Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,316
- 24,183
Hii ajali ya majuzi, treni kuacha njia baada ya mvua kubwa, limeniacha na maswali ambayo lazima yajibiwe.
Baada ya ajali mbaya ya train na MV Bukoba zilizotokea miaka ya My Mkapa, Awamu ya pili, nilitegemea tutakuwa kumetengenezwa Standard Operatinal Procedures kwa kuendesha hivi vifaa vyetu vya mass transport.
Haingii akilini kuwa reli haikaguliwi KILA KABLA YA SAFARI.
Na haingii akilini kuwa ma Station Master kati ya vituo vikubwa viwili vya karibu hawakuwasiliana.
Na haingii akilini kuwa dereva wa train hakuwa na weather reports, na hali ya mito mbele ya safari yake.
Haingii akilini vile vile kwamba kusafiri kwa reli za TRC is a question of chance, kufika safari yako ni majaaliwa.
Hata yote, TRC inapaswa kuyajibu.
UPANDE WA TRC
÷÷÷÷÷÷÷÷÷÷÷÷÷÷
MAELEZO YA CHANZO CHA AJALI
======================
Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha uhusiano cha Shirika la Reli Tanzania (TRC), Jamila Mbarouk treni iliyopata ajali juzi ilikuwa na abiria 720, mabehewa ya abiria 10 na ya mizigo mawili, jumla 12.
Alisema treni hiyo iliwasili Dodoma saa 9:15 alasiri na iliondoka saa 11:40 jioni. “Treni iliwasili katika kituo cha Kigwe saa 12:25 na kuondoka saa 12:27,” alisema.
ADVERTISEMENT
Jamila lieleza kuwa baada ya kuondoka kituo cha Kigwe ndipo treni hiyo ilikwenda kupata ajali baada ya injini yake na mabehewa sita ya abiria kuacha njia.
Chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa ni mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia juzi na maji yalifurika hata kusomba kokoto juu ya tuta la reli na kuiacha inaning’inia, hivyo injini ya treni iliyumba na kupinduka ikifuatiwa na mabehewa sita.
“Kwa sasa hicho ndio tunachoweza kuwaambia lakini baada ya uchunguzi kamili wa tukio hili tutatoa taarifa kwa wananchi,” alieleza Jamila.
Mwananchi Newspaper

YAH: TAARIFA YA AJALI YA TRENI B17 NA KICHWA CHA TRENI CHENYE NAMBA 9004
Dar Es Salaam Tarehe 3 Januari 2021
Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Unasikitika Kutangaza tukio la Ajali lilitokea Maeneo ya Kigwe-Bahi umbali wa Kilomita 508 Kutokea Dar Es Alaam na Kilomita 58 Kutokea Dodoma, Treni hiyo ilikuwa inatokea jijini Dar Es Salaam ikielekea Mikoa ya Tabora, Katavi (Mpanda), Kigoma na Mwanza ikiwa na Abiria wapatao 720.
Treni hii iliwasili Dodoma majira ya saa 9:15 alasiri na Kuondoka Dodoma majira ya Saa 11:40 Jioni. Treni hii iliwasili katika kituo cha Kigwe majira ya saa 12:25 Jioni na Kuondoka saa 12:27 Jioni.
Treni hii ilikuwa na Behewa 12 na kati yake Behewa 6 ndizo zilipata ajali Usajili wake ni kama ifuatavyo:
TCB 3603 ya kwanza kutoka kwenye kichwa cha Treni
TCB 3612 ya Pili kutoka kwenye kichwa cha Treni
TCB 3652 ya tatu kutoka kwenye kichwa cha Treni
TCB 3650 ya Nne kutoka kwenye Kichwa cha Treni
TCB 3619 ya Tano kutoka kwenye Kichwa cha Treni
Na ya Mwisho ni yenye Usajili wa Na. RCB 4526.
Mpaka sasa Majeruhi ni 66 na waliopoteza maisha ni watatu (3), akiwemo mtoto mmoja (1) na watu wazima wawili (2).
Majeruhi wamekwisha chukuliwa eneo la Tukio na wanaendelea na matibabu katika
Hospitali za Bahi na hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Uchunguzi wa Chanzo cha ajali unaendelea kufanyika na Shirika litaendelea kutoa Taarifa.
Uongozi wa Shirika la Reli unatoa Pole kwa Abiria wote waliofikwa na ajali, Majeruhi na Ndugu na Jamaa waliopoteza Wapendwa wao.
View attachment 1666115