Fikraduni,
Mimi nadhani Azimio la Arusha halikufa kwa sababu ya kutokueleweka. Lilipata umaarufu lililonao kwa sababu ya kutangazwa. Viongozi wetu waliamua kulizika sio kwa sababu ya kutokulielewa, bali hawakupenda lilichosimamia. Kumbuka ndani ya Azimio la Arusha ilikuwemo Miiko ya Uongozi ambayo haifanani na matendo ya viongozi wa sasa. Azimio la Arusha lilipinduliwa na Azimio la Zanzibar. Ninajiuliza swali kwamba, Azimio la Arusha na lile la Zanzibar lipi lilitangazwa au kujadiliwa sana? Hivi watu walipata nafasi ya kiliunga mkono au kulipinga? Lakini lipi linashamiri sana na kukumbatiwa na viongozi waliomwengi? Hata hivyo, ni lipi lililenga kulinda maslahi ya wananchi?
Nakubaliana na wewe kuwa Kiswahili kilifanikiwa kwa sababu ulizozitaja. Kumbuka kwenye Kiswahili hakuna ulaji. Kama kukua kwa Kiswahili kungekuwa na mahusiano ya moja kwa moja na kubana bana watu kuhusu suala la mlo, kingekwisha zikwa zamani. Hawa viongozi tulionao siwaamini kabisa. Tajiri akiwaambia kuwa siwapi fedha mpaka Kiingereza iwe ndio lugha ya Taifa, watafuta mitaala yote mashuleni. (Joke). Hata hivyo, Kiswahili kulikuwa kupitia juhudi za makusudi zilizofanywa na Viongozi pamoja na wananchi. Ngoma, Nyimbo, Maigizo, Ngonjera, Majigambo, Vitabu vya hadithi na simulizi za kale, Bendi za muziki, mashuleni, etc. Fikraduni, umekwisha fika Tanzania na ukasikiliza nyimbo za kizazi kipya na ukajaribu kuweka maono ya mwelekeo wa Kiswahili baada ya miaka 40 kuanzia sasa?
Nyamgluu
Hizo takwimu zinavutia sana kuzisoma. Hata hivyo, zimetolewa kwa ujumla sana kiasi kwamba haieleweki kati ya hizo bidhaa zinazonunuliwa na China, Tanzania kama nchi inapata kiasi gani? Au ni watanzania wangapi wanamiliki migodi ya maana ya Dhahabu? Hii migodi si ilibinafsishwa na hawa waheshimiwa wanaishia kulipa asilimia 3 ya mapato yao kwa sasa. Hata tukiuza dhahabu China yenye thamani ya $17 Million, tunaweza kusema nchi yetu inanufaika na huu uuzaji? Mimi nadhani Makaburu, Wamarekani, na Wakanada ambao wanamiliki hii migodi ndio wanapaswa hasa kufurahia hizi takwimu. Hivi kuna wakulima wa kawaida wanaomiliki mashamba ya Mkonge?
Hata hivyo, naona kuna mazao na mbegu za kila aina. Labda hii inaweza ikawanufaisha wananchi wa kawaida.