakushangaa!
 
Iran naye aliuziwa hiyo mitoy S-400 sijui huko aliko anajisikiaje kusikia wanaume wamefanya yao.
Inaonyesha babu putin kuhusu hizi s 200, s300, s400 Kawaingiza watu Choo cha kike... Juzi Israel kaingia msalani.... Leo bwana mkubwa kaingia sebleni Yaani ni hatari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom