Traffic wanabambikia watu faini, unaletewa meseji kwenye simu kwamba umepigwa faini na gari halijaenda popote

senzighe

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
1,978
1,511
Kumekuwa na hali ambayo haileweki ndani ya jeshi la polisi upande wa usalama barabarani ambapo unaletewa meseji kwenye simu kwamba umepigwa faini na unaandikiwa na kosa lako wakati huo wewe upo Dar es salaam na gari halijaenda popote siku nzima wewe upo nyumbani.

Ukiingia kwenye mtandao wao wa tms.tpf.go.tz unasachi gari yako unaona kweli umeandikiwa kosa kwa muda huo lakini unakuta kosa hilo limefanyikia mkoani. Ukienda kuripoti tatizo hilo unaelekezwa uende traffic Central ili tatizo lako liweze kushughulikiwa na kitengo kinachohusika na malalamiko kama hayo.

Hapo sasa unaanza kuzungushwa kwani unaambiwa uache namba ya simu watalishughulikia na wanakueleza uwapigie kuwakumbushia. Sasa ukishaondoka hapo baada ya siku chache ukimpigia yule mhusika hapokei tena simu yako na ukitazama kwenye mtandao deni liko palepale.

Tunaomba wakuu wanaohusika ndani ya Jeshi letu la Polisi walitazame jambo hili la kubambikiwa faini kwani linawanyima raha wananchi wanaotumia vyombo hivi na kuwafanya wakose imani na jeshi lao la polisi ambalo tunaamini kuna maeneo wanafanya kazi vizuri sana.
 
Kumekuwa na hali ambayo haileweki ndani ya jeshi la polisi upande wa usalama barabarani ambapo unaletewa meseji kwenye simu kwamba umepigwa faini na unaandikiwa na kosa lako wakati huo wewe upo Dar es salaam na gari halijaenda popote siku nzima wewe upo nyumbani.

Ukiingia kwenye mtandao wao wa tms.tpf.go.tz unasachi gari yako unaona kweli umeandikiwa kosa kwa muda huo lakini unakuta kosa hilo limefanyikia mkoani. Ukienda kuripoti tatizo hilo unaelekezwa uende traffic Central ili tatizo lako liweze kushughulikiwa na kitengo kinachohusika na malalamiko kama hayo.

Hapo sasa unaanza kuzungushwa kwani unaambiwa uache namba ya simu watalishughulikia na wanakueleza uwapigie kuwakumbushia. Sasa ukishaondoka hapo baada ya siku chache ukimpigia yule mhusika hapokei tena simu yako na ukitazama kwenye mtandao deni liko palepale.

Tunaomba wakuu wanaohusika ndani ya jeshi letu la polisi walitazame jambo hili la kubambikiwa faini kwani linawanyima raha wananchi wanaotumia vyombo hivi na kuwafanya wakose imani na jeshi lao la polisi ambalo tunaamini kuna maeneo wanafanya kazi vizuri sana.
5 tena
 
Bwana Senzighe hii inaitwa kuisoma namba. Huu ubeti ulikuhusu:

Kama namba mtasoma, kama tusomavyo sisi,
Awamu hii ya neema, labda kwa makasisi,
Kanda yetu ya Musoma, labda pia busisi!
Kwa kipyenga cha Senzige, Tunayeya safarini.

Kusoma namba kwani maana yake nini?
Duuh Brazaj umekuja hadi huku!
 
Beti hizo zanihusu,hakika yamenikuta
Deni lisilonihusu,labda liwe la Guta,
Limetoka Nyarugusu,Likabambikwa Toyota
Sasa unanisimanga,chondechonde Brazajei !

Upinzani wenye nguvu, Ilikuwa yao dawa,
Isingekuwa maguvu, wala full kuchachawa,
Vichwa vyao ni mafuvu, au wafugia chawa?
Walokuwa kutulinda, twamshtakia Mungu!
 
Kwani wana haja na leseni? Wao wanataka mwenye gari.

Wakikomaa na gari hela watapata.

Leseni ni collateral tu.
Mfumo wa utoaji faini ya malipo unahitaji kuwe na namba ya leseni ya dereva aiyefanya kosa barabarani
 
Mfumo wa utoaji faini ya malipo unahitaji kuwe na namba ya leseni ya dereva aiyefanya kosa barabarani

Ni kweli kuwa leseni inahitajika. Ulijiuliza kwa nini namba ya gari ihitajike? Kosa si kafanya dereva?

Kimsingi suala si kosa wala faini. Suala ni pesa. Inatakiwa pesa? Nani mwenye pesa? Inasadikika mwenye gari. Komaa na gari utapata pesa. Hesabu rahisi.

Cases za gari tied to a fictitious driving licence ni nyingi mno labda kama wewe hazija kukuta!
 
Kumekuwa na hali ambayo haileweki ndani ya jeshi la polisi upande wa usalama barabarani ambapo unaletewa meseji kwenye simu kwamba umepigwa faini na unaandikiwa na kosa lako wakati huo wewe upo Dar es salaam na gari halijaenda popote siku nzima wewe upo nyumbani.
Inawezekana ulikutwa na kosa siku tatu au saba nyuma,askari hakuwa na mashine,inampasa afike kituoni kuwasilisha data muhimu kwa waliopigwa fine.
Utaratibu ni kwamba askari anaepokea hizo data alitakiwa akupigie simu kwanza kukufahamisha kuwa anakulima fine kwa kosa ulilofanya tarehe fulani mahali fulani
Lakini pia unaweza kuangalia kwenye mtandao aina ya kosa,lilitendeka wapi na tarehe ngapi utajua tu kama gari alikuwa nalo dereva au mkeo kwa siku hiyo
 
Hapa ni rahisi.

Kwakuwa huwa wanaandika namba ya gari na leseni, waambie wakupe jina la mwenye leseni nae aitwe.

Wanaweza sema sawa ila gari wanaishikilia hadi mwenye hiyo leseni wampate.

Usisahau wana ruhusa ya kukupa gari yako bila matairi baada ya shauri!
 
Back
Top Bottom