Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,333
- 24,227
Comrade Kinana amepasua jipu.
Hili lilikuwa halisemwi na viongozi wengi maana Polisi ni chombo nyeti cha Ulinzi na Usalama.
Lakini vitendo vya Askari wetu wa Traffic vimekithiri kwa fines zinazoingizia serikali mapato na vile vile hela ya pembeni wanayopata askari.
Ni jambo la kawaida sasa ukisafiri kwa mfano kila mahali pa speed limit 50km/hr, basi yupo askari wa kupiga fine.
Mimi binafsi nimesafiri nchi ya Zimbabwe na niliingia vijijini kama kilometa 400 na mwenyeji wangu. Hatukuwahi kuona Traffic barabarani, bali askari wa check points ambao wanakuuliza kama mko salama na unaendelea na safari yako.
Comrade Kinana ambacho hakuenda mbali ni kwamba, hao askari wanotoza fine za serikali na za kwao binafsi iko hivi:
- Malori yanatozwa shs 1-2000/= kumalizana. Kama hapo njiani yanapita malori 200 kwa siku hapo ni 400,000
- Magari madogo ni 5-10,000/= kumalizana na kama yatapita magari 400 basi kwa siku askari anaweza kupata si chini ya milioni 1-2.
- Mkicheki vizuri askari anayekusimamisha haji na Defender bali gari lake binafsi analilificha vichakani-si mbali na anapo kamua mapato.
Kuna hisia kuwa mapato hayo kwa siku, wakubwa Traffic hata wakubwa zaidi wanapelekewa mgao ili vijana walindwe kikazi.
Vilevile kuna tetesi ya kiongozi wa ngazi za juu Polisi kuwa na ukwasi wa kutisha, ambapo hizi "fine" za barabarani zikiwa moja ya vyanzo vya ukwasi.
Hapo nyuma tulisitushwa na kauli ya kuruhusu hii rushwa, wakati Magufuli akiwa Rais, alisema ati hii ni hela ya kiwi!
Nampongeza Comrade Kinana kwa kulisemea hili tatizo la Traffic.
Ni wakati muafaka sasa, kwa serikali kujitathmini na jeshi lake la Polisi kitengo cha Traffic kukomesha kero ya wazi ya rushwa na usumbufu mkubwa barabarani.