Taarifa ya ajali ya Treni katika eneo la Bahi jijini Dodoma

Tanzania Railways Corp

Verified Member
Mar 23, 2018
159
500
YAH: TAARIFA YA AJALI YA TRENI B17 NA KICHWA CHA TRENI CHENYE NAMBA 9004

Dar Es Salaam Tarehe 3 Januari 2021

Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Unasikitika Kutangaza tukio la Ajali lilitokea Maeneo ya Kigwe-Bahi umbali wa Kilomita 508 Kutokea Dar Es Alaam na Kilomita 58 Kutokea Dodoma, Treni hiyo ilikuwa inatokea jijini Dar Es Salaam ikielekea Mikoa ya Tabora, Katavi (Mpanda), Kigoma na Mwanza ikiwa na Abiria wapatao 720.

Treni hii iliwasili Dodoma majira ya saa 9:15 alasiri na Kuondoka Dodoma majira ya Saa 11:40 Jioni. Treni hii iliwasili katika kituo cha Kigwe majira ya saa 12:25 Jioni na Kuondoka saa 12:27 Jioni.

Treni hii ilikuwa na Behewa 12 na kati yake Behewa 6 ndizo zilipata ajali Usajili wake ni kama ifuatavyo:
 TCB 3603 ya kwanza kutoka kwenye kichwa cha Treni
 TCB 3612 ya Pili kutoka kwenye kichwa cha Treni
 TCB 3652 ya tatu kutoka kwenye kichwa cha Treni
 TCB 3650 ya Nne kutoka kwenye Kichwa cha Treni
 TCB 3619 ya Tano kutoka kwenye Kichwa cha Treni
 Na ya Mwisho ni yenye Usajili wa Na. RCB 4526.

Mpaka sasa Majeruhi ni 66 na waliopoteza maisha ni watatu (3), akiwemo mtoto mmoja (1) na watu wazima wawili (2).
Majeruhi wamekwisha chukuliwa eneo la Tukio na wanaendelea na matibabu katika
Hospitali za Bahi na hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

Uchunguzi wa Chanzo cha ajali unaendelea kufanyika na Shirika litaendelea kutoa Taarifa.

Uongozi wa Shirika la Reli unatoa Pole kwa Abiria wote waliofikwa na ajali, Majeruhi na Ndugu na Jamaa waliopoteza Wapendwa wao.

IMG_20210103_014345_291.jpeg
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,683
2,000
Picha ya reli inaonesha kuwa kulikuwa na mmomonyoko kwenye reli hii inamaana reli haikufanyiwa ukaguzi kabla treni kuondoka stesheni ya mwisho.

Maelezo marefu ya shirika la reli tayari yanaonesha udhaifu wenu mliougundua wa kutoikagua reli kabla ya treni kuondoka na ni wazi uongozi wa shirika unawajibika kwa hili.
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
11,859
2,000
Uchunguzi wa nini sasa, hivi inahitaji rocket science kujua kuwa maji ya mvua yakiondoa udongo na kokoto kwenye reli treni itaanguka⁉️😤😤😤😤

Mnakera mno; mnawekaje taarifa bila kuonesha watu wanawezaje kufuatilia progress⁉️, nani anapaswa kuulizwa in the event anafuatilia alipo ndugu wake⁉️
 

JFK wabongo

JF-Expert Member
Aug 11, 2015
3,891
2,000
Mwaka jana nilisafiri kwa treni kwenda moshi, treni ilitarajiwa kufika saa 2 asubuhi lakini tulifika saa saba mchana. Sababu ya kuchelewa ilikuwa ni kusimama simama kwa treni kisa NYASI ZIMEFUNIKA RELI hasa baada ya stesheni ya Korogwe. Niliona ni uzembe wa stesheni masters wa vituo vile na kutokujali maisha ya abiria. Kufyeka nyasi tu kunawashinda?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom