Kuna mengi ambayo askari wa usalama barabarani wa Tanzania wanapaswa kujifunza kutoka kwa wenzao wa Rwanda

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,772
2,171
Nimerudi juzi Jumapili kutoka Kigali, Rwanda ambako nilikwenda na wenzangu 3 kwa shughuli za biashara. Tulikwenda kwa usafiri wa gari binafsi. Tulikaa huko siku 3. Nilishuhudia kitu kimoja kuhusu traffic polisi wa huko, jambo ambalo lilinifanya nitafakari na kulinganisha na traffic polisi wa huku kwetu.

Mara tu tulipovuka mpaka wa Rusumo na kuingia Rwanda, hatukuwahi kusimamishwa hata mara moja na maaskari usalama barabarani kwa kuulizwa hiki wa kile kwa siku zote tulipokuwa huko. Kila tulipowaona hawa maaskari tuliona wako mkao wa kusaidia au kuelekeza mwenendo wa magari kuliko kusimamisha na kuanza kutukagua.

Hapa kwetu traffic polisi wanapoona gari lenye usajili wa nchi za nje hiyo inakuwa sababu tosha ya kukusimamisha na kuanza kuuliza kama gari imeingia kihalali, kama lina ile "Yellow Card" au maswali mengine.

Nilimwuliza mwenyeji wetu tofauti niliyoiona kuhusu hawa traffic polisi. Mwenyeji wetu ambaye ana uzoefu mkubwa na matraffic wa kwetu alicheka na jibu lake lilikuwa hivi:" Falsafa ya maaskari usalama barabarani wa huku ni kwamba wanachukulia kwamba gari lolote lililo barabarani liko sawa na halina hitilafu yoyote. Pia wanaamini dreva wake ana leseni iliyo hai, na anaendesha aikiwa hajalewa, n.k.

Hivyo basi kwa mujibu wa falsafa hii, hawa maaskari huwa hawana utaratibu wa kukusimamisha hadi, kwa mfano waone unaendesha "recklessly" au kwa sababu yoyote ile", kuna mengi ambayo maaskari usalama barabarani wanayo ya kujifunza kutoka kwa wenzao wa Rwanda.
 
Tatizo hawa wa kwetu huku hawapo kazini bali wapo kwenye miradi yao. Kila gari kwao ni fursa ya kuvuna faida.

Trafic ananunua kiwanja na kuweka target kuwa kila siku apate pesa ya tofali 1000, hapo anaingia barabarani na mission moja tu, kutimiza kiasi alichojipangia.

Miaka kadhaa nyuma niliwahi simamishwa na traffic cop wa kike, alikaguwa kila kitu kwenye gari na kuona kipo sawa.

Alipokuwa anataka kunirudishia leseni akaona sandals zangu zipo upande wa kiti cha abiri na miguuni sikuwa na viatu. Nilivivua maksudi baada ya kumuona kabla hajanisimamisha.

Akasema nina kosa la kuendesha gari nikiwa nimevaa sandals zisizokuwa na mikanda ya nyuma. Nikamwambia aangalie vizuri viatu vilipo na mimi nilipo. Akasema basi nina kosa la kuendesha gari bila viatu. Nikamwambia anionyeshe sheria inayokataza mtu kuendesha peku.

Yule dada bila aibu akasema aidha nimpe pesa ya chai ama aniandikie fine ya 30,000. Nikamwambia andika fine ila elewa kuwa nina dashcam ambayo imerekodi maongezi yote hapa ikiwemo ya wewe kunipa option ya kukuhonga ama kuandikiwa fine.

Aliishia kunitupia leseni yangu tu na msonyo juu.
 
The hedge is always greener on the neighbour's side. Bora wetu wanakusimamisha na kusema shikamoo, Rwandaburundi miaka haijabita 20 walikuwa wanakusimamisha na kukuua kutokana na lafudhi yako. Isitoshe, Nji nzima ni ndogo kuliko mkoa wa Pwani, huwezi kulinganisha mnyo wa tembo. Ila kaduna ubaya kama ukihamia huko, majuzi Kagame alisema hauhitaji visa. Nenda.
 
Wajifunze wakati wako kwenye maokoto? Ukiambiwa wanavyo pangiwa oesa za kurudisha ofisini kwa boss wao utaomba kuhama nchi.
 
Kuna wakati mmoja kabla ya Pasaka nilisimamishwa na mmoja wa hao jamaa zetu. Alinistua kwa kuniambia kuwa anaomba kunikamata. Wao wanachojua hakuna gari ambalo halina kosa kabisa. Alianza na triangle, nilikuwa nayo. Akaenda kwenye fire extinguisher, nilikuwa nayo. Akaenda kwenye BIMA, akaona ipo sawa.

Akacheki leseni, ilikuwa poa. Cha mwisho kilichonishangaza zaidi akaniambia niweke hand break, nikaweka. Pamoja na kwamba taa za hiyo handbrake ilionesha uwepo wake, jamaa alitunisha misuli na kuanza kulisukuma gari langu ili kujidhirisha kama kweli hiyo break inafanya kazi. Kwa mshangao akashindwa kuliondoa hapo liliposimama! Unaweza kubashiri nini kilichotokea baada ya haya yote na utakuwa hujakosea!
 
Tatizo hawa wa kwetu huku hawapo kazini bali wapo kwenye miradi yao. Kila gari kwao ni fursa ya kuvuna faida.

Trafic ananunua kiwanja na kuweka target kuwa kila siku apate pesa ya tofali 1000, hapo anaingia barabarani na mission moja tu, kutimiza kiasi alichojipangia.

Miaka kadhaa nyuma niliwahi simamishwa na traffic cop wa kike, alikaguwa kila kitu kwenye gari na kuona kipo sawa.
Alipokuwa anataka kunirudishia leseni akaona sandals zangu zipo upande wa kiti cha abiri na miguuni sikuwa na viatu. Nilivivua maksudi baada ya kumuona kabla hajanisimamisha.

Akasema nina kosa la kuendesha gari nikiwa nimevaa sandals zisizokuwa na mikanda ya nyuma. Nikamwambia aangalie vizuri viatu vilipo na mimi nilipo. Akasema basi nina kosa la kuendesha gari bila viatu. Nikamwambia anionyeshe sheria inayokataza mtu kuendesha peku.

Yule dada bila aibu akasema aidha nimpe pesa ya chai ama aniandikie fine ya 30,000. Nikamwambia andika fine ila elewa kuwa nina dashcam ambayo imerekodi maongezi yote hapa ikiwemo ya wewe kunipa option ya kukuhonga ama kuandikiwa fine.
Aliishia kunitupia leseni yangu tu na msonyo juu.
Mkuu..traffic police nao wanatumwa na vigogo wao, pesa anayo daka kuna kiwango fulani anapeleka kwa boss wake...huo mtandao upo na umeshika Mizizi

Ole wako sasa usipopeleka mgawo, utatolewa Road na kupelekwa Linda benki au utatupwa katavi huko ndani ndani huko uchome mahindi

Ova
 
Jana ilibidi nimtafute Polisi wa Traffic Dar nimwulize jina la ZonalTraffic Officer wa Dar nikaambiwa ni Afande William! Sijui kama ni kweli na kama yupo kazini? Huyu Polisi niliyemwuliza alikuwa Raha Towers anatafuta madereva wenye makosa wanaotokea mzunguko uliopo Peugeot House kuja Raha Towers, wakati hapo aliposimama mataa ya Maktaba hayafanyi kazi na magari yamekorogana! Yeye anaona hahusiki na kukwamua huo mkorogano anaendelea kutafuta makosa ya madereva. Traffic wa siku hizi za SSH ama wanatafuta hela au wanapitisha viongozi wao wapite haraka, basi! Ni polisi wa ajabu kabisa!
 
Tatizo hawa wa kwetu huku hawapo kazini bali wapo kwenye miradi yao. Kila gari kwao ni fursa ya kuvuna faida.

Trafic ananunua kiwanja na kuweka target kuwa kila siku apate pesa ya tofali 1000, hapo anaingia barabarani na mission moja tu, kutimiza kiasi alichojipangia.

Miaka kadhaa nyuma niliwahi simamishwa na traffic cop wa kike, alikaguwa kila kitu kwenye gari na kuona kipo sawa.
Alipokuwa anataka kunirudishia leseni akaona sandals zangu zipo upande wa kiti cha abiri na miguuni sikuwa na viatu. Nilivivua maksudi baada ya kumuona kabla hajanisimamisha.

Akasema nina kosa la kuendesha gari nikiwa nimevaa sandals zisizokuwa na mikanda ya nyuma. Nikamwambia aangalie vizuri viatu vilipo na mimi nilipo. Akasema basi nina kosa la kuendesha gari bila viatu. Nikamwambia anionyeshe sheria inayokataza mtu kuendesha peku.

Yule dada bila aibu akasema aidha nimpe pesa ya chai ama aniandikie fine ya 30,000. Nikamwambia andika fine ila elewa kuwa nina dashcam ambayo imerekodi maongezi yote hapa ikiwemo ya wewe kunipa option ya kukuhonga ama kuandikiwa fine.
Aliishia kunitupia leseni yangu tu na msonyo juu.
Mimi nilimkazia mmoja pale check point ya igumbilo Iringa. Nilipakiza Mgonjwa na ndugu zake kwenye Gari hizi SUV. Walikuwa ndugu 4 na mgonjwa wakawa 5. Jamaa akanisimamisha na kunidai leseni. Nikamwambia sina, akakagua gari na kuniambia nimezidisha abiria. Baada 4 sasa wapo 5 so nitoe faint.

Nikamueleza hawa waliniomba lift na wana huyu mgonjwa wanampeleka Hospitali. Jamaa kakomaa nami nikamwambia, sina lesseni wala sina hata 100. Shwria imasemaje kama sijatembea na leseni? Akasema nimepe cash nikamwambia sina hata 100. Nikakaza pale alafu nikamwambia mi Mtumishi mwenzio wa serikali so unatakiwa uni handle vizuri. Jamaa akaogopa kwani nilikuwa nimevaa hizi kaunda suti akajua ni wale jamaa.

Akaniruhusu
 
Rwanda uzuri wameweka madhine barabarani. Ukikosea , ile madhine inatoa ujumbe kwa traffic police. Madereva wengi wa Tanzania wanapata shida.
 
Sheria ya kwetu ipo sawa kabisa na hiyo falsafa za askari wa huko ulikokuwa!

Tofauti ya kwetu na huko ni MFUMO WA RUSHWA!

Kama kuanzia nyumba nyeupe, mjengoni, wizarani, halmashauri n.k watu ni wapigaji traffic police ye ni nani asipige? Tena wana mfumo wao wa maokoto wanauita KIBATI!

Kuna kipindi lilisikika tamko kuwa waendelee kukusanya za kiwi!
 
Tatizo hawa wa kwetu huku hawapo kazini bali wapo kwenye miradi yao. Kila gari kwao ni fursa ya kuvuna faida.

Trafic ananunua kiwanja na kuweka target kuwa kila siku apate pesa ya tofali 1000, hapo anaingia barabarani na mission moja tu, kutimiza kiasi alichojipangia.

Miaka kadhaa nyuma niliwahi simamishwa na traffic cop wa kike, alikaguwa kila kitu kwenye gari na kuona kipo sawa.
Alipokuwa anataka kunirudishia leseni akaona sandals zangu zipo upande wa kiti cha abiri na miguuni sikuwa na viatu. Nilivivua maksudi baada ya kumuona kabla hajanisimamisha.

Akasema nina kosa la kuendesha gari nikiwa nimevaa sandals zisizokuwa na mikanda ya nyuma. Nikamwambia aangalie vizuri viatu vilipo na mimi nilipo. Akasema basi nina kosa la kuendesha gari bila viatu. Nikamwambia anionyeshe sheria inayokataza mtu kuendesha peku.

Yule dada bila aibu akasema aidha nimpe pesa ya chai ama aniandikie fine ya 30,000. Nikamwambia andika fine ila elewa kuwa nina dashcam ambayo imerekodi maongezi yote hapa ikiwemo ya wewe kunipa option ya kukuhonga ama kuandikiwa fine.
Aliishia kunitupia leseni yangu tu na msonyo juu.
Ukiona cop wa kike next time kuwa makini... Wengi wao ni prey!
 
Dhamira ya uzi sio kuwaattack traffic wa tz Bali ni kutuambia umetoka kigali it's okay aya sema fursa za kibiashara uko ulikotoka zikoje?
Muwe mnaficha mambo yenu ya kichoko hivi ungekaa kimya na kujifunza mambo yakoje Rwanda ungepungukiwa na nini?wewe unaona Kigali kitu Cha ajabu sana eeh nyoko gulefu wewe kama huna hoja Kaa kimya Pussy!!!
 
Tatizo huku njaa baba hapa nilipo nishasimamisha gari za kutosha
Hapa kwetu njaa na uhuni wa police wetu,nakumbuka nami nilikwenda Rwanda nilikaa kama mwezi but siku naingia pale Rusumo njiani sikusimamishwa popote sana sana trafiki walikuwa wakinionyesha kwa ishara ya mikono kuwa niende mdogomdogo, Kigali siku za mwanzo nilikuwa nasahau nachanganya letf na right hasa ukiwa roundabout but ukikosea hata dereva akiona T anacheka na kukuelekeza mkono wako.

Ila nadhani traffic wa Kenya wale ndio hatari zaidi na majangiri kupita maelezo,wale ukikamatwa na overspeeding hawaombi Rushwa bali wale wanakunyanganya Rushwa tena kubwa, wana zile mahakama za njiani wanazitumia kukutishia na kweli ukigoma utakutana na court na ukizingua zaidi unaweza jikuta mahabusu
 
Kwetu ni ufisadi (corruption) iliyotuharibu.

Nchi nzima inanuka rushwa na bado hatuchukuwi hatuwa stahiki kuitokomeza rushwa.
 
Tatizo huku njaa baba hapa nilipo nishasimamisha gari za kutosha
Kwani askari wa Rwanda wanalipwa mishahara mikubwa sana?!! Tena ni kidogo kuliko hawa wa kwetu, sema ni kuendekeza tu, na hiyo ni kutokana na mfumo mzima kuoza!! Kama ni njaa mgekuwa DRC, si mgekuwa mnauza na magari ya watu kabisa?!!
 
Back
Top Bottom