Kumekuwa na hali ambayo haileweki ndani ya jeshi la polisi upande wa usalama barabarani ambapo unaletewa meseji kwenye simu kwamba umepigwa faini na unaandikiwa na kosa lako wakati huo wewe upo Dar es salaam na gari halijaenda popote siku nzima wewe upo nyumbani.
Ukiingia kwenye mtandao wao wa tms.tpf.go.tz unasachi gari yako unaona kweli umeandikiwa kosa kwa muda huo lakini unakuta kosa hilo limefanyikia mkoani. Ukienda kuripoti tatizo hilo unaelekezwa uende traffic Central ili tatizo lako liweze kushughulikiwa na kitengo kinachohusika na malalamiko kama hayo.
Hapo sasa unaanza kuzungushwa kwani unaambiwa uache namba ya simu watalishughulikia na wanakueleza uwapigie kuwakumbushia. Sasa ukishaondoka hapo baada ya siku chache ukimpigia yule mhusika hapokei tena simu yako na ukitazama kwenye mtandao deni liko palepale.
Tunaomba wakuu wanaohusika ndani ya Jeshi letu la Polisi walitazame jambo hili la kubambikiwa faini kwani linawanyima raha wananchi wanaotumia vyombo hivi na kuwafanya wakose imani na jeshi lao la polisi ambalo tunaamini kuna maeneo wanafanya kazi vizuri sana.