Waziri Masauni anapwaya! Trafiki wanajiamulia cha kufanya, magari yanajiendesha

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411
aaaa.jpeg

aa.jpeg
aa.jpeg

aaa.jpeg


Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye jeshi la Polisi limo ndani yake anaonekana kufeli pakubwa na so far Mama Samia anamvutia pumzi.

Waziri Masauni, ama kwa kujua ama kutokujua kuna makosa makubwa sana anayofanya. Watu kadhaa wanahofiwa kufariki baada ya ajali iliyohusisha gari aina ya Fuso (T 861 ASN) lilikiwa likivutwa na BREAK-DOWN kwa mnyororo kufeli breki na kugonga Bajaji, Pikipiki pamoja na Muuza magazeti katika kituo cha mabasi cha Ubungo Maji, Dar es salaam.

Ajali hiyo imetokea leo katika barabara ya Morogoro ambapo imeshuhudia hatua za uokoaji zikiendelea huku ikiendelea kuzitafuta Mamlaka husika kuhusu taarifa za Mashuhuda juu ya uwepo wa vifo katika ajali hiyo.

Saa tatu Kasoro asubuhi nilikuwa naenda Mjini. Nilipofika maeneo ya Kimara Baruti, nikaona Fusso mbovu inavutwa na BREAK-DOWN mbovu iliyochakaa tena kwa mnyororo chakavu.

Nikamwambia dereva wa Bolt asikie karibu naye na kusema uvutaji wake ilikuwa hatari. Fuso gani inavutia na nyororo. Polisi walikuwa wapi? Polisi waapo barabarani kukamata Kirikuu na kukusanya kodi kwa niaba ya TRA badala ya kuanagalia usalama.

Bodaboda na Bajaji kwenye hii Morogoro Road zipigwe marufuku, imekuwa hatari sana. Tatizo magari hayafanyiwi check up, POLISI NA TRAFFICK wanaseoma nunua stika ya wiki ya NENDA KWA USALAMA BARABARANI , unanunua stika badala ya gari kukGuliwqa. Daladala za Mwananyamala -Posta- Stesheni zikikaguliwa nata na mwanafunzi wa VETA wiki ya kwanza hakuna itakayobaki barabarani.

Dalalda za MASAKI -KARIAKOO zimeoza kabisa, ila kwakuwa wamiliki wengi ni wale jama wa Oysterbay -Poli-polii hazikamatwi, hazikaguliwi lakini hebu IGP na Waziri wa Mambo ya Nakwambieni uhai wetu ni muhimu kuliko maokoto ambayo yanatumika kutuzika. Tanzania magari au uhai wa mtu kwao sio cha maana kwao cha maana pesa shenzi kabisa corrupt system inatutesa tunazidiwa hadi na nchi zenye vita

1. Kuwaacha Traffick Polisi kugeuka kufanya kazi ya TRA, wanaweka Camera na vizuizi njiani kukagua madeni ya Gari zilizopigwa faini , imagine kila baada ya siku 7 faini inaongezeka nusu nzima, Sasa mtu anayetoka Dar kwenda Msibani Bukoba kumzika mke wake, anapigwa faini ya Tshs 30,000 kwa kukosa stika ya elfu 5: Anfika Bukoba wakati anamzika mke wake deni lionaongezeka kwa Tshs 15,000/- wakimaliza maziko akikaa matanga na kukabidhi nguo faini inafika Tshs 60,000/- Hii ni dhambi na laana kwa nchi, ni kilio cha wengi , watu wapo kimya lakini si vyema kabisa na credibility ipo chini sana.

2. Polisi wamejikita karibu nchi nzima kila asubuhi kusimamisha daldala na dereva ama utingo kushuka na kwenda kumshika traffick mkono, haijulikani hiyo salamu in maana gani, ila gari haikaguliwi.Abiria wanachelewa makazini, hospitali na mabasi ya mikoani , iweje kila siku ya Mungu gari inasimamishwa

3. Polisi /Traffick wamegeuka kero kuliko Nzi anayeingia kwenye sharubati mghahawani. Umeme ukikatika hawajishughulishi kuongoza magari bali hukjidicha kuvizia gari zinazopita na red-lights. Umeme ukirudi nao ndio wanarudi kwenye mataa kuongoza magari(kuvuta gari).

4. Traffick wa Salander Plice station Wanakaa njia ya Muhimbili Hospital na Agha Khan na kusimamisha gari mpya kabisa na gari zisizo na makosa na kuanza kumwambia dereva tunafanya ukaguzi wa kawaida, huyu traffick amekaa njia ya kwenda hospitali ya Taifa, mtu una mgonjwa, unawahi mochwari kuchukua miti, unawahi daktari amekupa appoinment mtu anakuuliza triangle, stika, anazunguka akikuta hakuna kosa anakwambia niachie lunch.Masauni hivi huwa hujui kwamba watu hawaendi Muhimbili kula biriani ila wengi wanakuwa wamechanganyikiwa kuwahi wagonjwa na maiti?

5. Trafick ukikutana naye barabarani hata kama garo haina tatzo, kila kitu kipo sawa lakini dereva anaogopa na kuona kero kwakuwa anacheleweshwa tu bila sababu.

6. Bajaji za Mbezi-Kimara-Magomeni Usalama, zinapita wrong sight, zinasababisha foleni kwa kushuhsa na kupakia katikati ya barabara lakini polisi wamewaachia huku wakikimbizana na magari.

BARAZA LA USALAMA BARABARANI LINASTAHILI KUWEPO? WAJUMBE HAWAUMII ROHO KWA YANAYOENDELEA?

Baraza hili linaundwa :-
1. Mwenyekiti- JNAIBU WAZIRI JUMANNE SAGINI
2. Makamu Mwenyekiti, NAIBU W-UJENZI GODFREY KASEKENYA
3. wajumbe wasiopungua 10
4. Katibu wa Baraza huwa ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Tanzania.

MAPUNGUFU YA BARAZA
1. Hakuna sifa za mtu kuteuliwa katika hizo nafasi 10, wengi wanaoteuliwa ni wamiliki wa malori, mabasi na wafanyabiashra wakubwa Tanzania.
2. Baraza linafanya kazi kwa mazoea, hakuna impact yeyote .

KAZI ZA BARAZA
Kwa mujibu wa kifungu cha 97 cha sheria ya usalama barabarani kazi kuu za baraza ni zifuatazo:
(a) Kuwa chombo kikuu cha kusimamia shughuli zote za kuimairisha usalama barabarani na kutumia maarifa na uzoefu uliopo kuhusu usalama barabarani;
(b) Kuhamasisha tafiti kuhusu vyanzo vya ajali;
(c) Kuhamasisha tafiti za kitakwimu kuhusu idadi,aina, na gharama za ajali za barabarani;
(d) Kwa kutumia takwimu za kitafiti zilizopo kubaini vyanzo vya ajali na kutoa mapendekezo ya jinsi ya kukabiliana na tatizo la ajali;
(e) Kutambua viashiria vya ajali, kubuni na kupendekeza hatua xa kuchukuliwa na kushauri mamlaka husika kuchukua hatua;
(f) Kutoa mapendekezo ya kurekebisha sheria ya usalama barabarani kwa lengo la kupunguza ajali za barabarani;
(g) Kutoa hamasa na mafunzo na elimu kwa watumiaji wa barabara;
(h) Kukuza uelewa wa watumiaji wa barabara kuhusu vihatarishi mahsusi, namna vinavyotokea na namna ya kukabiliana navyo;
(i) Kujenga fikra chanya kwa usalama barabarani kupitia mihadhara, vielelezo; kampeni, au kitu kingine chochote;
(j) Kukusanya, kuandaa, na kusambaza machapisho mbalimbali ya kielimu kuhusu usalama barabarani;
(k) Kuandaa na kusambaza program mbalimbali za taarifa kwa umma na kuzitangaza kwa njia ya vyombo vya habari;
(l) Kushauri kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo uundaji wa magari, matela, vifaa na matengenezo yahusuyo vyombo vya usalama barabarani;
 
Back
Top Bottom